Mfanyakazi wa Ubalozi wa Canada adaiwa kumtemea mate Polisi

Wakuu, hapa tunaweza kuanza kumkumbuka Nyerere, tujiulize tulipigania uhuru kwanini? kwa sababu hatukutaka kunyanyaswa, kupuuzwa na kudharauliwa. mimi nimekasirishwa sana na kitendo cha polisi wetu kutemewa mate. Na kama ningekuwa na madaraka, huyu jamaa hatakiwi kuondoka in 24 hrs anatakiwa ashikishwe adabu kwanza kabla ya kuondoka. Kama serikali haiwezi kulinda utu wetu na heshima yetu na ya polisi wetu ingekuwa ni vizuri tutumie sheria zetu za jadi.
In fact ningekuwa mimi nimetemewa mate hiyo ingekuwa top story world over, sidhani hata m-canada yeyote anaweza kuunga mkno ujinga wa mcanada mwenzao.

Hii inaweza kuwa another test kwa serikali, kama kweli inaweza kulinda dignity yetu.
 
kesi kama hiyo huku Eastern europe sisi waga haina mwamuzi tunamalizana hapo hapo wenyewe...yaani hapo ilikua ni kumpa ngumi ya usoni na kumtemea mate mdomoni ...basi kesi kwisha.....
 
Usishangae hadi kesho hakuna chochote.

Na jinsi bongo ilivyo askari wacentral watakua wanaangalia upepo, watu wakitulia
wanakula dili mzungu nje kwishney.

Sina imani kama mzungu atachukuliwa hatua, otherwise labda watu wapige sana mayowe
ndo huenda sheria butu zitafanya kazi.

BONGO NI ZAIDI YA UIJUAVYO.
 
Kama kweli hili limetokea huyu mtu hata credentials zake za ubalozi zinatia shaka, tutaanza kufikiri kwamba kwa kuwa mtu wa ubalozi yuko hivi basi ni representative wa wa-Canada, which is not fair.

Huyu anaweza ku-invoke diplomatic immunity kirahisi, lakini ubalozi wa Canada kama unajua whats good for them na hautaki kuonekana unafuga watu washenzi ni bora wangemrudisha kwao.

Unfortunately watu wa ubalozi kuwashitaki ni tabu sana, hasa kwa kesi kama hii.

Mtafutieni mabasha.

Vinginevyo Watz wa Canada wamfungulie kesi huko kwao.
 
Inabidi na yeye atemewe mate mara mbili! na kesi hiyo ifungwe that is enough for him!
 
Wakoloni wametukamata hadi machoni,na sheria imesiginwa kilichobaki ni kutumia mbinu mbadala kama KIBANGA alivyomdunda majebu mkoloni,Maana tutaambiwa upelelezi unaendelea na baadaye faili liko kwa DPP,na mwisho ni kushika tama kama BROWN
 
Hili lisipochukuliwa hatua za kuridhisha ikiwa ni pamoja na kumuadabisha huyo mzungu hakika Watanzania tutajikia vibaya sana na wanyonge ndani ya nchi yetu pendwa. Pole Trafiki na Pole Jerry Muro. Ni kitendo cha kikoloni hakika
 
Kaka mkuu ...Punguza chuki !! Subiri kwanza rufaa zidi ya Zombe, wakishinda tena ndipo tutatoa hukumu kwa Mzungu !!! Jibu lipo kwenye Mabano !!!!!

Mkuu umesomeka, nimefungua mabano!!! chuki sina ila nina hasira tu mazee
 
Kama kweli hili limetokea huyu mtu hata credentials zake za ubalozi zinatia shaka, tutaanza kufikiri kwamba kwa kuwa mtu wa ubalozi yuko hivi basi ni representative wa wa-Canada, which is not fair.

Huyu anaweza ku-invoke diplomatic immunity kirahisi, lakini ubalozi wa Canada kama unajua whats good for them na hautaki kuonekana unafuga watu washenzi ni bora wangemrudisha kwao.

Unfortunately watu wa ubalozi kuwashitaki ni tabu sana, hasa kwa kesi kama hii.

