Mfanyabiashara wa Arusha apuuza agizo la Serikali

MJINGA KWA WOTE

New Member
Feb 24, 2016
2
4
Katika hali ya kushangaza mmiliki wa kampuni ya ujenzi ya Elerai construction na Northern Engineering amepuuza agizo alilotoa naibu waziri wa kazi alipofanya ziara ya ghafla katika kampuni hiyo January mwaka huu.

Agizo la serikali kwa mmiliki huyo ni kuhakikisha anaacha kuajiri wageni kwa kazi zinazoweza kufanyika na watanzania.

Siku moja baada ya agizo hilo bwana Samwel Lema alimpuuza waziri, kwa kuwaajiri mafundi wapya toka kenya siku moja baada ya waziri kutoa agizo hilo.

Baadhi ya walioajiriwa ni hawa.
1. Peter Kiloli Meneja biashara wa Northern Engineering( amefanya kazi hapo kwa miaka 10 sasa) raia wa Kenya.

2. Anthony Kimani msimamizi wa mafundi wa Elerai (amefanya kazi miaka 14) Raia wa Kenya.

3.Godwin ( meneja wa manunuzi Northern) Raia wa Kenya.

5. Moris ( msimamizi wa mafundi).

6. Adul (meneja wa usafiri) Raia wa Pakistan.

7. Vibarua zaidi ya 15 wa ujenzi toka Kenya.

8. Technicians 10 toka Parkistan.

Pia waziri aliagiza malimbikizo yote ya NSSF na PPF ya wafanyakazi ya zaidi ya miaka mitatu yapelekwe panapostaili.

La kushangaza ni kwamba bwana Lema badala ya kulipa madeni, anawahonga mameneja wa mkoa wa mifuko ya jamii ili asishtakiwe.

Uchunguzi uliofanyika unaonyesha kuwa Lema (mmiliki) ni marafiki wa karibu na meneja wa mkoa wa NSSF wanashinda pamoja jioni pale kibo palace na gymkhana, hivyo hawezi kumchukulia hatua ili kuwasaidia wanachi wanaonyanyaswa.

Baadhi ya wafanyakazi ambao hawakutaka majina yao kutajwa kwa kuhofia kufukuzwa wameomba waziri afuatilie agizo lake mwenyewe na asiwaamini watumishi wa serikali mkoani hapa kwakuwa huyu mfanya biashara anawahonga.

Hivyo wameomba task force toka makao makuu ya maofisa wa TRA, UHAMIAJI, na MIFUKO ya jamii ikafanye ukaguzi kwa mfanyabiashara huyo.
 
Tatzo la watanzania wengi tunaongea sana. Utendaji ukiwa hafifu sana. Lema ni mfanya biashara. He needs to make money and pay tax. Kama alifuata taratibu za kuajiri wageni.. Shida iko wapi? Watanzania wengi sisi ni wazembe na tunapenda ujanja ujanja. Sioni ajabu kama Huyu bwana kaamua kuajiri foreigners! Nenda hata mahotelini..utakuta wahudumu kelele nyingi..ooo tunanyanyaswa...oohh..hivi..ohh vile..lakini ukweli hata maji ya kunywa watakupa kwenye glasi chafu! Kikubwa ni kwamba huyo Lema AFUATE SHERIA STAHIKI ZA NCHI. Mengine ni majungu! Tujisahihishe. Tubadilike.
 
kwani sheria inakataza mfanyabiashara asiajiri toka nje? haya mengine ni majungu tu. Hamna lolote.
 
Agizo la Serikali gani???

Tanzania tutakuwa na Serikali mara baada ya kuwaondoa CCM Madarakani.
 
Nenda kwenye kituo chochote cha polisi kilicho karibu nawe. Nenda mbele counter yao halafu sema" Tanzania haina serikali mpaka uitoe CCM madarakani". Kisha utuletee mrejesho hapa. Kama Polisi mbali, basi hata kwenye kikosi chochote cha jeshi. Hata hapo utapata matokeo mazuri tu.
 
