"Kilaza" Mfano mzuri wa ukuaji wa lugha ya Kiswahili

Inasemekana Juma Kilaza na Mwinshehe wote wakiwa wanamziki, walibishana kila mmoja akitamba kuwa na uwezo kumshinda mwenzake hasa kwenye upigaji wa vyombo kama gita. Waliandaliwa tamasha la kuwashindanisha, Juma Kilaza alishindwa vibaya sana na Mwishehe. Kuanzia hapo watu wote wenye uwezo kidogo walianza kuitwa KILAZA!
 
Mbaraka Mwinshehe na Juma Kilaza walikuwa ni mahasimu wa aina yake.

Alipofariki Salum Abdalah ambae ndie alikuwa kiongozi wa Cuban Marimba ndipo Juma Kilaza akashika usukani kuongoza bendi hiyo.

Kama mnakumbuka wimbo wa "Mkono wa Iddi" ulitungwa na Salum Abdalah.

Lakini Juma Kilaza akaanza zogo mjini Morogoro kwa kuimba wimbo wake uitwao Dada Kidawa (lakini nakaribisha mwenye kumbukumbu anirekebishe hapa).

Ndipo kuona hivyo Mbaraka akamjibu kutaka kumtuliza Juma Kilaza na kumkumbusha kwamba pale mji kasoro bahari pana walotangulia, akatunga kwa wimbo wake usemao "Matusi ya nini?"

Hii ni sehemu ya wimbo huo wa Mbaraka Mwinshehe kwenda kwa Juma Kilaza:

"Tulikua na Salumu mpaka kaenda Ahera wala hatukutukanana,
Alipoingia yeye aliyoleta si miziki bali ni matusi,
Mji wa Morogoro ulisifika sana kwa mambo ya miziki na nyimbo zenye maana ooo,
Amekuja mchafuzi wa jina la Moro Jazz na Mororgoro nzima,
Chorus Huyooo aona kijicho Sululu la chuma liko Imara,
Matusi yake Mjini Morogoro yameleta sifa mbaya,
Sifa ya Moro jazz ni ya Taifa chuki yake ni ya bure"

Juma Kilaza alikaa na kutafakari sana juu ya ujumbe huu, anapoambiwa atulie Morogoro.

Mwenyezi Mungu azidi kuwarehemu wanamuziki hawa magwiji.
 
Tunaomba msaada wa tafsri toka hizi taasisi za polisi, mahakama na wanasheria,Tuki na viongozi Wa serikali.

Tunaomba hiyo tafsiri ije haraka naona ishakuwa hatari huku mtaani na hivi vi smartphone vyenye whatsapp tutaishia jela.

Neno kil.aza ni tusi?
 
Kil.aza linaweza lisiwe tusi....isipokuwa linaleta maana mbaya kulingana kusudio la anayetaja neno kwa mlengwa wake.....

Vile vile katika kipindi hiki linaleta tafsiri mbaya.....kulingana na linavyotumika kipindi hiki.....
 
tunaomba msaada wa tafsri toka hizi taasisi.
polisi
mahakama na wanasheria
Tuki
viongozi Wa serikali

tunaomba hiyo tafsir ije haraka naona ishakuwa hatari huku mtaani na HIV vi smartphone vyenye whatssap tutaishia jela.

neno kil.aza ni tusi?
Ngoja mahakama itatoa tafsiri na ikiwezekana tafsiri itoke Court of appeal.
 
tunaomba msaada wa tafsri toka hizi taasisi.
polisi
mahakama na wanasheria
Tuki
viongozi Wa serikali

tunaomba hiyo tafsir ije haraka naona ishakuwa hatari huku mtaani na HIV vi smartphone vyenye whatssap tutaishia jela.

neno kil.aza ni tusi?
Polisi watakuja kulitolea ufafanuzi hili.
 
Back
Top Bottom