Mfalme HERODE Na RC wa Dodoma...!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Wengi tulishasoma habari za Mfalme Herode wa Israel jinsi alivyoamua kuua watoto wote wachanga wa kiume, baada ya kupata habari kutoka kwa Mamajusi wa Mashariki, kuwa amezaliwa mtoto ambaye atakuwa mfalme wa Uyahudi nzima.

Herode alikuwa na wasiwasi kuwa mtoto huyo aliyezaliwa atampora nafasi yake ya Ufalme, na kumharibia heshima yake kwa jamii! Lakini pamoja na Herode kufanikiwa kuwaua watoto wote wa kiume huko Bethehemu, Yesu alisalimika baada ya wazazi wake kuonywa kupitia ndoto kuwa wakimbilie Misri wakajifiche huko.

RC wa Dodoma jana alipiga marufuku mikutano ya Kisiasa mjini Dodoma kwa kisingizio cha uwepo wa vikao vya Bunge, na hivyo anahofia wageni kuwa wengi mno Dodoma kiasi cha kushindikana kudhibitiwa.
Je mkuu huyu wa mkoa ametafiti na kukuta kuwa mikutano ya siasa inaleta wageni wangapi mjini Dodoma?
Lakini hapohapo sheria ya nchi hii inaruhusu raia yeyote kuwepo sehemu yoyote ya nchi hii, ili mradi kama hahalifu sheria. Pia mikutano ya kisiasa ni haki ya msingi ya vyama vya siasa.

Hakuna kumbukumbu zozote zilizoonyesha kuwa mikutano ya kisiasa imeshawahi kukwamisha shughuli za Bunge, maana mikutano hii inahudhuriwa na wananchi wa kawaida ambao si sehemu ya Bunge.

Ikumbukwe pia kuwa amri hii imekuja baada ya chama cha Chadena kufanya mkutano wakemkubwa leo katikA Viwanja vya Barafu Mjini Dodoma.

Je, katazo hili la Mkuu wamkoa wa Dodoma ni kama hofu ya Mfamle Herode ya kuzaliwa kwa Chama kitakachochukua madaraka ya watawala waliomweka madarakani?
...tujiulize na kutafakari!
 
Na ndio ile ya kitimoto kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe!...macho na ubongo wao viko kwenye likizo!

Mambo ya kulipa fadhila hayo. Hakuna la maana analoliongea zaidi ya kufuata maagizo ya kijinga aliyopewa. Hii inanikumbusha kipindi ile walipozuia maandamano ya kupinga DOWANS kulipwa kwa kisingizio cha Al Shabab wakati huo huo timu ya Taifa ya Kenya ipo National Stadium inacheza Challenge huku majeshi ya Kenya yakipigana na Al Shabab huko Somalia.

Akili nzuri ukiwa nayo
 
Maoni yako yanakaribia sana na ukweli halisi, mkuu wa mkoa ameogopa sauti. Hivyo vyeo vya kupeana kishikaji ndiyo tatizo lake. Siku zao mbona zinahesabika!
 
Hawa wakuu Wa mikoa na wakuu wa Wilaya hivi vyeo wanapewa Kama zawadi kutoka kwa raisi.V8 bure marupurupu mshahara mkubwa,unafikiri ni nani controler kwa hawa watumishi zaidi ya raisi aliewateua!!!???
 
Bora angepiga marufuku mkutano wa Bunge kutokana na kuwapo kwa wageni hao wengi waliokwenda kwa ajili ya mikutano ya kisiasa
 
Du ukimuona alivyokuwa anaongea utazani kakaa chini na kuainisha ni usmbufu gani unaojitokeza wanasiasa wakifanya mikutano. Kwa kweli nazidi kuamini sasa kuna hof kubwa ya watawala kuhusu upepo. UTAZUIA MAANDAMANO,LAKINI KAMA SIKU ZMEFIKA HUTAWEZA KUZUIA MABADILIKO. NA HAPO KWA KWELI MIMI IMENISIKITISHA SANA KWA UPEO WA VIONGOZI WETI. AMALIZIE KABISA KWA KUSEMA "NI MARFUKU MAHUBIRI YOYOTE YA WAZI KWA DINI ZOTE HAPA DODOMA"
 
Lema malizia maombi uanze kazi ya ukombozi!
Wameyataka wenyewe sasa wacha wayakute!
Tuliwaambia badilikeni hawakusikia sasa tumebadilika sisi(wananchi)!

