Meya wa Kinondoni afanya ufisadi

Mmarekani mtarajiwa. Naombea hukumaanisha nilivyokuelewa. Kama ni hivyo kwa mwendo huu utaishia lupango huko unakoishi. Naomba naomba unifahamishe hasa ulikuwa na maana gani au umwombe msamaha huyu dada yetu. Kama ni mimi mwenye mawazo mabaya naomba unisamehe.

Umarekani sitaki nahamia Bahama sasa.
 
2010 siyo mbali, kama ndio kampeni hizo, basi namimi nitaanzia humu humu kujiunga nao na kuondoa ufisadi Kinondoni. Duh hasira zingine bwana. Basi ndio kampeni hiyo.
 
""EMBE LIKISHADONDOKA HALIRUDISHIKI TENA MTINI**2

"MANENO YAKISHADONDOKA HAYARUDISHIKI MDOMONI""

"NYAMA IKIFIKA BUCHANI HAIRUDISHIKI KUWA NGOMBE""

"""Halifichiki hee hee alifichiki pembe la ngombe mwenzenu halifichiki""

"mwisho wao umefika jamani hawafichiki"
 
Cry the beloved country!!!!!!! Tanzania Tanzania tutatoka vipi kama mwendo wenyewe ndio huu??????
 
Kuna kitu watz hawaelewi,
ukiwa na chama kimoja kinachothibiti (kwa wingi wa wabunge au madiwani) taasisi fulani, then wanafanya mambo kienyeji bila woga.

2010 inabidi watz waelewe kwamba tunahitaji upinzani wenye nguvu, si kwa kukichukia chama 'twawala' ila ila kupata matokeo bora zaidi.
 
Naona gazeti la fisadi Rostam Azizi limeanza kuanika ufisadi wa mafisadi watoto. Ufisadi huanza kidogo kidogo na baadaye kufikia hatua ya kuiba mabilioni na kuanza kuua watu.

Masahihisho tu kwa nyie waandishi, hakuna kitu kinaitwa jiji la Florida hapa Marekani.




http://www.newhabari.com/mtanzania/habari.php?id=2238&section=kitaifa

NAPENDA KUWAKUMBUSHA WAANDISHI KUACHA KUWAKA HOVYO.ANGALIA SASA KUMBE NI UWONGO MTUPU LONDA WALA HAKUTAKA KUNUNUA VX MBOVU KWA MIL 3 BALI ALIPELEKA ZABUNI YA WAZI NA AKASHINDWA THEN NIAMBAIE KOSA MTU KUTENDA ZABUNI?KWA HIO ATA KUTENDA NA KUKUOSA NI UFISADI?SWALA LA KUPELEKA WATOTO USA KWA KUPITIA MSAFARA WA WABUNGE NA TENA WAMEJILIPIA WENYEWA NI UDHAIFU WA WATZ WENGI,WAPO WALIOENDA KWA MISAFARA YA DINI,WAPO KWA KUFUNGA NDOA ZA UONGO ILI WAPATE VIZA ETC.LAKINI WENGI WANAENDA KUISHIA KUOSHA VYOO NA KUFAGIA BARABARA,WANAKUWA THIRD CLASS CITIZENS,MIPANGO YAO YA SHULE INAKWAMA WANABAKI NA NDOTO ZISIZOTIMIA.
 
bIG UP,MWAFRIKA WA KIKE,hapa ubaoni kila fisadi ataaanikwa tu. Londa anasubiri nini kujiuzulu? kila kiongozi wa CCM awamu hii kajaa kashfa kibao. Kitaeleweka tu. Hili gazeti la fisadi Rozitam nalo linaanza kuleta habari za mafisadi ndani ya nyumba yake,isije kuwa kiini macho
 
Ni kosa kisheria kwa kiongozi kuogombania tenda yeyote na madiwani ndio kabisaaaa hawaruhusiwi kugombea tenda yeyote ndani ya halmashauri za wilaya au manispaa. Fisadi mtoto umenipata. na hili la Marekani,ni udhaifu wa kiongozi. Londa ajibu mapigo siyo weye kibaraka wake,
 
Huyu ni fisadi mkiubwa sana na kuna kila sababu ya kumtaka ajiuzulu kwani nakumbuka kuwa mbunge wa CHADEMA Halima Mdee alipolishikia bango suala hili la kiwanja cha shule kuuzwa na huyu fisadi alijifanya kulifanya kuwa ni issue ya kidini kati ya waislamu na wakristo hadi mkuu wa mkoa alipoingiloia na kuwataka watu wa ardhi kwenda kupima na kukuta wananchi wana haki na hiyo ardhi.

sasa sijui ataenda tena msikiti wa mtambani na kuwahimiza waisilamu kwa vipeperushi ili aweze kuuzima tena na moto huu ama ataanzia wapiu sijui.

