Mfanyakazi wa Ubalozi wa Canada adaiwa kumtemea mate Polisi

Talking about DNA, nadhani itakuwa vyema wakamfania DNA test huyu mtasha, nahisi one of his grand grand parent alikuwa Chatu au Cobra!

Mkuu hapo nikupata vyema! Kutemea watu MATE mara mbili lazima huyo MAMA ana asili ya NYOKA au jamii ya MAJOKA
 
Na bado labda wamuhoji huyo mzungu kuna kosa gani aliloliona mpaka kupelekea kutemea mate watu ? Huenda aliombwa rushwa Tunataka source ya jambo hili
 
wazungu wanakuwa na stress za kipumbavu sana , si ajabu ukakuta alikuwa na mahasira yake ya nyumnani, can se sisi waafrika tumakuwa na uwezo wa kuvumialia stress sana , hawa wazungu vichwa vya dagaa, ingekuwa ni kwao ungekuta wameshaandamana kunako usiku wa manane, very wajinga
 
Trafiki kutemewa mate:Jeshi la Polisi launda tume


Written by Administrator Friday, 11 December 2009 11:07 Na Waandishi Wetu, jijini

KUTOKANA na kitendo cha ofisa wa Balozi wa Canada kumtemea mate askari wa kikosi cha usalama barabarani na mwandishi, Jeshi la Polisi limeunda tume ya kufuatilia kwa kina shambulio hilo.

Hayo yamesemwa na Insptekta Jenerali wa Polisi, Saidi Mwema, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo.

Amesema jeshi la polisi limesikitishwa na kitendo hicho cha udhalilishaji kilichofanywa na raia wa Canada, Jean Touchatte (48), ambaye ni Katibu Muhtasi wa ubalozi huo.

Kamanda Mwema amesema tume hiyo inaanza kazi leo na mara baada ya kukamilisha kazi yake, taarifa itatolewa kwa wananachi ili hatua ziweze kufuata na ikiwezekana raia huyo kuondolewa nchini.

Jana Kaimu Kamanda Mkoa wa Dar es Salaam, Charles Kenyela, alisema tukio hilo lilitokea juzi eneo la Banana baada ya trafiki mwenye namba E 1653, Cpl Samsoni, akiwa kazini ghafla mtuhumiwa, akiwa anatokea Ukonga kuelekea Uwanja wa Ndege akiwa na gari namba T 17 CD 178 Toyota Land Cruiser Prado rangi ya bluu mali ya ubalozi wa Canada, alifungua kioo cha gari kisha kumtemea mate trafiki huyo.

Amesema baada ya kufanya kitendo hicho raia huyo aliondoa gari kuelekea mjini ambapo askari huyo alitoa taarifa juu ya kitendo hicho na kuanza kulifuatilia gari hilo na kisha kufanikiwa kulikamata katika Barabara ya Nyerere eneo la Kamata.

Kamanda amesema muhusika huyo alipelekwa Makao Makuu ya Polisi Trafiki na wakati akiendelea kuhojiwa Mwandishi wa habari wa TBC 1, Jery Muro, alifika ili kujua sababu za raia huyo kufanya kitendo hicho cha udhalilishaji, lakini naye alitemewa mate.

Kutokana na hali hiyo, Muro alilazimika kufungua jalada la shambulio lenye namba CD /1R/ 4818/2009. Hata hivyo, mhusika huyo alipohojiwa na polisi kuhusu kitendo hicho hakuwa tayari kutoa maelezo kwa madai kwamba hadi awepo Balozi wake.












DarLeo, Powered by Business Times Ltd!
 
Huo sio utu hata kidogo. Kutokana na watanzania kudharaulika na kuomba sana misaada ndio matokeo yake hayo. Hela tunazo, wachache wanazila (mafisadi) kisha tunaenda na kibakuli kwao.
1. Kwa nini polisi hawakutumia ile kawaida yao ya kumlamba virungu na mabuti au kwa kuwa ni mzungu? Angekuwa mbongo hakika leo angekuwa Muhimbili na pingu.
2. Msitegemee kuwa atapewa adhabu kubwa sana huyo ni mzungu bwana, hii nchi kwa wazungu haisemmi japo alifanya kwa kukusudia.
 
SAFI sana. Ninadhani ofisa balozi huyo alikuwa anaonesha dharau ya juu kabisa kuhusu waandishi ambao sikuhizi badala ya kufuatia mambo ya maana wameanza na wao kuwa magazeti ya udaku. Kuanzia yale makubwa hadi yaliyoanzishwa juzi ni udaku mtupu na hakuna habari yoyote ya maana.

Waandishi wenyewe ndio wamekuwa wala rushwa wakubwa. Makampuni ya dhahabu yamewahonga kushoto na kulia pamoja na viongozi wao na sasa hatusikii lolote kuhusu hao Wakanada na dhahabu wanayoendelea kutuibia na kuua watu wetu kwa mercury na uchafu mwingine.

Waandishi hamna maana kabisa. Wote mngelikusanyika na nchi nzima tuitwe kuwatemea mate ndio mngelijua jinsi tulivyowachoka siku hizi.

Kusoma hamtaki. Kujiendeleza hamtaki. Na wengine ninasikia wanahongwa kwa kupewa nafasi za masomo nyoronyoro kishwa wanapasishwa ili warudi kuendelea na udaku bila kuelimika.
 
