Mfanyakazi wa low voltage afumwa na umeme wa million 25

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Haya kazi kwenu kw ahabari zaidi soma mtanzania leo uk wa 5
ni sh 500 tu ,tukiandika kila kitu wafanyakazi watalipwa wapi
jamani ..ila hali ndio hiyo kijana kakutwa na umeme huo na kabanwa ameanzakuwataja
sehemu alipokuwa anawauzia ngoma nzito kwenu mliokuwa mnawaonyesha majumbani
mwenu vijana wanakuja huko huko
moja ya sehemu maaruufu ni bar na shule za sekondari na ameanza kuonyesha
hii ni taahdhari tu tumia harak uishe wasije kukumhando
 
Mtuhumiwa huyu amekamatwa na vitu vya tanesco ambavyo mtu wa kawaida aruhusiwi kuwa navyo na ameomba nafasi kuwataja waliomletea hivyo vifaa kutoka tanesco baada ya kuhakikishiwa punguzo la adhabu...na amekiri ana miaka 7 anafanya kazi na watu wa tanesco kwa kuiba umeme ...uuuuwiiii;ikiwemo kutaja sehemu alikokuwa akiweka hizo namba za luku
za mamiliion ..kweli mjini shule
 
Katika kinachonifurahisha jamaa alikuwa na ofisi yake kabisa imekutwa ukiacha vifaa kuna
faili za wateja wake kabisa...risiti zake iwapo ukiitaji kadi za wateja,na mita kadhaa za luku
 
Hawa jamaa hawajaiibia Tanesco wametuibia wananchi.

Watajwe wote kila siku tunasema Jk mbaya lakini wabaya wengine tuko miongoni mwetu...... Majumba yao na sehemu zao za biashara ziwekwe wazi.

Bravo... Prof Sospeter Muhongo.... Bravo JK kwa uteuzi wa Muhongo.
 
Katika kinachonifurahisha jamaa alikuwa na ofisi yake kabisa imekutwa ukiacha vifaa kuna
faili za wateja wake kabisa...risiti zake iwapo ukiitaji kadi za wateja,na mita kadhaa za luku

Wameacha tracing nzuri....... ndio mwanzo wa kukamata wote na wakitajwa wengi tutabaki vinywa wazi.
 
Chenge na RADA ya magumashi anasamehewa... wajasiriamali wananyanyaswa grrrrrrrrrrrrrrrrrrrr?
 
Mtuhumiwa huyu amekamatwa na vitu vya tanesco ambavyo mtu wa kawaida aruhusiwi kuwa navyo na ameomba nafasi kuwataja waliomletea hivyo vifaa kutoka tanesco baada ya kuhakikishiwa punguzo la adhabu...na amekiri ana miaka 7 anafanya kazi na watu wa tanesco kwa kuiba umeme ...uuuuwiiii;ikiwemo kutaja sehemu alikokuwa akiweka hizo namba za luku
za mamiliion ..kweli mjini shule

JK kazi ya kuwabadili Watanzania unayo na ni kubwa ni vema kama tukafikiria kunyonga watu kama hawa...... wanachangia sana serikali kuchukiwa.
 

Kampuni inayoihujumu TANESCO yanaswa Dar
• Inauza luku, kufunga mita, kutengeneza umeme kwa bei poa

na Irene Mark


amka2.gif


KAULI ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospiter Muhongo kwamba kuna vigogo wanaoshirikiana na wafanyakazi wa Shirika la Umeme (TANESCO), kulihujumu shirika hilo, imethibitika.
Jana, TANESCO iliinasa kampuni hewa inayotoa huduma sawa na shirika hilo na kulisababishia hasara ya mabilioni ya shilingi kwa miaka saba sasa.

Kampuni hiyo yenye makazi yake Mwananyamala barabara ya Mwinjuma jijini Dar es Salaam, ilisajiliwa kwa jina la Low Voltage Distribution ambayo mmiliki wake ni Mussa Mtavazi, ilibainika jana baada ya watendaji wa TANESCO na maofisa wa polisi kuvamia eneo hilo.
Kampuni hiyo ipo kwenye nyumba namba 648 mali ya Bakari Issa aliyeeleza kwamba mkataba wa upangaji kwenye nyumba hiyo, uliwekwa kati yake na Mtavazi kwa makubaliano ya kulipa pango la sh 25,000 kwa mwezi malipo yanayofanyika kila baada ya miezi minne.

Zoezi la kumnasa mmiliki huyo mwenye ‘TANESCO’ ndogo lilifanikiwa jana saa saba mchana wakati watendaji wake wakiwa kazini kama kawaida ghafla maofisa wa polisi kutoka kituo cha Oysterbay waliokuwa na hati ya upekuzi, watumishi wa TANESCO na waandishi wa habari walipovamia nyumba hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi hiyo muda mfupi baada ya kukamatwa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Low Voltage Distribution, Ibrahim Said alikiri kwamba kampuni hiyo inafanya shughuli zote za TANESCO ikiwemo kuuza luku, kufunga mita kwa wateja, kutengeneza umeme na shughuli nyingine.

Hata hivyo, ndani ya ofisi hiyo kulibainika kuwepo kwa sare za watumishi wa TANESCO, mita za umeme na vifungio vya mita (Seal), mikanda na ngazi za shirika hilo inayotumika kupanda kwenye nguzo, tokeni za luku, kufunga umeme majumbani na mafaili yenye namba za wateja.
Kwa upande wake Meneja Habari na Mawasiliano wa TANESCO, Badra Masoud alisema kazi hiyo ni sehemu ya maboresho ya utendaji wa shirika hilo huku akiwataka wote wanaolihujumu kuacha vinginevyo mkono wa sheria utawafikia.

