Mfalme juha:milioni 100 kumuua mnyama.

LUCIFER

Senior Member
Aug 14, 2012
183
88
Habari zenu Wana JF....!
Leo sina mengi ila kuna jambo nimelisoma kwenye magazeti kadhaa ya Leo kwamba Kibopa mmoja wa Yanga ameandaa milioni 100 kama timu yao itamfunga Mnyama....Nikafikiria zilikuwa wapi hizi pesa wakati timu inalala wawili wawili kwenye mgahawa wa mbavu za mbwa mbeya?kutakuwa na kipi special kama YEBOYEBO mtamfunga MNYAMA halafu timu ikakosa ubingwa na kuendelea kushiriki mashindano ya ndani?Mjipange,acheni kukurupuka hata ukuta wa ROME haujajengwa kwa siku moja....Tunataka mpira hizo style za kumwaga pesa kwa ajili ya kuhonga viongozi na marefa ili umfunge Flani zifike mwisho.Saudia Arabia na pesa zao walipigwa 8-0 Kombe la dunia....
Narudia tena ni muhimu kutoa pesa pale zinapohitajika,na si kutoa pesa pale unapohitaji kutoa...huo ni UFALME JUHA!
NAWASILISHA
DSC02170-450x600.jpg

DSC02177-424x600.jpg
 
Nakubaliana na wewe kabsa, kweli yule dogo ni mfalme juha. Timu ina madeni mpaka fifa wanalitambua hilo, them milion 100 kuifunga simba wakati hata wagosi wa kule tanga coastal union wanawazidi point.
ama kweli wajinga ndio waliwao. Mnyama ataendelea kuwapakata...
 
Zile TANO bado zinawachanganya.........inanikumbusha utotoni nilimdunda jamaa wakati wa PASAKA akanivizia mpaka CHRISTMAS na bado nikamdunda tena
 
mkuu nadhani hii pesa ingetumika kuwalipa papic njoroge mtakatifu 'tom n jerry' ingekuwa busara zaidi.

Sent from my blackberry 9300 using jamiiforums
hehe mbona mnauchungu na hizo milioni sijui ngapi waacheni wazitumie kwani nyie kinawauma nini?au hakuna mgawo wenu?eheeeeeee vituz vinakuja tusubiri.its like simba has nothing to loose right?
 
...Ni zile za Meremeta... na huyo aliyetoa ahadi, ni yule yule msanii ambaye inji yake watu wanakufa njaa lkn yeye anashinda ana text na Lulu.... !!
 
Mleta hoja, una hoja nzuri tu. Na hii ni kwa timu zote simba na yanga wanajiandaa kwa sifa na mbwembwe kwa ajili ya uchawi na kuhonga. Haifai kwa sababu ni furaha ya muda mfupi.

LAKINI badilisha id yako maana kuitwa shetani duuuu .........................
 
@LUCIFER hebu badili ID yako tafadhali sio nzuri hata kidogo. Bora hata ujiite Shetani walau kuliko hilo jina

back to the point. Watapunguza idadi ya magoli kutoka 5-0 hadi 3-1 maana timu yenyewe haina kocha.
 
Mbona mnaweweseka na pesa isiyotoka mifukoni mwenu?Nyie akina nani mpaka mtupangie how to spend our cheddar?If you have nothing valuable to tell us then you better keep mum!
 
Wameanza kutafuta sababu mapema,wakifungwa waseme ni zile Mil 100 kama vile walikuwepo wakati hiyo cheque ikiandikwa.
 
Eti sababu,kwa tim ipo ya kuifunga simba?na kwa taarifa yenu msimu huu tunatoka unbeaten,
 
habari zenu wana jf....!
Leo sina mengi ila kuna jambo nimelisoma kwenye magazeti kadhaa ya leo kwamba kibopa mmoja wa yanga ameandaa milioni 100 kama timu yao itamfunga mnyama....nikafikiria zilikuwa wapi hizi pesa wakati timu inalala wawili wawili kwenye mgahawa wa mbavu za mbwa mbeya?kutakuwa na kipi special kama yeboyebo mtamfunga mnyama halafu timu ikakosa ubingwa na kuendelea kushiriki mashindano ya ndani?mjipange,acheni kukurupuka hata ukuta wa rome haujajengwa kwa siku moja....tunataka mpira hizo style za kumwaga pesa kwa ajili ya kuhonga viongozi na marefa ili umfunge flani zifike mwisho.saudia arabia na pesa zao walipigwa 8-0 kombe la dunia....
Narudia tena ni muhimu kutoa pesa pale zinapohitajika,na si kutoa pesa pale unapohitaji kutoa...huo ni ufalme juha!
Nawasilisha
View attachment 66420

View attachment 66421
sababu wanaotoa hizo milioni 100 hawana interests na maendeleo ya soka...bali wanatafuta sifa itakayoweza kuwa shield kwenye mambo yao mengine ya kidunia...ni suala la "total mind control" nadhani lucifer unajua hii theory
 
kwani simba hawana wa kuwapatia milioni 100?..hahaha, yule kibaka mbunge wa tabora hana iyo hela...si alienda ndani kwa kuiba laki nane...hahaha. mnyama bwana hata hamjui watu wa kuwaweka kama viongozi...
 
Kama uwanjani zinacheza noti sawa, lakini kama ni wachezaji ishirini na mbili bado hizo milioni mia hazitasaidia kitu.
 
Back
Top Bottom