Kimenuka! Kimenuka!

Mkuu bahati mbaya ninatumia Mchina! Hii nimeipenda! Basi pokea Like ya mdomo mwanangu! Yaani wasomi wa TZ ubongo wetu umechina. Eti huyu naye ni Dr uuuuhwiiiii!! Hizi PhD za kwenye mtandao ni janga la kitaifa! Huyu sasa hata hatumii masaburi kufikiri bali anatumia Ku.m! Mods tuheshimiane!
 
Mimi bado sijazinduka kabisa kutokana na sababu alizotoa. Kama ni mkutano kuleta wageni, mbona zaidi ya asilimia 99 ya waudhuriaji bungeni ni wageni?? Kama hawatoi ulinzi kwa wageni basi wasimamishe na kikao cha Bunge. Pia hatutarajii mkutano wa kisiasa toka chama chochote ufanyike Dodoma.
 
Du ukimuona alivyokuwa anaongea utazani kakaa chini na kuainisha ni usmbufu gani unaojitokeza wanasiasa wakifanya mikutano. Kwa kweli nazidi kuamini sasa kuna hof kubwa ya watawala kuhusu upepo. UTAZUIA MAANDAMANO,LAKINI KAMA SIKU ZMEFIKA HUTAWEZA KUZUIA MABADILIKO. NA HAPO KWA KWELI MIMI IMENISIKITISHA SANA KWA UPEO WA VIONGOZI WETI. AMALIZIE KABISA KWA KUSEMA "NI MARFUKU MAHUBIRI YOYOTE YA WAZI KWA DINI ZOTE HAPA DODOMA"
...ukisikia mtu anaogopa kivuli chake ndo kama huyo RC mganga njaa...
 
...angepewa dsm wanakoingia wageni wengi kila leo ingekuaje!?
Ooooh! Angezuia magari, ndege, treni yote kuingia.
 
Wakati mwingine ukisikia amri kama hii kutoka kwa "Mkuu wa Mkoa" unajiuliza alifikaje hapo kama thinking capacity ndio hiyo aliyonayo.
 
Hii hali inatisha km mkuu wa mkoa anaongea vitu ambavyo havina maana ....mhh!!! ccm bwana ...wanavuta shuka na asubuhi imefika ....
 
Wekeni CV yake humu, tusipoteze Muda kumjadili mtu ambaye ana CV kimagamba magamba!

mengine hayahitaji hata CV kujua udumavu wa fikra zake;
  1. ameonyesha kwamba, pamoja na kuwa mkuu wa ulinzi na usalama, haamini jeshi na vyombo vyote vya kulinda sheria kulinda wabunge, in short ameonyesha kutoamini serikali yake kulinda watu wake wenyewe tena kwenye makao makuu ya serikali
  2. anaonyesha kutofanya proper intelligence ya kujua vyanzo vya threats za mkoa wake na hata kujua SWOT ya system ya mkoa wake wenyewe
  3. amefeli miserably kwa kuwa na knee-jerk reaction.... angesubiri basi afanye hata consultation na mikoa mingine kama Dar iliyozoea wageni tena wengine husinda kuomba-omba tu toka dodoma
In short; kusoma CV ya huyu mkuu wa mkoa ni sawasawa na kutafuta habari za uchumi kwenye magazeti ya shigongo

Hii ni kumbusho tu la namna tusivyowahitaji wakuu wa mikoa, kwani ni nafasi za kujaza wanapropaganda za kitoto
 
Back
Top Bottom