Consular and Diplomatic Immunity under the Vienna Convetion [ambayo Tanzania Imeisaini na Bunge Kuipitisha kama sheria mama] inamlinda huyo mtuhumiwa dhidi ya mashtaka yote ya jinai. Membe et al wanatakiwa kumtangaza huyu jamaa 'persona non grata' na kupewa masaa 24 arudi kwao. Nachelea kusema hiki kitu kinaweza kwisha kimya kimya[rejea wale wanajeshi waliomuua dada wa kitanzania kule Kunduchi Beach jinsi suala lake lilivyoishia kienyeji enyeji]

Sometimes 'njaa' na 'umimi' vinatuponza sana watz. wake up tz!
 
hii habari imenipandisha hasira sana. kama kuna mtu ana namba ya ubalozi wa canada aiweke hapa haraka. itabidi niongee nao kwa kiingereza. yaani nimekasirika mpaka nimemkosa teke sista wake waif. sheenz sana hawa!
 
Kama sio juhudi zako nyerereeeee...kamasio juhudi zako nyerere....na uhuru tungepata wapiiiii????????......NAJISIKIA KULIA MACHOZI YANANILENGALENGA....

Natamani nyerere angekuwapo..an eye 4 an eye ..a tooth for a tooth ..can solve this issue as simple as ABC...aitwe balozi wa kanada hapo central...kisha jerry muro na traffic waitwe na membe awepo....hukumu itoke hivi
membe:- mr balozi huyu mtuhumiwa hapa mbele ni mtu wako?
balozi:- yes mr. minister
membe:- bwana trafic police na mr. jerry muro mnamfahamu huyu mzungu hapa mbele yenu
washtaki:- ndio mh.
membe:- mnaweza kuelezea kilichotokea?
washtaki:- ndio mh. mie nikiwa kazini pale ukonga huyu mzungu alinitemea mate usoni...na mimi mh. nilitemewa mate hapa hapa kituoni nikichukua habari za huyu bwana kumtemea mate traffic..waulize hata wakuu wa kitu walikuwepo
membe:- mkuu wa kitu anayosema mshtaki muro ni ya kweli
mkuu wa kituo:- ndio mheshimiwa
membe:- mr. balozi umesikia haya yote yaliyosemwa?
balozi:- yes mr. minister...but you know he is under protection to this types of cases?
membe:- thank you mr. balozi najua llakini hawa watu wangu hawataridhika mpaka nao wamwonyeshe kuwa alichofanya sio kizuri....
membe:- washtaki naomba mjiridhishe kwa kumtemea mate huyu mtuhumiwa usoni kama alivyowafanyia ninyi
washtaki:- asante sana mheshimiwa....
membe:-...mr. balozi nadhani huitaji kumrudisha huyu kijana wako canada ...anaweza kuendelea na kazi kama kawaida...maana keshatemewa mate na yamekwisha.
washatki:- tunashukuru mheshimiwa...sie hatuna tena ugomvi na yamekwisha
membe:- thanks mr. ambassador ..hope u have no clue the way i ressolved this matter
balozi:- ohhh yes i dont...i like the way you put ur people first...thats very good diplomatic approach
membe:- you are welcome....afterall we now have enough uranium reserves

NA HAPO ISSUE INAKUWA IMEISHA KI-STAARABU NA TUNAENDELEA KUDUMISHA UHUSIANO WETU WA KINDUGU NA KUPEANA BURE MIGODI NA MISAADA YA VTYANDARUA KATI YA CANAD/USA NA DANGANYIKA
 
Consular and Diplomatic Immunity under the Vienna Convetion [ambayo Tanzania Imeisaini na Bunge Kuipitisha kama sheria mama] inamlinda huyo mtuhumiwa dhidi ya mashtaka yote ya jinai. Membe et al wanatakiwa kumtangaza huyu jamaa 'persona non grata' na kupewa masaa 24 arudi kwao. Nachelea kusema hiki kitu kinaweza kwisha kimya kimya[rejea wale wanajeshi waliomuua dada wa kitanzania kule Kunduchi Beach jinsi suala lake lilivyoishia kienyeji enyeji]

Sometimes 'njaa' na 'umimi' vinatuponza sana watz. wake up tz!

