Mshahara wa Maximo wamshangaza Mzambia
Michael Momburi,Kampala
KOCHA wa Zambia ambae juzi aliteta na Marcio Maximo kwenye hoteli Ivys, ameshtushwa na mshahara wa kocha huyo na ameomba namba ya simu ya TFF.
Herve Renard ambae ni raia wa Ufaransa, timu yake ilitolewa juzi katika hatua ya makundi ya kombe la chalenji baada ya kufungwa mabao 2-0 na Sudan.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha huyo alisema yeye analipwa dola 7000 za Marekani, lakini aliposikia Maximo analipwa dola
15,000 akashtuka na kushika mdomo.
Herve alisema kwamba amevutiwa na Tanzania baada ya kukaa na Maximo wakateta na akamuambia kwamba Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete na serikali yake wanathamini sana michezo na ndio mabosi wake.
Kocha huyo alisema kwamba anatamani kufanya kazi Tanzania kutokana na mambo aliyoyasikia.
"Hela nyingi sana hizo analipwa Maximo inaonekana mnapenda sana michezo namna viongozi wazuri,"alisema kocha huyo kijana.
"Kwani mkataba wa Maximo unamalizika lini? Nipe na namba ya Rais wa Shirikisho lenu,Tanzania ni nchi nzuri sana."
Kocha huyo baada ya kuambiwa kwamba Maximo mkataba wake unamalizika Julai na amegoma kuongeza, aliomba namba ya Rais wa TFF, Leodegar Tenga, lakini hakutaka kuweka bayana ni ya nini.
Herve ambae timu yake ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, alisema kwamba anaelekeza nguvu zake kwenye michuano ya CHAN mwezi ujao.
Source: Mwananchi Read News