Kitu kimoja kumbukeni ni kuwa inapowadia wakati wa kushughulikia mafisadi popote ulimwenguni historia inaonyesha kuwa wanaanguka wote hadi wale wadogo zao na hapa kwetu mnaweza kuanza kuona jinsi wanavyotafunana wenyewe kwa wenyewe.

Hawa wakina RA walimtafuna Jeetu Patel wakidhani kuwa watamwangusha peke yake kumbe wameliwa na sasa ona wanamwangamiza mshirika wao kwenye ufisadi naye huyu hatakubali kufa peke yake kwani kiwanja hicho alikiuza kwa baraka za mr.clean naona RA ananusa kuwa wanataka kumwaga hivyo anataka afe na mtu yangu macho.
 
Ni kosa kisheria kwa kiongozi kuogombania tenda yeyote na madiwani ndio kabisaaaa hawaruhusiwi kugombea tenda yeyote ndani ya halmashauri za wilaya au manispaa. Fisadi mtoto umenipata. na hili la Marekani,ni udhaifu wa kiongozi. Londa ajibu mapigo siyo weye kibaraka wake,

KAKA NYAMAZA KIMYA KUFICHA UJINGA WAKO,PROCUREMENT ACT YA MWAKA 2004 HAIZUII MTU YEYOTE KUOMBA ZABUNI YA UNUNUZI ILI MRADI HASIWE KWENYE TENDA BOARD YA EVALIATION NA KAMA YUKO KTK EVALUATION COMMETEE ANACHOFANYA NI KUDICLARE INTEREST NA KUTOHUDHURIA KIKAO
 
Hii imetoka kwenye Gazeti la Mtanzania Kuna Paragraph huko Chini imenifurahisha , aliwapa Waandishi 40thou kila mmoja kuwasaidia kurudi nyumbani


Londa azungumza
na beatrice moses

MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Alhaji Salum Londa, ameibuka na kudai kuwa tuhuma zote zinaripotiwa kwenye vyombo vya habari dhidi yake zinalenga kumdhalilisha.

Meya Londa alitoa madai hayo jana, alipozungumza na waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari nchini, kwenye Ukumbi wa Manspaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, Londa alisema amesikitishwa na kuchapishwa kwa kwa tuhuma hizo, kwa sababu hazina uthibitisho, na zinaweza kuleta madhara makubwa katika jamii.

Alidai kuwa, chini ya uongozi wake, Manispaa ya Kinondoni, ni moja ya manispaa ambazo zimeongoza kwa utawala bora.

Akizungumzia kuhusu tuhuma za gari ambalo alikuwa akilitumia awali, alidai kuwa siku zote anayejua ubovu wa gari ni dereva, na ndiye aliyetoa taarifa za ubovu wa gari hilo, ambalo ni kweli lilitengenezwa kwa Sh milioni 9, lakini kwa kufuata utaratibu wote unaostahili kiutendaji.

"Mimi nafikiri hapo cha kuangaliwa ni kwamba fedha zilizotumika kugharamia matengenezo ya gari hilo zilitolewa vipi? Zilifuata utaratibu unaokubalika, na gari halikupelekwa kutengenezwa kwenye gereji ya Londa, kwa hiyo zikaingia kwenye mfuko wake.

"Hapo labda kungekuwa na jambo la kuhoji, nilifikiri kwamba ningeonewa huruma, walitaka kuona Meya anatembea kwa miguu, maana gari lingine lililoagizwa lilichelewa kufika," alisema Alhaji Londa.

Alisema, anashangaa kuandikwa kwamba alitaka kulinunua gari hilo kwa Sh milioni 3, wakati yeye alitaka kulinunua kwa milioni 3.5. kwenye zabuni, hata hivyo alikiri kushindwa kwenye zabuni hiyo, ambayo alishinda mtu aliyetajwa kuwa ni A. S .Mohamed kwa Sh milioni 14,200,000.