Huyu jamaa hawezi kushitakiwa wala kutoa maelezo yoyote polisi kwa vile ana kinga ya kibalozi.

Sasa kitakachofanyika baada ya kukamilika upelelezi. balozi wake(Canada) ataamua kama avulie kinga ya kibalozi kisha ashitakiwe kwa sheria za Tanzania. au Arudishe kwao haraka na kushitakiwa kwa sheria za Canada.


Sasa ni jukumu la Wizara ya nje kufatilia hili ili Trafik na mwandishi wa habari wapate haki zao.


Poleni sana wahanga. Kuna haki yenu hapo. mkalieni kooni tu ili sheria ichukue mkondo wake.
 
Huyo mzungu nashauri awekwe lock up masaa 48 segerea alale na walalahoi
 
ngoja tusubir case preceedings lakini ukitaka kujua nchi hii viongozi hamnazo ni jinsi uyo jamaa atakavyoachiwa kirahisi, ningekua mimi ningempa kibano kwanza ili kurudisha heshima na kusettle scores, wanadharau sana hawa watu!
 
hii habari imenipandisha hasira sana. kama kuna mtu ana namba ya ubalozi wa canada aiweke hapa haraka. itabidi niongee nao kwa kiingereza. yaani nimekasirika mpaka nimemkosa teke sista wake waif. sheenz sana hawa!

Nimegoogle, nimepata haya
High Commission of Canada to Tanzania in Dar es Salaam

The High Commission represents Canadian interests in Tanzania, Madagascar, Seychelles, and the Union of the Comoros.
Address, Telephone, Fax, Email

Street Address
High Commission of Canada
38 Mirambo St. Garden Avenue
Dar es Salaam, Tanzania


Postal Address
High Commission of Canada
38 Mirambo Street / Garden Avenue
P.O. Box 1022
Dar es Salaam, Tanzania


Telephone: 255-22-216-3300
Fax: 255-22-211-6897
Email: dslam@international.gc.ca
Hours of Operation

Monday to Thursday: 07:30 – 16:00
Friday: 07:30 – 13:00
Office closures during 2009: DateClosed for:01 JanuaryNew Year's Day09 MarchMaulid Day10 AprilGood Friday13 AprilEaster Monday29 JuneCanada Day (in lieu)22 September Eid-El-Fitri 23 SeptemberEid-El-Fitri12 OctoberCanadian Thanksgiving09 DecemberRepublic Day25 DecemberChristmas Day28 DecemberBoxing Day (in lieu)

Unaweza kuandika au hata kuanzisha email ya petition, na sisi tutakusaidia kuisign na kuiforward ilimradi wasirudie tena

MTM
 
Wrong priorities, ardhi inachukuliwa na wageni hatusemi sana, madini yanachukuliwa hatusemi kabisa, rasilimali zinachukuliwa, tunanyonywa na wageni hatusemi. Kama kweli askari katemewa mate imetokana na uzembe wetu wa kuwakabidhi uchumi wetu na kutufanya tunyonywe na matokeo yake wao wanajumuisha kuwa kama tumewapa uchumi na uhuru wetu basi hata utu hatuna.

Tuamke kwenye rasilimali zetu na uhuru wetu kwanza.


Tukiwa navyo hivyo hakuna atayethubutu kututemea mate.
 
Talking about DNA, nadhani itakuwa vyema wakamfania DNA test huyu mtasha, nahisi one of her grand grand parent alikuwa Chatu au Cobra!
 
Jery Muro & Traffic Officer pole sana - Jery nilikusikia kwenye BBC jana jioni ukisema kuwa kama mambo yatepelekwa ndivyo sivyo utafungua shauri "solo" - Je hili linawezekana? Kama linawezekana (wanasheria watusaidie) nadhani waTz wengi watakuwa wa msaada kwako.
 
Back
Top Bottom