Kwani nchi inaongozwa kwa maagizo au sheria. Uyo waziri nae ndo wale wale wazee wa kukurupuka. Kampuni ya mtu binafsi sio ya serekali huwezi kumpangia watu wa kuwaajiri
 
Mkuu, naona umetoa data za kutosha na wanaohusika watafuatilia. Lkn pia hii itupe changamoto sisi watz. kwa nini makampuni haya hayataki kuajiri watz? je yanatubagua tu au ni kweli iko shida katika utendaji kazi? maana ni ukweli pia kwamba watz wengi hatuendi hata kufanya kazi nje, lakini wakenya wako kibao hapa tz. tatizo letu nini?
 
Duh MJINGA KWA WOTE ni kweli meneja wa manunuzi Bwana Godwin hala mchango wowote wa kuwazidi Shwahibu au Ndugu Msesi.Ni kasumba mbaya ya Bwana Lema ya kupenda raia wa kigeni ukilinganisha na watanzania ambao ndio wamemfikisha hapo alipo.

Niliwahi kuwauzia Land Cruiser mwaka jana nilishangaa kumkuta raia wa Paksatan Bwana Abdul eti ndio Transport Manager nikajiuliza mpakistan analipwa mshahara wa waTanzania kumi anasomesha mtoto Braeburn marupurupu hayo akipewa mtanzania atashindwa kweli ?.

Bwana Lema mbona umewaamini sana kina Shayo Project Accountant anafanya kazi nzuri,Bwana Migire Financial Manager anapiga mzigo vizuri kama haumfahamu unaweza kufikiri Migire ni shareholder.Yupo mwanamama Glory Minja ana kiwango bora kabisa ni kwanini hawapewi nafasi kubwa badala yake Lema anakwenda kuokota raia wa kigeni wasiokuwa na uwezo zaidi ya kuongea kingereza ?.

Ni wakati wa serekali kuchukua hatua badala ya kupiga makele na vyombo vya habari na kutafuta sifa za kitoto.Watanzania wapo wenye uwezo mkubwa sana sema tuna tabia ya kudharau.
 
Ungekuwa unafahamu aina ya integration inayotengeneza EAC (East African Community), ungejua msingi wake ni "Free movement of factors of production - labour/human resources and capital". Usisikie vibaya kuajiriwa kwa hao wakenya, hao WaPakistan unaweza kuwa na hoja. Hata Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kuna watanzania wameajiriwa na kufanya shughuli zao na hujasikia wakiaNa michango ya NSSF unaweza kuwa na hoja pia. Urafiki wao na habari za kwenda Kibo Palace na Gymkhana sio mambo yanayokuhusu na epuka kuwa stalker!!

Jua hili pia. Maagizo ya mdomo wakati wa ziara ni jambo la siasa. Lema sio tu anapuuza, pia hajapata maagizo ya kisheria ambayo yanataka "official communication" ikielezea kwa vifungu ya kisheria jinsi ELERAI ilivokosea na inavotakiwa kurekebisha. Ni communique hiyo itaweza kupingwa au kutekelezwa. Sio maelekezo ya mdomo eti kwa kuwa ni waziri mdogo kasema.

Hata hivo ni vema wafanyakazi wa kitanzania mkafuatilia jambo hili. Linaweza kuwa mwanzo mwema wa kizalendo.
 
MASANJA, MFAMAJI,HAMFCB,TREBORX,NEWORDER
wote mupo sawa 100% watanzania wengi kasi, hamasa na nidhamu ya kazi hawana.
mfano rahisi customer care ya airtel ni wachovu vya kutosha, ukija mahotelini ndio kabisaa hoi, bado uende ukatue halmashauri na sekta nyingine za utumishi wa umma ndio utaganda kwa masikitiko.
hili linachangia gdp ya nchi kutokuongezeka kwa kasi
 
Katika hali ya kushangaza mmiliki wa kampuni ya ujenzi ya Elerai construction na Northern Engineering amepuuza agizo alilotoa naibu waziri wa kazi alipofanya ziara ya ghafla katika kampuni hiyo January mwaka huu.

