Mfanyabiashara Said Mohammed Saad wa Home Shopping Center (GSM Foundation)

mfadhili wa naninihiii,mahela yanatoka siku hiz tu huko dsm,tunasubiria milioni 50 za pambano la bela na banana la kuijipongeza kwa mikutano mubashara iliyotatua kero za dsm na kuzimaliza kabisa
 
Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu.

Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.
Jeshi letu la polisi halina mfumo wa kulinda key informant.
 
Hapa ndipo ninaposhindwa kuielewa Tanzania kwa upana nisioufikia kwakweli... Huyu jamaa na kampuni zake za uyoga anaendelea kutambaaaaa kama matembere na shutuma zikimwagika na sasa hivi kaingia kuisaidia jamii pamoja na serikali nimeona magari yake yakitumika kwenye ziara za mkuu wa jiji maarufu.

Nashindwa kuelewa UADILIFU wa viongozi wa serikali zetu hasa za Kiafrica, mtu anatajwa kwa shutuma nyingi hasa ambazo anakiuka sheria kukandamiza wengine na kujiiunua mwenyewe na kuiibia serikali mapato lakini bado anakumbatiwa na viongozi hao hao wa serikali pamoja na watendaji wake..

Sasa jamani mimi binafsi naomba kitabu hiki kifungwe kama inaonekana hawezi kufanywa kitu basi aachwe na atambe naye tuje tumchague sijui ubunge...

.....Ni Tanzania pekee wezi wanatamba na kuandamana na viongozi wa serikali.....!!!!
 
Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

Utangulizi

Mfanyabiashara Said Mohammed Saad anamiliki Kampuni ya Home Shopping Center iliyopo Kariakoo Mtaa wa Swahili na Msimbazi katika Jengo la Ghorofa lenye vioo vilivyochorwa picha za waigizaji wa Kikundi cha Orijino Commedy kinachorusha vipindi vyake Televisheni ya taifa ya TBC1.

Mfanyabiashara huyu ambaye ana uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Saud Arabia, anafanya uhalifu na kuhujumu uchumi nchi kwa kushirikiana na wafanyabiashara wengine wakubwa

Tuhuma

Mfanyabiashara Said Mohammed ameshiriki katika matukio mengi ya kihalifu yakiwamo ya kupiga risasi watu na kesi zake zimekuwa zikifunguliwa na baadaye anazizima kwa kutoa rushwa polisi.

Moja ya matukio hayo ni kumpiga risasi mfanyakazi wake mwaka 2005 wakati akishusha bidhaa za kuuza dukani kutoka katika gari lake, kumpiga risasi mwanafunzi wa Shule ya Msingi Vingunguti, Deo Vicent Agosti 15, 2006 saa 1:00 usiku Mtaa wa Msimbazi na Swahili Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mfanyakazi wake alimpiga baada ya kumbishia Said kwamba hawezi kumpiga risasi kwa sababu anajua sheria za nchi haziruhusu kufanya hivyo. Alimpiga kuonyesha kwamba yeye yupo juu ya sheria za nchi. Kesi hiyo nayo aliimaliza kimya kimya kwa kumpa hela mfanyakazi huyo na ndugu zake na polisi.

Mtoto Vicent yeye baada ya kupigwa risasi aliliripoti Polisi na baadaye alilazwa katika Wodi namba 17 Moi kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Alipigwa risasi ya mguuni wakati akipita karibu na duka la Said baada ya mashabiki wa Simba waliokuwa wakisherekea ushindi wa timu yao kupita katika eneo hilo.

Hata hivyo, alimaliza kesi hiyo nje ya mahakamani kwa kuwapa hela wazazi wa mtoto huyo.

Pia anamiliki genge la Wahalifu ambalo analitumia kumlinda na kuwaadhibu wapinzani wake au maadui zake akishirikiana na mdogo wake Ghalib Mohammed Saad.

Kundi hilo linalojulikana kama Ze Popobawa ndilo ambalo Agosti mwaka huu lilitumika kumteka nyara Mlebanoni mfanyabiashara ambaye ana duka la vitu vya ndani Mtaa wa Morogoro karibu na makutano ya barabara za Morogoro na Bibi Titi na baadaye kumwingilia kinyume cha maumbile kisha kumpeleka kwa nguvu Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kumrejesha kwao Yemen kinyume cha taratibu.

Kisa kilichofanya mfanyabiashara huyo ambaye yupo nchini kisheria ni kumpa mimba mdogo wa Said anayeitwa Salha bila ya kuoana kama zilivyotaratibu za mila zao za Yemeni.

Mfanyabiashra huyo wa Mlebanoni ambaye awali alikuwa rafiki yake mkubwa na Said, amemfanya tangu tukio hilo litokee kuishi kwa kujificha kwa kuhofia kufanyiwa unyama mwingine na Said ambaye anaendelea kumtisha.

Unyama mwingine

Baada ya kumfanyia unyama mfanyabiashra Mlebanoni , Said hakuishia hapo bali aliamua kumwadhibu dada yake Salha kwa kumpiga. kumnyoa nywele zake zote na kumnywesha vidonge ambavyo havijulikani aina yake na alimpa kwa sababu zipi?

Salha baada ya kufanyiwa nyama huo nyumbani kwao Msasani wilaya Kinondoni aliamua kwenda kuripoti polisi kituo cha Osterbay ambako lilifunguliwa jalada la kesi namba OB/RB/13915 ambayo ilifunguliwa Agosti 5 mwaka huu.

Hata hivyo, mbali ya polisi kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini wanashangaa tangu Salha aripoti tukio hilo, hajarudi kituoni hapo wala simu yake mkononi ambayo aliicha namba zake kituoni hapo wakati akiandikisha maelezo haipatikani, kitu ambacho kinawapa wasiwasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye anasema huenda suala hilo wamelimaliza kifamilia. Ingawa kuna tariafa kuwa msichana huyo amewekwa kizuizini chumbani ambako haruhusiwi kutoka nje. Polisi kituo cha Oysterbay hawajafuatilia suala hilo kutokana na kupozwa kwa kupewa kitu kidogo rushwa na Said ili kuzima suala hilo.

Ushirika wa kihalifu

Kutokana na kushirikiana vyema katika shughuli za dawa za kulevya na kutorosha nyara za taifa wakimtumia Mfanyabiashara huyu, Said, Manji ameamua kumpa vijana wake wa Orijino Commedy kuwapa ufadhili wa kutangaza bidhaa zake anazoingiza nchini za mashuka na nguo.

Hivi karibuni baada ya Manji kushiriki katika kuigiza mchezo wa kikundi cha Orijino Comedy kama mfanyabishara ambaye alikuwa akihitaji msaada wa kupata fedha za kufadhili Klabu ya Yanga na kuwapa wagizaji wa kikundi hicho kutumia ofisi yake kuigiza, Said naye wiki iliyofuatia aliwapa wana kikundi hicho nafasi kuingiza katika ofisi yake na kuwapa gari lake kulitumia.

Wizi wa makontena bandarini

1. Mfanyabiashara huyu anamiliki kampuni nyingi za Clearing and Forwarding ambazo hutumika kuiba makontena ya bidhaa anazoziingiza nchini kutoka nje na akishirikiana na baadhi ya wafanyakazi wa TRA.

Hata hivyo, Kampuni hizi zimefungiwa baada ya kubaini kuhusika na wizi huo wa makontena, lakini kila inayofungiwa husajili nyingine Brela akitumia majina feki.

Kampuni ambazo zimefungiwa na TRA kwa kuhusika na wizi wa makontena zaidi ya 30 kila moja ni Mbasi Clearing and Fowarding, Clinton Clearing and Forwarding, London Freight Forwarding, Exceptional Freight Forwaders na Upland Clearing and Forwarding.

TRA imethibitisha kuzifungia kampuni hizo kufanya kazi ya Clearing and Fowading, kwa kutumia kifungu 145 (3) cha sheria ya Jumuia ya Afrika Mashariki ya utawala wa Forodha ya mwaka 2004.

Hata hivyo, wamekataa kutaja majina ya wamiliki wa kampuni hizo wakisema Brela ndio wenye jukumu hilo. Ingawa wamekuwa wakikubali kuendelea kumhudumia mteja huyo huyo ambaye anaiba makontena na kufungiwa kampuni zake kisha anafungua nyingine chap chap kama uyoga.

Hata hivyo, Brela kuna kumbukumbu ya kampuni mbili tu ambazo ni London Freight Fowarders Ltd yenye usajili namba 39834 iliyosajiliwa Agosti 15, 2000 ikionyesha wamiliki wake ni Angelo Peter mwenye hisa 2000, Richard Mulenga mwenye hisa 1500 na Abdulkarim Zaharan Salim mwenye hisa 1500. Kampuni hiyo ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

Kampuni nyingine za kwake zenye kumbukumbu Brela ni Exceptional Freight Fowarders Ltd ambayo wamiliki wake ni Lumba Nguku mwenye hisa 5,000 na Salim Suleiman mwenye hisa 5,000. Kampuni ilianzishwa ikiwa na mtaji wa sh milioni 10.

Dawa za kulevya na kutorosha nyara

Mfanyabiashara huyu anajihusisha na uingizaji wa dawa za kulevya nchini kwa kushirikiana na mfanyabiashara Manji wakitumia kampuni zake za Clearing and Fowarding ambazo huiba makontena yenye dawa hizo yanapoingia bandarini.

Mfanyabiashara huyu ni mmoja wa watu waliotajwa katika orodha ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya iliyowasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2006 akitajwa kama Said Abuu mfanyabiashra wa Kariakoo.

Nyara za taifa

Mfanyabiashara huyu amekuwa akitumia kampuni zake kusafirisha makontena yenye nyara za taifa kwenda Vietnam, Philipiness na Malaysia akishirikiana Manji na Rostam Aziz ambaye pia ni mmiliki vitalu vya uwindaji. Kampuni ya Rostam ya Uwindaji inaendeshwa na mdogo wake anayeitwa Akram.

Ili kufanikisha mtandao wao huo wana watu wao katika sehemu nyeti za TRA, bandari, Polisi na usalama wa taifa unaowalinda kwa hali na mali.

Utajiri wa kutisha

Kutokana na Said kujihusisha na biashara hizo haramu kwa muda mfupi tangu mwaka 2004 alipoanza hivi sasa ana utajiri wa kutisha. Anamiliki nyumba sita eneo la Kariakoo pekee.

1. Moja ipo Swahili na Msimbazi, Ghorofa saba ambayo ameamua kuipangisha watu sehemu ya juu, lakini TRA akidaganya kwamba ni hoteli ili kukwepa kulipa kodi.
2. Congo na Agrey ghorofa sita,
3. Uhuru mkabala na shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa bado inajengwa ni ya ghorofa,
4. Livingstone na Uhuru ipo,
5. Mkunguni Kariakoo Sokoni karibu na dula la Azam Ice Cream ghorofa sita,
6. Lumumba karibu na CCM makao makuu limepakana na Hospitali ya Burhan.

mtoa mada ile campuni inayoitqa silence pua ni yake?
 
Kuna kitu ambacho mi nimekigundua mkulu kwa sisi wanyonge ndio sifa kututumbua ila kwa madoni thubutu na mm hapo ndipo namdharau mkulu wetu inamaana power yake ni kututia adabu sisi kajamba nani tena nilisikiaga tetesi alishawahi kumwambia mkulu wetu kipindi hicho waziri kwamba siongei na mbwa bali naongea na mwenye mbwa
 
Mhh..is this real ama majungu haya?

Hivi watu wa usalama wana uzalendo na hii nchi kweli?

Afu kwa nijuavyo Tz huwezi kuwa na uraia wa nchi mbili....,huku lazima ukane Uraia wa nchi moja...

Majitu kama haya unaya eliminate tuu...! Hawa ndo wakung'oa kucha sio kina ulimboka...

Huku ingekuta ni korea, unapigwa risasi afu tunakusahau...

Sasa TISS wanadeal na kina Ben saanane amabo wanamiliki bustani ya mgomba tuu huko Rombo..ili hali kuna washenzi kama hawa..
 
Naona heading imekuwa doctored,
mwaka 2012 hakukuwa na GSM FOUNDATION,

wala huyo said sio boss wa GSM FOUNDATION.

hizi habari ni sawa tu na uzushi wa magari 700 ya washawasha
 
6a2c7374f358e9ce241e6aa7ba5ba5fc.jpg
 
Mdogo wao kupewa mimba wamembabu SEYA kijana wa watu. Mbona huyo Ghalib kaaribu(rusha ukuta) sana watoto wa kibongo China serikali haija mbabu Seya?
 
Back
Top Bottom