Ushahidi wa mate kwenye fulana na Jerry utakuwepo kweli baada ya masaa machache!?

huyo jonalisti anayo futeji nzuri ya tukio zima kwenye tepu!...huyu mzungu ni mpumbavu sana, mm nisingevumilia mtu wangu ni kichwa tu.ila jamaa amesema atakomaa na isyu mpaka kieleweke :evil:
 
SAFI sana. Ninadhani ofisa balozi huyo alikuwa anaonesha dharau ya juu kabisa kuhusu waandishi ambao sikuhizi badala ya kufuatia mambo ya maana wameanza na wao kuwa magazeti ya udaku. Kuanzia yale makubwa hadi yaliyoanzishwa juzi ni udaku mtupu na hakuna habari yoyote ya maana.

Waandishi wenyewe ndio wamekuwa wala rushwa wakubwa. Makampuni ya dhahabu yamewahonga kushoto na kulia pamoja na viongozi wao na sasa hatusikii lolote kuhusu hao Wakanada na dhahabu wanayoendelea kutuibia na kuua watu wetu kwa mercury na uchafu mwingine.

Waandishi hamna maana kabisa. Wote mngelikusanyika na nchi nzima tuitwe kuwatemea mate ndio mngelijua jinsi tulivyowachoka siku hizi.

Kusoma hamtaki. Kujiendeleza hamtaki. Na wengine ninasikia wanahongwa kwa kupewa nafasi za masomo nyoronyoro kishwa wanapasishwa ili warudi kuendelea na udaku bila kuelimika.

Ndugu Mbona story haieleweki?
 
apigwe tanganyika jeki mpaka airport, mzabe vibao viwili halafu weka kwenye KLM arudi kwao...kazi nyingine za maana ziendelee
 
Wrong priorities, ardhi inachukuliwa na wageni hatusemi sana, madini yanachukuliwa hatusemi kabisa, rasilimali zinachukuliwa, tunanyonywa na wageni hatusemi. Kama kweli askari katemewa mate imetokana na uzembe wetu wa kuwakabidhi uchumi wetu na kutufanya tunyonywe na matokeo yake wao wanajumuisha kuwa kama tumewapa uchumi na uhuru wetu basi hata utu hatuna.

Tuamke kwenye rasilimali zetu na uhuru wetu kwanza.


Tukiwa navyo hivyo hakuna atayethubutu kututemea mate.

sijawahi kusikia katika jamii kuna priority moja...
ya ardhi yapo na yana platform yake,
ya mate yapo na yana platform yake
Ya kubakwa na mbwa yapo na yana platform yake
ya rushwa yapo na yana platform yake
ya madini yapo na yana platform yake
ya utalii yapo na yana platform yake
ya pepfar yapo, na yana platform yake
ya ngozi yapo na yana platform yake

as long as we love tz we should make all fronts to fight for our country
 
Jamani, ninaomba msaada.
Re:
Katibu Mhitasi
Hili neno MHITASI ndio maanake nini? Tunawatafsiria hii habari ya Alasiri ubalozi wa Canada katika nchi fulani - sio Tanzania. Mwenyekujua anijulishe kwa haraka, kwani ninangojea.
Atashika adabu yake huyo alietemea mate crown yetu. Hatotema mate maisha!!!
 
Inasikitisha kwa kweli maana anajua fika sheria za ki diplomatic zinamlinda inaudhi sna tena sana.
 
sijawahi kusikia katika jamii kuna priority moja...
ya ardhi yapo na yana platform yake,
ya mate yapo na yana platform yake
Ya kubakwa na mbwa yapo na yana platform yake
ya rushwa yapo na yana platform yake
ya madini yapo na yana platform yake
ya utalii yapo na yana platform yake
ya pepfar yapo, na yana platform yake
ya ngozi yapo na yana platform yake

as long as we love tz we should make all fronts to fight for our country
Mkuu, while in principle I agree with you, please do not forget that "huyu Mkanada ameonyesha wazi kuwa haoni sababu ya kuheshimu nchi hii ambayo anajua siri za mapato yake, ufisadi wake na udhaifu wa viongozi wake" kuwa bila misaada yao hatuwezi kusimama. Kusema hivyo siyo kwamba tunakubaliana na tendo lake, la hasha. lazima aadhibiwe. But looking at the situation utaona tu kuwa amemtemea mate maana hakuridhika na kwamba alingoja sana muda mrefu pale bila kuruhusiwa kupita kuendelea na safari yake. Therefore, katika kila tukio liwe la utani, liwe chafu kiasi gani there is a message for us and if the leaders are smart enough should come up with lessons learnt.
 
kama polisi angemchapa kibao huyo ofisa ubalozi basi kibarua chake
kingeota majani. mmesahau yaliyompata marehemu balozi mwasakafyuka?
alitetea heshima ya nchi akahamishwa foreign na kupelekwa mkoani.
 
Tanzania anger at 'diplomatic spat' with Canada



The Tanzanian Foreign Ministry has summoned the Canadian High Commissioner after a Canadian diplomat allegedly spat at a policeman and a journalist.

A Tanzanian ministry spokesman condemned the incident, saying that his country is considering whether to expel the diplomat concerned.

Reporters say the diplomat, angered by a traffic jam, wound down his window and spat at the policeman on duty.

The Canadian High Commission in Dar es Salaam said it was investigating.
Tanzania's foreign ministry says the incident was a humiliation not just for the police officer and journalist concerned, but for the entire country.

The alleged incident occurred in the Banana district on the outskirts of Dar es Salaam.

The journalist was allegedly spat at after he went to the police station where the diplomat was taken after being arrested.

The diplomat was freed because he had diplomatic immunity.

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/8408589.stm
 
Back
Top Bottom