Mfalme wa Uhispania awaomba samahani raia wake

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Mfalme wa Uhispania, Juan Carlos, amewaomba samahani raia wake kwa kosa la kwenda "Safari ya Mawindo" Botswana huku taifa lake linakabiliwa na hali ngumu ya uchumi. Katika safari hiyo Mfalme Juan Crlos alipata ajali na kurejeshwa Uhispania kwa matibabu.

Samahani hizo zinakuja baada ya maoni tafauti ya wanaharakati na wanaomuunga mkono, kuwa "Iweje mkuu wa nchi aende safari ya mawindo ambako ada ya kuua tembo mmoja tu ni kiasi cha shilingi milioni 60, wakati nchi inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi.

Akiwa kwenye mlango wa hospitali alikokuwa amelazwa, Juan Carlos alisema, "Ninawaomba samahani, mnisamehe. Nimefanya makosa na sitorudia tena."

Hoja yangu, Watanzania hatustahiki kuombwa msamaha na Vasco da Gama wetu, ambaye kila siku nchi inadidimia katika matatizo na yeye ndio kwanzaaaa, kama aliyelishwa miguu ya kuku, kila siku safarini?
 
Siku litakapomkuta kama lililomkuta mwenzake ndo atajua nini maana ya kutulia nyumbani.
 
Back
Top Bottom