Mfanyakazi wa Barrick mwaathirika wa kemikali afariki

mgomba101

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
1,817
706
mfanyakazi_wa_barrick.jpg


MFANYAKAZI wa Kampuni ya Africa Barrick Gold aliyekuwa akifanya kazi mgodi ya Bulyanhulu, wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Samuel Kamudulu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na mapafu na uti wa mgongo.

Akizungumza kwa simu kutoka Arusha, kaka wa marehemu, Lekiu Kamdulu alisema Samuel alifariki ghafla walipokuwa Arusha baada ya kutoka matibabu Dar es Salaam.

“Samuel alifariki Oktoba 25 saa 2:00 usiku. Unajua baada ya kumwandikia ile habari kwenye gazeti la Mwananchi, kampuni ilimchukua na kuanza kumtibu. Kwa hiyo tuliitwa Kahama tukafanyiwa utaratibu na kurudishwa tena Dar es Salaam kwenye matibabu,” alisema Kamudulu na kuongeza:

“Baada ya kutoka kwenye matibabu tulikuja Arusha nyumbani tangu wiki iliyopita hadi alipofariki juzi.”

Wakati wa uhai wake, Samuel alisema mapafu yake yameathiriwa na kemikali zinazotumika kwenye uchimbaji madini ya dhahabu.

“Mapema mwaka huu nikiwa kazini ndani ya mgodi niliishiwa nguvu ghafla na kuanguka. Nilibebwa bila kujitambua na kupelekwa hospitali ya kazini na kuambiwa kuwa nina ugonjwa wa mapafu (pneumonia),” alisema Samuel wakati wa uhai wake na kuongeza:
 
Kampeni ya Fao la kujitoa hiyo. Haya tutaiona serekali yenu kama sikivu au imeziba pamba masikioni.
 
Kampeni ya Fao la kujitoa hiyo. Haya tutaiona serekali yenu kama sikivu au imeziba pamba masikioni. R I P
 
RIP ndugu Samwel...

Lakini hii stori ina walakini kidogo, inaonekana kama mwandishi ana 'bifu' na Barrick kiasi anashindwa kutally facts kuattribute kifo cha mhanga kimetokana kweli na kemikali hizo. Ni vigumu sana kuwe na wajiriwa kadhaa, mnafanya kazi moja exposed kwa kemikali moja...halafu augue mmoja tu. Plus Pneumonia inaweza sababishwa na dozens of reasons..kuna evidence gani hii ilikuwa 'Chemical Pneumonitis'?
 
[size=4 said:
kwamtoro;4930691]kampeni ya fao la kujitoa hiyo. Haya tutaiona serekali yenu kama sikivu au imeziba pamba masikioni. R i p[/size]
hili nalo neno hivi ana miaka 55 kweli.
 
Back
Top Bottom