Mfanyabiashara JJ bado anatafutwa na Interpol -Waziri

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,147
Mfanyabiashara JJ bado anatafutwa na Interpol -Waziri
Na Michael Uledi, Dodoma

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Lawrance Masha, ameliambia Bunge kuwa Jeshi la Polisi nchini linashirikiana na Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) ili kumtafuta, Mfanyabiashara Jaffar Abubakar maarufu kwa jina la JJ wa mjini Moshi, ambaye anatuhumiwa kumwua kijana Peter Swai, kwa kumchoma moto, kwa kile kinachodaiwa kuwa walimsingizia kuiba Sh 150,000.


Waziri huyo alikuwa akijibu mchango wa maandishi wa Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Owenya (Chadema) aliyeliibua suala la mkazi huyo wa Moshi mjini, aanayedaiwa kuuawa kwa

kuchomwa moto kama ndafu na mfanyabiashara wa mjini humo ajulikanaye kwa jina la Jaffar Abubakar maarufu kwa jina la JJ na mwenzake, Haruna Yusuph.


Kutokana na hali hiyo, Waziri Masha alisema kuwa, ni kweli kuwa dereva huyo aliunguzwa na kwamba ulifanyika upelelezi mara ya kwanza na Jeshi la Polisi na ikabidi ufanyike uchunguzi mwingine.


''Kwa bahati mbaya, pale ambapo tulifanya upelelezi mara ya pili na tuakaamua kuchukua hatua dhidi ya mtuhumiwa, mtuhumiwa huyo alitoroka nchini na sasa hivi tubashirikiana na wenzetu wa Interpol ili kuweza kumtafuta mtuhumiwa huyo,'' alisema Waziri Masha.


Owenya katika mchango wake wa maandishi aliochangia katika bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani, alidai kuwa Swai aliuawa kikatili kwa kumwagiwa mafuta ya taa na kisha kuchomwa moto, akisingiziwa kuwa aliiba Sh 150,000, madai ambayo hayakuwa kweli.


Kwa mujibu wa Mbunge huyo, fedha hizo zilidaiwa kuwa zilikuwa zimeibiwa katika hoteli, ambapo hata hivyo, baada ya kumchoma moto Swai, walikwenda kupekua ndani ya hoteli hiyo na kukuta fedha zile ndani ya mto.


“Aliyeibiwa alikuwa ametoka kwenye harusi na ulevi wake, akaficha fedha zile kule na kusahau alipoziweka na kwa kuwa walijuana na wakubwa, wakati huo JJ akachukua sheria mkononi na kumchoma kijana Swai,” alisema Owenya katika mchango huo wa maandishi ambao, Mwananchi inayo nakala yake.


Pia alisema kuwa, miongoni mwa mambo yanayotia mashaka ni pamoja na harusi ya dada yake Jafar Abubakar(JJ) ilihudhuriwa na maofisa wa andamizi katika jeshi la Polisi wakati huo Mkuu wa Jeshi hilo, Omary Iddi Mahita na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Mohamed Chiko.


Alisema kuwa, kutokana na hali hiyo, kulijengeka hisia kuwa haki isingetendeka kwa kesi ya marehemu, na kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wakati ule, Adadi Rajab, baada ya watuhumiwa kukimbilia kusikojulikana aliagizwa atafutwe.


“Swali, hakuna tangazo lolote lenye picha za watuhumiwa zinazoonyesha wanatafutwa. Yawezekana kabisa labda wapo ndani ya nchi, lakini bila picha zao watu watajuaje wanatafutwa?” alihoji Owenya katika mchango wake

huo wa maandishi.
 
samaki wakubwa wataendelea kuwala samaki wadogo, simba wataendelea kuwala nyumbu na swala!!!!
lakini siku na saa ya mapinduzi ipo...!
 
Back
Top Bottom