“Tunajua kwamba shirika linahujumiwa tena tunaamini wanaolihujumu sio watu kutoka mbali, wapo humu humu ndani ni watumishi wenzetu wanaoshirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu.
“Hivi vitu zikiwemo sare za TANESCO tulizozikuta kwenye hii kampuni vinagharama kubwa kuvipata, lakini yeye anavimiliki isivyo halali… ameiba channel (njia) ya luku na anawauzia wafanyabiashara wengine kinyume cha sheria, mapato hayatufikii.

“Ukija hapa kununua luku unaipata kwa bei nafuu sana halafu sasa hizo pesa anabaki nazo huu ni wizi kwa shirika, tunajua kwa miaka hiyo saba amewauzia watu wengi na sisi tutawafuatilia mmoja baada ya mwingine na kuwanasa.
“Nawashauri wote wanaoliibia shirika kujisalimisha… tukimgundua sheria inachukua mkondo wake, hakuna msalie mtume katika hili,” alisema Badra huku akiwaonyesha waandishi wa habari baadhi ya vifaa vya TANESCO vilivyokutwa kwenye ofisi hiyo.

Kwa mujibu wa Badra, shirika litafanya tathimini ya hasara na gharama ya mali zilizokutwa kwenye ofisi hiyo ili kujua gharama halisi huku watendaji wake wakiendelea kuwatafuta wananchi wengine wanaoshiriki kulihujumu shirika huku akisisitiza kwamba wahujumu wote watachukuliwa hatua za kisheria.
Hivi karibuni akiwa bungeni, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo aliwataja baadhi ya watu, Taasisi na Makampuni yanayoshiriki kulihujumu shirika la umeme akiwemo Mbunge wa Viti Maalum, Getrude Lwakatare kupitia shule zake za St. Mary’s.

Profesa Muhongo alisema, hadi sasa TANESCO imewabaini wezi wakubwa wa umeme wapatao 50 na kwamba kazi hiyo itaendelea ili kuhakikisha shirika hilo linaweza kujihudumia bila madeni makubwa na kutoa huduma bora kwa wateja wake.

Hawa ndio wahujumu uchumi.
 
TANESCO majizi mengi sana huu mchongo wa wakubwa mark my word
 
huyu mwizi alikuwa mjasiriamali, ni vema akaajiriwa TANESCO kitengo cha ukusanyaji maduhuli a.k.a mapato
 
Mtuhumiwa huyu amekamatwa
na vitu vya tanesco ambavyo mtu wa kawaida aruhusiwi kuwa navyo na
ameomba nafasi kuwataja waliomletea hivyo vifaa kutoka tanesco baada ya
kuhakikishiwa punguzo la adhabu...na amekiri ana miaka 7 anafanya kazi
na watu wa tanesco kwa kuiba umeme ...uuuuwiiii;ikiwemo kutaja sehemu
alikokuwa akiweka hizo namba za luku
za mamiliion ..kweli mjini shule

Lazima utakuwa mchongo wa mabosi huko huko Tanesco! Kwa nini akamatwe sasa na ameshaoperate muda mrefu? Kuna anayetolewa kafara hapa.
 
dah! amaa kweli, Tanzania ni zaidi ya uijuavyo. cha ajabu huyu nae tutaambiwa upelelezi haujakamilika. huyu haraka ale mvua pamoja na walionyuma ya hii mission mbovu ya kuhujumu uchumi. Sasa siku zote hizo, kwenye mji mkubwa na muhimu kama DAR ES SALAAM uliojaa wakugenzi kibao wa mambo ya uharifu na usalama, haingii akilini yote haya yanafanyika bila hata kugundulika kweli?? au ndo miradi ya waheshimiwa wameanza kufichuana?? hii nchi hii si ajabu hata viwanda vya cocaine vimo humu humu. jamani Tanzania yetu!!!!!!! wanajamvi, naomba mnijuze majukumu ya usalama wa taifa kwa mujibu wa sheria tafadhari ili nijiridhishe kuwa hili haliwahusu.
 
Ni mhujumu uchumi...ok.

Ila inawezekana kabisa kuwa huduma zake zilikuwa za haraka zaidi, ukitaka umeme leo na ukalipia leo leo, nguzo zitakuja (if need be), luku itafungwa na umeme utawaka leo leo! Why not?....oops sorry pipoz. was just thinking out loud.
 
Ni mhujumu uchumi...ok.

Ila inawezekana kabisa kuwa huduma zake zilikuwa za haraka zaidi, ukitaka umeme leo na ukalipia leo leo, nguzo zitakuja (if need be), luku itafungwa na umeme utawaka leo leo! Why not?....oops sorry pipoz. was just thinking out loud.

Jamaa alikuwa fasta kuliko hata tanesko yani kila kitu leo leo basi angesajiliwa tu atoe huduma fasta
 
Ni mhujumu uchumi...ok.

Ila inawezekana kabisa kuwa huduma zake zilikuwa za haraka zaidi, ukitaka umeme leo na ukalipia leo leo, nguzo zitakuja (if need be), luku itafungwa na umeme utawaka leo leo! Why not?....oops sorry pipoz. was just thinking out loud.
Sure,
Ingekua umeme wa Tanesco ni reliable tusingehangaika na huyu jamaa.

Tanesco ndio wametufikisha hapa tulipo.

Kwanza uchumi gani unaohujumiwa hapa, watu wamepiga EPA, Radar, n.k na hawajaitwa wahujum uchumi sembuse huyu mvumbuzi???
 
Back
Top Bottom