Mfanyakazi The Guardian Ltd aaga dunia

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,109
Gud(3).jpg

Mfanyakazi wa Kampuni ya The Guardian Limited, Michael Salira (70)


Mfanyakazi wa Kampuni ya The Guardian Limited, Michael Salira (70), pichani, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Yombo Makangarawe Barabara ya Mwinyi, jijini Dar es Salaam.

Baba mdogo wa marehemu, Norbert Ikonko, alisema mwanaye aliaga dunia ghafla akiwa amelala nyumbani kwake.

Ikonko alisema wanatarajia kuusafirisha mwili wa marehemu Salira, kesho Jumapili kwenda katika Kijiji cha Ruaha, Kata ya Mwaya, Tarafa ya Mahenge Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kuzikwa siku ya Jumatatu.

Alisema mwili wa marehemu utaagwa nyumbani kwake Yombo Makangarawe kesho kuanzia saa 7:00 mchana.

Marehemu alihitimu masomo yake katika Shule ya Sekondari Kwiro mkoani Morogoro mwaka 1959.

Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari, alijiunga na Chuo cha Ualimu Mpwapwa mkoani Dodoma mwaka 1960 hadi mwaka 1961 na kutunukiwa Cheti cha Ualimu Daraja la 1.

Baadaye, alijiunga na Wizara ya Elimu ambako alifanya kazi hadi alipostaafu mwaka 1995.

Aliajiriwa rasmi na Kampuni ya The Guardian Ltd Septemba Mosi, 2007 kama Mhakiki Kurasa (Proof Reader), kazi aliyoifanya kwa weledi na uadilifu mkubwa hadi kifo chake.

Ameacha mjane, watoto wanne ambapo wawili kati yake ni wa kike na idadi kama hiyo wa kiume pamoja na wajukuu wanane.

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Salira. Amina.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom