Mfanyabiashara Said Mohammed Saad wa Home Shopping Center (GSM Foundation)

Mfanyabiashara Said Mohammed Saad

Utangulizi

Mfanyabiashara Said Mohammed Saad anamiliki Kampuni ya Home Shopping Center
Mfanyabiashara huyu ambaye ana uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Saud Arabia,
Report za Kipolisi nilizisoma kwenye thread humu Kuwa ni Raia wa Lebanon na si Mtanzania kwa maana hiyo...

Mwingereza adakwa na nyara za serikali


Na Bilal Soud


RAIA wa Uingereza, Robert Dewar, amekamatwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh 118,314,900 jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, mtuhumiwa huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trans Afrikas Logistics (TALL), akikamatwa Agosti 9, mwaka huu, akiwa na nyara hizo.

Alizitaja nyara hizo kuwa ni vipande vinane vya meno ya tembo, vinyago 11, meno ya tembo 20, meno 20 na kucha 22 za Simba, ndege mmoja aina ya kasuku, vipande vya miti ya mpingo na idadi kubwa ya vinyago, vyote vikiwa na uzito wa kilogramu 24.

Mtuhumiwa huyo pia alikutwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa ni madini pamoja na ganda moja la bomu lenye ukubwa wa milimita 130.

Kamishna Kova aliongeza kuwa mtuhumiwa amekuwa akisafirisha vitu hivyo sehemu mbalimbali duniani, na kwamba atafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Katika hatua nyingine,
Jeshi la Polisi limeahidi zawadi nono ya sh milioni 100 kwa mtu atakayetoa au kufanikishwa kukamatwa wahalifu wanaotuhumia kutumia tindikali kuwadhuru watu mbalimbali.

Kamishna Kova alisema kuwa matukio hayo yamekithiri nchini, ikiwamo tukio la raia wa Lebanon ambaye ni Mkurugenzi wa Home Shopping Centre jijini Dar es Salaam kumwagiwa kemikali iliyomletea madhara makubwa.

Katika hatua nyingine, watu wawili wamesomewa shitaka katika Mahakama ya Mwanzo ya Wilaya ya Ilala wakikabiliwa na tuhuma za wizi wa kutumia silaha.

Washtakiwa hao, Abdalla Shamte (30) na Mussa Hassan (40) wanadaiwa kuiba mabati 47 na vipande 11 vya mbao, vyenye thamani ya sh 3,084,000 mali ya Dk. Justine Paul.

Washtakiwa wote walikana kosa hilo lilisomwa na Mwendesha Mashtaka, Munde Hamisi, mbele ya Hakimu Joyce Minde.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 26, mwaka huu na washtakiwa walipelekwa rumande.

Au Kuna kitu kinafichwa behind? na hiyo zawadi nono nadhani itakuwa imeongezwa na huyo jamaa navyojua mimi uwezo wa Serikali ni million kumi tu dollar elfu sita na ushee
 
Shughuli pevu iyo! Kwa mantiki nyingine HSC ni biashara anayoitumia kusafisha hela sio?

Je records zake zinasema hana mkopo benki yoyote?

Mtaji wa biashara yake ambayo inaonekana ni legit, ambayo ni HSC alipata wapi?

Idara za juu za TISS zinampango gani na mtu huyu?

Nzowa anasemaje pia?

Kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo, ila za mwizi arobaini, lazma atanasa tu siku moja!



kaka watu kama hawa ni wengi ktk nchi hii. watu tunaowategemea wawakamate watu wa aina hii, ndiyo hao hao wanaowalinda.watakamatwa na akina nani??????? hii hali inauma sana.
 
Ngpja nirnde kanisani kwanza nkasali.. nchi hii IMEOZA

uploadfromtaptalk1376802133552.jpg
 
Ndiye huyo aliyemwagiwa tindikali? JHe waliofanya hivyo walikuwa wanalipiza kisasi? Kama hayo ni kweli, basi hapo ndipo swala la udhaifu wa serikali unakuja tena. serikali ndiyo inayofanya raia wajichukulie sheria mkononi, jambo ambalo siyo zuri.
 
Badala ya kuanza kushambuliana wa JF tungeuliza maswali muhimu k.m. inakuwaje huyo jamaa ana uraia wa nchi mbili (duo nationality)? Immigration kazi kwao!
 
"THAT'S MEAN IN SHORT, AMEIWEKA NCHI YETU MIFUKONI MWAKE"who's to blame! only CCM huyu mtu kumbe mnyama! smuggler,cheater,REAL WE DONT HAVE GOVT.
 
Umeongea mengi sana kuhusu Said kuna ya ukweli kuhusu majengo lakini mengine naona una sababu zako binafsi...halafu ilo ghorofa unalosema lipo Swahili na Udoe sio Swahili na Msimbazi Mbona huyo RPC wa siku nyingi sana mkuu. Mkuu kama mzalendo na unapenda nchi yako kwa nini huu ushahidi wako usipeleke polisi.
Utakufa kifo kibaya sana wewe!
 
Back
Top Bottom