Mfanye Awe Wako Peke Yako!

eRRy

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
1,125
204
1259819411_black_couple_1.jpg


Mapenzi ni sawa na bustani nzuri ya maua rafiki zangu, wakati mwingine inahitaji mbolea, kumwagiliwa maji na hata kupaliliwa...
Kwa kufanya hivyo utazidisha ladha ya mapenzi na kuyafanya yazidi kuwa na nguvu zaidi ya awali. Lakini kama hutamwagilia, hutaweka mbolea, hutapalilia, hesabu kwamba mapenzi yako yanaweza kuanza kupoteza nguvu taratibu na hatimaye kufa kabisa.

Kikubwa ambacho nimepanga kuzungumza nanyi leo ni jinsi ya kumfanya mwenzi wako awe wako peke yako. Umeshawahi kufikiria kwamba, kama ukishindwa kutimiza mambo fulani katika penzi au ndoa yako, mwenzi wako anaweza kuwa wa kushea?

Kama bado, inakubidi ufahamu hilo kuanzia leo. Mpenzi anahitaji mambo mengi ili aendelee kuwa mwaminifu kwenye penzi lenu. Ni kweli kwamba uaminifu upo kwa mtu mwenyewe, kama mtu ni mwaminifu basi atadumisha uaminifu uliopo ndani yake, lakini kama kuna mambo unakosea, lazima utasalitiwa!

Tena basi, kama mwenzi wako anakupenda, atakusaliti huku analia! Kwanini? Kwasababu analizwa ba kitendo ambacho hajapenda kukifanya ila wewe mwenyewe ndiyo umemlazimisha afanye hivyo.

NINI HUSABABISHA ZAIDI USALITI?
Tukiachana na tamaa, hulka na ushawishi, wakati mwingine mpenzi anaweza kusaliti kwa kukosa yale ya muhimu zaidi katika penzi au ndoa yake.

Kwa bahati mbaya sana, watu wa aina hii huwa hawasemi moja kwa moja kuwa wanakosa vitu fulani au wanapenda vitu fulani, badala yake hutumia lugha za ishara zaidi na kama hutaelewa basi huona suluhisho na kutafuta pumziko lingine.
Hapa sasa mwenzi wako anakuwa si wako peke yako tena! Lakini lazima uhakikishe mpenzi wako anaendelea kuwa wako bila kushea na mtu yeyote na jambo hili linawekana kabisa ikiwa wewe mwenyewe utataka iwe hivyo.

Zipo hatua au mambo mengi ya kumfanyia mpenzi wako ili awe wako peke yako, lakini hapa nitakupa yale ya msingi zaidi yatakayokusaidia katika penzi lako.

Kama inavyoonekana hapo juu, nimeyafananisha mapenzi na bustani nzuri ambayo ina mahitaji yake. Sasa katika uchambuzi huu, nitaainisha jinsi ya kuitunza bustani (penzi) yako vizuri sana na kuifanya bora zaidi kila inapoitwa leo.
Mbolea

Hapa nazungumzia penzi ambalo tayari limeshakuwa penzi! Kama ni bustani basi tayari mboga-mboga zako zimemea vizuri. Lakini ukumbuke kwamba, bustani yako haitaweza kuendelea kuwa bora kama haitakuwa na matunzo. Hapa penzi linahitaji mbolea.

Mbolea ninayoizungumzia hapa ni maneno matamu yaliyojaa huba. Fikisha hisia zako kwa mwenzi wako kwa namna ya kipekee iliyojaa penzi la dhati.

Mweleze jinsi unavyompenda na jinsi maisha yako ambavyo hayawezi kukamilika bila yeye. Huu ni wakati wako wa kumsumbua kwa meseji zilizojaa tungo za mahaba, kadi, maua na zawadi ndogo ndogo. Baadhi ya wanandoa wakishaoana, huacha utaratibu huu. Kuna wanaosema: “Ah! Hayo mambo ya kizamani bwana, kipindi akiwa demu wangu, sasa hivi yupo ndani, kwanini nihangaike?”

Haya ni makosa makubwa ndugu yangu. Shamba bila mbolea kuna mavuno kweli?

Maji!
Yes! Pia bustani yako itahitaji maji kwa ajili ya kuzidisha ustawi wa mazao yako. Hapa unatakiwa kuwa mbunifu zaidi katika mambo yanayohusu mapenzi moja kwa moja.

Unatakiwa kubadilisha aina ya ufanywaji wa mapenzi, mahali pa kukutana na hata sehemu za mitoko. Inashauriwa ili kuboresha penzi ni vizuri kutoka sehemu mbalimbali na mwenzi wako. Inapendeza zaidi angalau mara tatu kwa miezi sita, kulala na mwenzako hotelini.