Agizo la serikali kwa mmiliki huyo ni kuhakikisha anaacha kuajiri wageni kwa kazi zinazoweza kufanyika na watanzania.

Siku moja baada ya agizo hilo bwana Samwel Lema alimpuuza waziri, kwa kuwaajiri mafundi wapya toka kenya siku moja baada ya waziri kutoa agizo hilo.

Baadhi ya walioajiriwa ni hawa.
1. Peter Kiloli Meneja biashara wa Northern Engineering( amefanya kazi hapo kwa miaka 10 sasa) raia wa Kenya.

2. Anthony Kimani msimamizi wa mafundi wa Elerai (amefanya kazi miaka 14) Raia wa Kenya.

3.Godwin ( meneja wa manunuzi Northern) Raia wa Kenya.

5. Moris ( msimamizi wa mafundi).

6. Adul (meneja wa usafiri) Raia wa Pakistan.

7. Vibarua zaidi ya 15 wa ujenzi toka Kenya.

8. Technicians 10 toka Parkistan.

Pia waziri aliagiza malimbikizo yote ya NSSF na PPF ya wafanyakazi ya zaidi ya miaka mitatu yapelekwe panapostaili.

La kushangaza ni kwamba bwana Lema badala ya kulipa madeni, anawahonga mameneja wa mkoa wa mifuko ya jamii ili asishtakiwe.

Uchunguzi uliofanyika unaonyesha kuwa Lema (mmiliki) ni marafiki wa karibu na meneja wa mkoa wa NSSF wanashinda pamoja jioni pale kibo palace na gymkhana, hivyo hawezi kumchukulia hatua ili kuwasaidia wanachi wanaonyanyaswa.

Baadhi ya wafanyakazi ambao hawakutaka majina yao kutajwa kwa kuhofia kufukuzwa wameomba waziri afuatilie agizo lake mwenyewe na asiwaamini watumishi wa serikali mkoani hapa kwakuwa huyu mfanya biashara anawahonga.

Hivyo wameomba task force toka makao makuu ya maofisa wa TRA, UHAMIAJI, na MIFUKO ya jamii ikafanye ukaguzi kwa mfanyabiashara huyo.

Tujiulize kwa nini waTanzania wenye sifa kama hizo hawaajiriki wakati wapo? Elerai siyo yenyewe.
 
Mkuu, naona umetoa data za kutosha na wanaohusika watafuatilia. Lkn pia hii itupe changamoto sisi watz. kwa nini makampuni haya hayataki kuajiri watz? je yanatubagua tu au ni kweli iko shida katika utendaji kazi? maana ni ukweli pia kwamba watz wengi hatuendi hata kufanya kazi nje, lakini wakenya wako kibao hapa tz. tatizo letu nini?

TATIZO LETU WATANZANIA LINAANZIA KWENYE INSTITUTION ZETU. MIMI NI MTANZANIA NAISHI NJE KWA MUDA MREFU NA NIMEJENGA CULTURE NA NIDHAM YA KAZI. NIMELETA VIFAA NA KUFUNGUA OFISI TANZANIA NIKIJUA PAMOJA NA KUJISAIDIA, NITATOA AJILA NA NIA IKIWA NI KUTOA SERVICE ZA HALI YA JUU KABISA KAMA HATA MAFUNZO KWA WATANZANIA.

KABLA HATA HUJAAJILI, TANESCO/TTCL/MANISAPA NK. EXCUSES NYINGI KUKUFUNGIA HUDUMA AMBAZO UNALIPA MAMILIONI NA HAWAJI. LA KUSHANGAZA HATA MWENYE NYUMBA ANACHARGE TU BILA KUJALI NYUMBA YAKE ALIKUWA HAJAIWEKEA UMEME/MITA. HII NI MBALI YA WATUMISHI AMBAO WANA EXCUSES PIA, KUUMWA, KUUGULIWA, KUKOSA USAFIRI NA MAMBO KADHA WA KADHA UTAZANI HAYO NDIO WALIO AJILIWA KWAYO. TUFIKE MAHALI TUJITAFAKALI SANA SIO LAWAMA TU. HATA MIMI NAONA WAKATI MWINGINE NI BORA KUFANYA BIASHARA SIO NYUMBANI.
 