"Mimi nashangaa sana jamani ndugu waandishi, zabuni hiyo sikuomba peke yangu, hata Mkuu wa Mkoa, Abass Kandoro, aliomba, ingawa yeye alitaka kununua Isuzu Tipper, lakini hakufanikiwa kupata, hii yote nawathibitishia kuwa Kinondoni kuna utawala bora, maana isingekuwa hivyo, angepewa bila taratibu za zabuni kufuatwa, na bila hata kuangaliwa kiasi chake cha pesa ambacho kilikuwa Sh milioni 3." alisema Londa.

Meya Londa pia alikanusha kutumia madaraka yake vibaya kutaka kumpeleka Amina Salehe Londa, ambaye ni mtoto wake Marekani, kwa kumjumuisha katika orodha ya madiwani vijana waliokuwa wamealikwa jijini Florida, mwaka jana na Taasisi ya Sister City International.

"Mimi nina watoto 12, wa kike sita, na wakiume sita, kati yao wengi wanaishi huko tangu mwaka 1996, Amina siyo mtoto wangu, ila ni kweli nilimchagua kwa sababu kwa nafasi yangu naruhusiwa kuchagua madiwani wawili.

"Sijakatazwa kuchagua hata mwanangu, ili mradi awe na sifa zinazostahili, hivyo nilimchagua huyo pamoja na mwanangu Haji Londa, lakini gharama za safari hazikutolewa na manspaa, bali walijigharamia wenyewe, ingawa Amina hakufanikiwa kupata visa," alifafanua.

Pia alikanusha kuiuzia Manispaa kompyuta, akidai kuwa hajawahi hata kuiuzia kalamu achilia mbali hizo kompyuta ndogo (laptop) 20, ambazo alidaiwa kurejea nazo kutoka Marekani kwenye safari hiyo ya madiwani vijana. Ilidaiwa kuwa, aliuza kila kompyuta kwa Sh milioni 3, bei ambayo ni kubwa ikilinganishwa na iliyopo kwenye soko.

"Sijawahi kuuza hata penseli kwa Manispaa, ingawa pia sizuiwi kurejea na kitu chochote halali na kukiuza, ili mradi tu natakiwa kufuata taratibu zilizowekwa," alisisitiza.

Akizungumzia kuhusu mgogoro wa kiwanja namba 965, Meya Londa ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kawe, alikanusha vikali kuhusika na uuzwaji wa kiwanja hicho, ambacho alisema kuwa kilikuwa ni mali ya Kiwanda cha Tanganyika Packers, na kilipimwa mwaka 1996.

"Kiwanja hicho kimeanza kuwa na mgogoro tangu miaka ya 1990, ambapo kuwa wakati ambapo Mkuu wa Wilaya alikuwa ni Hawa Ngulume alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kiislamu kuwa wameamua kuvamia na kujenga msikiti kwenye kiwanja hicho.

"Kwa sababu tayari kuna makanisa matatu yamejengwa katika eneo hilo, lakini hakuna hata msikiti, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliamua kusimamisha ujenzi wa msikiti huo ambao ulikuwa kwenye linta, na kuamuru wavamizi hao wafuate taratibu za kuomba kiwanja hicho," alisema.

Alisema, hivi sasa kiwanja hicho kinamilikiwa kihalali na Waislam hao baada ya kufuata maelekezo yote waliyopewa, ili kuweza kupata kibali cha kumiliki, ambapo walichagua taasisi yao ya Qiblatain, ili kuweza kuwasaidia kupaendeleza mahali hapo kwa kujenga msikiti, madrasa na shule ya awali.

Meya Londa alipoulizwa iwapo yupo tayari kujiuzulu kutokana na tuhuma hizo, alisema hawezi kujiuzulu kwa mambo ambayo hayana ushaidi, hivyo alitaka mtu yeyote ambaye ana ushahidi wa kweli kuhusiana na tuhuma hizo ajitokeze, na kuziwasilisha kunakohusika.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Meya Londa aliwapatia Sh 40,000 kila mmoja, ili kuwawezesha kurejea salama kwenye vyumba vya habari.
 
