Mfalme wa Qatar atua Zenj kwa mbwembwe

kwamwewe

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,801
541
Mfalme wa Qatar, Ahmad Bin Khalifa Al Thani amewasili Zanzibar kwa mbwembwe akiwa katika mapumziko ya Eid el Fitri yatakayochukua muda wa wiki moja na kulala katika boti ya kisasa iliyofunga nanga katika mwambao wa bahari ya Zanzibar.

Mtawala huyo wa Qatar aliwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akiwa katika ndege aina ya Air Bus 340, akiwa na wasaidizi zaidi ya 42 mnamo saa 4 juzi usiku.

Akiwa ameambatana na mkewe na watoto, baada ya kuwasili alielekea katika bandari ya Malindi na wasaidizi wake walikwenda moja kwa moja katika hoteli ya kimataifa ya La Gema, iliyopo katika kijiji cha Nungwi, mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mfalme huyo amekuwa akilala katika boti maalum yenye huduma zote ikiwemo ulinzi na usalama mkubwa, boti hizo mbili ambazo ziliwasili Zanzibar siku mbili kabla ya kufika kwake.

Baada ya kuwasili katika bandari ya Malindi boti maalum inayomilikiwa na kampuni ya Azam Marine ilipewa jukumu la kubeba mizigo ya wageni hao kupeleka katika boti za mfalme.

Wasaidizi wa kiongozi huyo wameibua mjadala mkubwa Zanzibar kutokana na msaada wa kifedha wanaotoa kwa vijana wanaowasidia shughuli zao, baada ya juzi vijana waliokuwa wakiwabebea mizigo kulipwa dola 100 kila mmoja kwa kazi ya saa moja.

“Kweli leo nimeamka vizuri sikutegemea kupata dola 100 kwa kazi ya saa moja kupeleka mizigo na kuja kwa mfalme ni faraja kubwa kwetu”, alisema mfanyakazi mmoja.

Hata hivyo, ndege iliyomleta mfalme huyo baadaye iliondoka uwanja wa ndege Zanzibar kulekea Dar es Salaam ambako itaegesha kumsubiri mfalme hadi atakapomaliza mapumziko yake kutokana na uwanja wa Zanzibar kuwa na nafasi ndogo.

Imeelezwa kwamba mfalme huyo akiwa Zanzibar atajishughulisha na michezo ya baharini, ikiwemo kuzamia, ambapo pia atafanya ziara kama hiyo kisiwani Pemba pamoja na kutembelea baadhi ya visiwa vidogo viliyopo Zanzibar.

Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma amethibitisha kuwasili kwa kiongozi huyo, lakini alisema ziara yake ni ya kibinafsi na sio ya serikali.

Hata hivyo, alisema kuja kwa kiongozi huyo ni faraja kwa Zanzibar hasa katika kutangaza sekta ya utalii na kuizihirishia dunia kuwa Zanzibar ni nchi ya amani hasa wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Zanzibar imewahi kuwa na mfumo wa uongozi wa Kifalme kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Waacheni Wanzazibar wawe nchi hata Muungano wakitaka wavunje tu...Kwanini watung'ang'anie sie wakati nchi imevunda kwa rushwa..Wakati umefika tuamke tuipiganie Tanganyika yetu iliyonajisiwa kwa miaka kadhaa tuache kushupalia ya watu yakwetu yanatushinda.
 
hapo kaletewa vimwana bikira vya kitanzania kwaajili ya kuwaburudisha , waarabu hawa wamekuwa wakifanya hivi kule Loliondo hawana maadili ni wachafu sana na pesa zao za mafuta.
 
hapo kaletewa vimwana bikira vya kitanzania kwaajili ya kuwaburudisha , waarabu hawa wamekuwa wakifanya hivi kule Loliondo hawana maadili ni wachafu sana na pesa zao za mafuta.

Mbona mavuvuzela haya hayakusikika wakati alipokuja BUSH Tanganyika?.
 
hapo kaletewa vimwana bikira vya kitanzania kwaajili ya kuwaburudisha , waarabu hawa wamekuwa wakifanya hivi kule Loliondo hawana maadili ni wachafu sana na pesa zao za mafuta.

Kumbuka amekuja na mke wake!
 
Naona tayari utumwa unarudi zanzibar,hivi tayari tushawaachia hako kakisiwa ama bado??kelele zao zote sababu kubwa ni hiyo,mwarabu arudi awapakate.
 
Soma sentensi ya mwisho......ndio wanarudi hivo....ukitoa $100 kwa watu 1,000,000 nchi ni yako...what is $100m to him?

Acheni wenye pesa zao wapumzike na watutangazie nchi yetu huko ughaibuni. Maana huko Ughaibuni ukitaja Uganda, mara moja watakwambia 'Idd Amin'. Sasa taja Tanzania ni mtafutano, mpaka aingie kwenye mtandao, wapi na wapi.
 
Acheni wenye pesa zao wapumzike na watutangazie nchi yetu huko ughaibuni. Maana huko Ughaibuni ukitaja Uganda, mara moja watakwambia 'Idd Amin'. Sasa taja Tanzania ni mtafutano, mpaka aingie kwenye mtandao, wapi na wapi.


Hahahhahah! acha nicheke kwanza, maana hayo uliyosema yananikuta kila siku. Idd Amin wanamjua kama nini, Kenya wanaijua kwa kufukuza upepo. Tanzania, mmmmmmmmmmmhhhh labda uanzie kilimanjaro mountains. ndo uje Tanzania.
 
Back
Top Bottom