Hapa utakuwa unanakshi zaidi penzi lako. Outing yako ni vyema ikawa ya kimahaba zaidi, kuanzia mavazi, sehemu mnazotembelea n.k Mfanyie mwenzi wako mambo ya kimahaba sana mnapokuwa wawili. Mbusu, mkumbatie, mwambie jinsi unavyojisikia wa pekee kuwa wake.

Palizi
Baada ya muda bustani huota majani mengine ambayo si mboga! Yawezekana kabisa, kwa bahati mbaya uchafu ukaingia bustanini. Wakati wa palizi ni muda sahihi wa kuondoa vyote hivyo.
Hata katika mapenzi pia hutakiwa kufanya jambo hili. Kugombana au kupishana kiswahili kwa wapenzi ni jambo la kawaida sana, hivyo ni vyema kuweka sawa tofauti hizo mapema, kabla tatizo halijawa kubwa zaidi. Hii ndiyo palizi ninayoizungumzia.

Usikae na kinyongo moyoni mwako, kuwa mjanja, hata kama ni yeye ndiye aliyekosea, zungumza naye ukimweleza jinsi ambavyo hupendi mgombane, mkimweleza hisia zako kwamba unatamani sana muelewane katika siku zote za maisha yenu. Weka mambo sawa.

green.gif
 
Mmmmh!!! Mapenzi yana kazi kweli wandugu
haya senks
 
eRRy84:

Mambo uliyoeleza ni mazuri sana na mtu akiyafuata, hakika atafanikiwa sana katika penzi lake.

Lakini shida inakuja kwamba watu wengi wana'rush kwenye mapenzi bila kufuata hatua hizo ulizozisema(Mbolea, Maji na Palizi).

Actualy imefikia mahali ambapo kila mtu anayeingia katika hatua ya mapenzi (hasa hiki kizazi chenu), anafanya anachojua yeye kichwani mwake, bila guidances zozote toka kwa watangulizi au miongozo kama huu wako!
 
Actualy imefikia mahali ambapo kila mtu anayeingia katika hatua ya mapenzi (hasa hiki kizazi chenu), anafanya anachojua yeye kichwani mwake, bila guidances zozote toka kwa watangulizi au miongozo kama huu wako!
Mpwa tusitiri japo kidogo Mkuu
 
eRRy84:

Mambo uliyoeleza ni mazuri sana na mtu akiyafuata, hakika atafanikiwa sana katika penzi lake.

Lakini shida inakuja kwamba watu wengi wana'rush kwenye mapenzi bila kufuata hatua hizo ulizozisema(Mbolea, Maji na Palizi).

Actualy imefikia mahali ambapo kila mtu anayeingia katika hatua ya mapenzi (hasa hiki kizazi chenu), anafanya anachojua yeye kichwani mwake, bila guidances zozote toka kwa watangulizi au miongozo kama huu wako!

Rekebisha hiyo RED kidogo mkuu
 
Mwingine utaweka mpaka mbolea za kizungu na kufunga pampu ya kumwagilia lakini atakusaliti tu!
 
Mpwa tusitiri japo kidogo Mkuu
Mmezidi Mkuu Sipo!

Kijana wa miaka 15, utamsikia ...sijui nininini demu wangu!...Pumbaaaaf!

Mi nimejua demu niko 4m 4, tena wakati wa party ya kuagana, ndo nikajikakamua ku'do!...huh!
 
Mmezidi Mkuu Sipo!

Kijana wa miaka 15, utamsikia ...sijui nininini demu wangu!...Pumbaaaaf!

Mi nimejua demu niko 4m 4, tena wakati wa party ya kuagana, ndo nikajikakamua ku'do!...huh!
Kumbe hata na wewe Mpwa uliwahi mkuu kuingia ukubwani
 


Actualy imefikia mahali ambapo kila mtu anayeingia katika hatua ya mapenzi (hasa hiki kizazi chenu), anafanya anachojua yeye kichwani mwake, bila guidances zozote toka kwa watangulizi au miongozo kama huu wako![/QUOTE]

Tatizo hapo mkubwa suala hili la mapenzi halina shule/tuition ni vile tu kasi ya mtu na akili zinavyolichukulia jambo hilo japo naamini tunaiga baadhi ya matendo fulani fulani aidha kutoka kwa waliotutangulia ama wengi wanasema eti kwenda na wakati. Cha msingi hapo mkubwa mi naona ninyi mlioelimika kwenye kitengo hicho mtoe tuition/mafunzo kwetu sisi tunaoanza kuyatafuta mapenzi kama hivi ulivyoamua kuchukua hatua hii nzuri ya kuwaelimisha raia.
 
Back
Top Bottom