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Meya Londa aliwapatia Sh 40,000 kila mmoja, ili kuwawezesha kurejea salama kwenye vyumba vya habari.

Hii ni rushwa katika herufi kubwa ili kuwafumba macho waandishi wa habari.
 
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Meya Londa aliwapatia Sh 40,000 kila mmoja, ili kuwawezesha kurejea salama kwenye vyumba vya habari.

TAKRIMA ... ili waende ku-copy na ku-paste kile alichokisema bila ya kujiuliza maswali mengi. Ukiwaruhusu waandishi watafakari uliyoyasema unaweza kujikuta unaingia matatani ama ukawachochea ili wasake more details ili ku-verify zaidi news ulizowapatia na hivyo press conference yako ikawa haina maana.

Kilichoniacha hoi ni namna ambavyo Meya anaruhusiwa hata kuteua mwanae kuungana na madiwani vijana kwenda safari ya nje ya nchi. Hivi hizo trip ni zawadi ama ni za nini? Kwa mwendo huu sijui kama ufisadi utaisha!
 
Baada ya kupitia makala husika, hakuna cha maana alichokiongea Meya Londa zaidi ya kuthibitisha yale aliyotuhumiwa kuyafanya
 
Mbona hamuuzunguzii ile posho ya 105,000 BoT mfanyakazi hulipwa tena mda wa kazi?

Posho 40,000 kila mwandishi- heri hata nao waandishi wapewe chao maana mambo yaeshaharibika!

Chukueni pesa- ila andikeni mambo ya kweli!

Nililiona Bongo- kama ukuwaita usipowapa pesa -habari yako hawaipi kipaumbele!- au hawaji siku ingine!

Hii haipo ktk vyombo vya habari tu- angalia Wabunge, na wakuu wote wa serikali- ni lazima uwaandalie bahasha nene!

Hii ni kama vile imeshazoeleka- na inaonekana kawaida!

Serikali naona inakaa kimya!
 
TAKRIMA ... Kilichoniacha hoi ni namna ambavyo Meya anaruhusiwa hata kuteua mwanae kuungana na madiwani vijana kwenda safari ya nje ya nchi. Hivi hizo trip ni zawadi ama ni za nini? Kwa mwendo huu sijui kama ufisadi utaisha!

...i was surprised too,lakini unajua he may be right(legally) lakini to me this is morally wrong,lakini kwa sababu ni fisadi hakuliona hilo na anaamini yuko right bila kuangalia upande mwingine na watu kama hawa hawafai kwa sababu hawaoni ubaya au aibu kutumia loopholes kujinufaisha ambazo walitakiwa wazizibe na kibaya zaidi ni hiyo 40,000 ambayo anataka tuamini ameitoa bila motive,kazi ipo!
 
Sasa kesha kubali uozo wote na hakupata kuhojiwa maswali ya kitaalam soi anapeta ila ananjua kwamba JF iko macho watatafuta info zaidi ili kuwasaidia waandishi wa habari . Nimepata habari kwamba Londa alipelekewa habari kwamba ule Mtandao ambao haulali wala kumuogopa mtu una habari zako ndipo akaitisha mkutano na waandishi .Hongereeni JF . Nimesha ingia Dar natokea Dodoma na Kesho naelekea Kenya kwa siku moja kujua ODM nao wamefikia wapi .
 
na amehalalisha kumpendelea Mtoto wake, kisa sheria inamruhusu.
Na Waziri wa Serekali za Mitaa hati neno, wala Waziri Mkuu, Wala Prezida na Tume ya Maadili na Taasisi zingine kama PCCB etc etc
 
Sasa kesha kubali uozo wote na hakupata kuhojiwa maswali ya kitaalam soi anapeta ila ananjua kwamba JF iko macho watatafuta info zaidi ili kuwasaidia waandishi wa habari . Nimepata habari kwamba Londa alipelekewa habari kwamba ule Mtandao ambao haulali wala kumuogopa mtu una habari zako ndipo akaitisha mkutano na waandishi .Hongereeni JF . Nimesha ingia Dar natokea Dodoma na Kesho naelekea Kenya kwa siku moja kujua ODM nao wamefikia wapi .

Acha zako hizo wewe mzee wa mafix....
 
Back
Top Bottom