Meya Londa kufikishwa polisi

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234

Meya Londa kufikishwa polisi

Na Beatrice Shayo

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa atahojiwa Jumanne ijayo na Kamati Maalum iliyoundwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi, kufuatia sakata la uuzaji wa maeneo ya wazi kinyemela katika manispaa hiyo.

Kiongozi mwingine atakayehojiwa na Kamati hiyo ni Naibu Meya, Ibrahim Kizoki ambaye atahojiwa Jumatatu (kesho).

Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka vyanzo vyetu vya habari zilieleza kwamba baada ya mahojiano hayo viongozi hao watatakiwa kufikishwa katika kituo cha polisi hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja ni kituo gani.
Kamati hiyo pia imeshawahoji madiwani watano jana. Hata hivyo, majina yao hayakuweza kupatikana mara moja.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Naibu Meya Kizoki, alithibitisha kuitwa katika mahojiano hayo.

Gazeti hili lilimtafuta Londa kwa njia ya simu mara kadhaa lakini iliita bila kupokelewa.

Akizungumza na gazeri hili jana, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alikiri kuwepo kwa taarifa za kuhojiwa kwa viongozi hao.

"Kweli najua hawa watu watahojiwa lakini sifahamu hapa kwangu wataletwa saa ngapi," alisema.

Mwanzoni mwa wiki, Lukuvi alifanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za idara ya ardhi na kubaini uuzaji holela wa maeneo ya wazi na kuamuru jeshi la polisi kumtia mbaroni Magesa Magesa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Ardhi wilayani Kinondoni, baada ya kubainika kuwa ndiye mhusika mkuu wa sakata hilo.

Kufuatia sakata hilo, Lukuvi aliamua kuzifunga ofisi nyingine za kitengo cha ardhi zilizopo katika Wilaya ya Ilala na Temeke ambapo alibaini kuna ubadhirifu mkubwa unaofanywa kinyume na sheria ambapo kutokana na uamuzi huo wananchi watakosa huduma kwa muda wa wiki moja na nusu.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa watuhumiwa wote wakimaliza kuhojiwa watafikishwa katika mahakama ya Kisutu kujibu tuhuma zinazowakabili.

Chganzo: NIPASHE
 
Magesa ameshtakiwa kwa kosa gani na Londa anahojiwa kwa tuhuma zipi? Mwenye data atujuze?
 
Kama nakumbuka vizuri moja ya makosa anayoshitakiwa nayo Magesa ni kugushi muhtasari wa vikao vya ardhi vilivyotoa ruhusa ya kuuzwa maeneo hayo na pia kugushi saini ya mkurungezi wa ardhi wa wilaya kinondoni, nadhani Londa na wenzie watashitakiwa kama their ally!
 
Back
Top Bottom