Tatzo la watanzania wengi tunaongea sana. Utendaji ukiwa hafifu sana. Lema ni mfanya biashara. He needs to make money and pay tax. Kama alifuata taratibu za kuajiri wageni.. Shida iko wapi? Watanzania wengi sisi ni wazembe na tunapenda ujanja ujanja. Sioni ajabu kama Huyu bwana kaamua kuajiri foreigners! Nenda hata mahotelini..utakuta wahudumu kelele nyingi..ooo tunanyanyaswa...oohh..hivi..ohh vile..lakini ukweli hata maji ya kunywa watakupa kwenye glasi chafu! Kikubwa ni kwamba huyo Lema AFUATE SHERIA STAHIKI ZA NCHI. Mengine ni majungu! Tujisahihishe. Tubadilike.
Hoja kama hizi hutoka upande mmoja na bila evidence based arguments. Naamini kampuni hizi zina matawi ya cyama vya wafanyakazi na mabaraza ya wafanyakazi. Je cyombo hivi vimeyafanyia kazi matatizo haya na matokeo yake yamefikishwa katika ngazi zote pamoja na wafanyakazi? Mmiliki wa kampuni kunywa vinywaji na boss wa NSSF, PPF au TRA hayo ni masuala bunafsi.
 
Duh MJINGA KWA WOTE ni kweli meneja wa manunuzi Bwana Godwin hala mchango wowote wa kuwazidi Shwahibu au Ndugu Msesi.Ni kasumba mbaya ya Bwana Lema ya kupenda raia wa kigeni ukilinganisha na watanzania ambao ndio wamemfikisha hapo alipo.

Niliwahi kuwauzia Land Cruiser mwaka jana nilishangaa kumkuta raia wa Paksatan Bwana Abdul eti ndio Transport Manager nikajiuliza mpakistan analipwa mshahara wa waTanzania kumi anasomesha mtoto Braeburn marupurupu hayo akipewa mtanzania atashindwa kweli ?.

Bwana Lema mbona umewaamini sana kina Shayo Project Accountant anafanya kazi nzuri,Bwana Migire Financial Manager anapiga mzigo vizuri kama haumfahamu unaweza kufikiri Migire ni shareholder.Yupo mwanamama Glory Minja ana kiwango bora kabisa ni kwanini hawapewi nafasi kubwa badala yake Lema anakwenda kuokota raia wa kigeni wasiokuwa na uwezo zaidi ya kuongea kingereza ?.

Ni wakati wa serekali kuchukua hatua badala ya kupiga makele na vyombo vya habari na kutafuta sifa za kitoto.Watanzania wapo wenye uwezo mkubwa sana sema tuna tabia ya kudharau.
Aisee huyu migire ni kichwa Sana, Steven migire kama sikosei zao la ilbroru enzi hizo alipata point 08 olevel kujituma ni hulka yake.
 
Kweli kabisa, Ilborians tunamkumbuka

Lakini inawezekana Migire alikuwa kichwa darasani tu si katika mambo ya kazi. NImeshaona watu wengi wa namna hii katika nchi yetu. Wanavyeti vya kutisha, lakini ukija kwenye kazi wanaogoza kwa uzembe, wizi na kukosa maadili ya kazi.....
 
  1. Siyo kwamba watu wanapenda kuajiri wageni. Kwanza ni gharama kubwa kuwalipia vibali vya kufanya kazi n.k. lakini tatizo ni letu sisi waTZ. Tunacheza na kazi za watu. We are not serious. Mimi kikampuni changu kidogo lakini nimeajiri wahindi baada ya kuchoshwa na wabongo. Mtu ume mpa kazi, anafanya kama anavyotaka, anakuibia, wanaacha kazi ghafla bila utaratibu yaaani shida tu.
 
Back
Top Bottom