Meya Jiji la Mwanza Mbaroni kwa mauaji ya Katibu wa CCM

Bihondo amekaa muda gani kwenye Udiwani na Umeya wa Jiji lile? Kwa nini KATIBA yetu imempa Rais wetu vipindi viwili vya miaka mitanomitano imeacha UDIWANI na UBUNGE watu waogelee wanavyotaka? Matokeo na madhara yake ndio kama haya. Mtu mwingine anayeelekea kufanana na Bihondo atakuwa huyu Londa wa Kinondoni. Time will tell. Subirini tu.
 
According to the dataz kuhusu tukio hili

1.Yule kijana ambaye amemuua huyu mama alilipwa malipo ya awali laki tano kwa ajili ya kazi hii

2.Kuna zaidi ya Bihondo katika suala hili,na polisi wanaendelea kwa uchunguzi zaidi

Naomba vyombo vya dola vilifuatilie suala hili na wahakikishe huyu jama anachukuliwa hatua kali za kisheri..

NN ,this guy look like a bandit..

Unajua hii habari haiingii akilini vema! kwanza namna mauaji yalivyopangwa...yaani upange kumuua mtu ofisini kwake halafu ukimbie kwa mguu kuelekea ziwani kama ni kweli huyu meya kahusika basi lazima MZA wana meya kilaza!
lakini kwa rafu za wenzetu hawa inawezekana hajahusika ila tu wagombea wameamua kumuunganisha ili kumtia kwenye track...mpaka ijulikane si yeye tayari ni zaidi ya october! Kingine pia mie siamini kabisa kama ni ishu ya ububge tu ndio chanzo kwa sababu MZA ina kata ngapi? influence ya huyu mama ilikuwa kubwa kiasi gani kiasi cha kugharimu uhai wake? hapa kuna hadbari tusioijua na kwa TZ ilivyo inawezekana kamwe tusiijue
 
Mimi ndiyo maana nikauliza kuhusu hicho kibano alichopewa mtuhumiwa? Kweli alikosa pengine pa kumuulia mpaka amfuate ofisini mchana kweupe? Na alipoingia akaanza kupandishana nae ndiyo amchome kisu? Mtu wa kutumwa si angefanya kazi yake bila kupandishana? Au wanataka kutuambia kuwa huyu bwana ni zezeta? Usijekuta wakati wa kibano alikuwa akiulizwa " si ulitumwa na fulani?"! Hapana, hP kuna kitu kisicho sawa.

Amandla..........
 
Nashukuru mkuu kwa kunielewa hapa kuna kitu zaidi ya tunachosimuliwa na kuhadithiwa! Hofu yangu ni ukweli kutojulikana maana ndio siha na haiba yetu
 
Meya keshapandishwa kizimbani leo hii pamoja na wenzake na kusomewa shtaka la mauaji na hivi sasa yuko gereza la Butimba. Linalowashangaza wengi ni speed ya Polisi katika kushughulikia swala hili tofauti na kesi zingine. Hasa katika suala la mtu kutajwa tuu (kama kweli alitajwa) na kuunganishwa katika mashtaka.
Mivutano katika kuwania jimbo la Nyamagana inafahamika, na wakazi wa Mwanza wanaelewa Marehemu alikuwa katika kambi ipi, nguvu za Meya kisiasa nazo zinafahamika na alikuwa kambi gani. Stay tuned na mtasikia umafia uliopo ndani ya Chama cha wenyewe.
 
alibanwa vilivyo vipi? Walim-waterboard? Ushahidi wa mtu aliyebanwa vizuri hivyo kweli unaaminika?

Amandla........

meya wa jiji la mwanza amefikishwa mahakami leo saa 8 mchana katika mahakama ya mkoa amesomewa shitaka
 
Wakuu, hii ndiyo CCM ya zama hizi! Chama ambacho kina viongozi ambao wako tayari kutoa roho za wenzao wasio na hatia kwa ajili tu ya kutaka madaraka. Viongozi ambao wako tayari kuua watawezaje kuwa na huruma yoyote na wananchi wanaowaongoza? Tafakari.........
 
Huyo KATIBU wa CCM wa kata aliyeuawa alikuwa ana maslahi gani kwa huyu mtuhumiwa? Mtu kufikia kupanga mipango ya kutoa uhai wa mtu mwingine lazima kuwe na something very big at stake! Wameendelea kufanya haya mambo siku nyingi, sasa wataumbuana vizuri..

Nikijaribu kutafsiri maoni ya Aristotle na jinsi alivyokuwa akitilia wasi wasi demokrasia, alisema, mara nyingi wanaoingia ktk siasa ni watu ambao hawana kazi mbadala na wakisha ingia hawataki kutoka maana hawajui pa kwenda. Wanakosa kazi mbadala kwa sababu ya mapungufu ya ubora wao.

Haya ya Mwanza ni matokeo ya kuifanya SIASA kuwa ni sehemi ya ajira bora kuliko zote. Bahati mbaya wana siasa wetu waliowengi hawana ajira mbadala. Angalia umri wao. Walio vijana na hasa chama tawala, pia nina wasi wasi kama wana uwezo wa kushindana ktk soko la ajira.

Sasa mtu akitaka kukuondoa utachukuwa hatua gani?
 
B in Court 1.JPG
meya wa jiji la mwanza leonard bihondo akitinga mahakamani jana saa 8 mchana mwanza
 
Kumuua MWANAMKE kinyama hivi,kwa alleged contract killing is beyond belief .Haya mambo yapo huko Pakistan,Afghanistan au Somalia
ambapo wanawake ni second citizen.
Kwa Tanzania yetu jamani what can we do.Huu ni mchezo wa CCM utafika wapi?

CONTRACT killing katika Jamhuri ya Wato Wa Tanzania?????????????????Tena unamuua mwanamke?
 
Mstahiki Meya wa JIJI LA MWANZA Leonard Bihondo na diwani wa CCM kata ya Isamilo kwa tiketi ya CCM, amekamatwa na jeshi la polisi jana jioni Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati akitokea Dar es salaam. Kukamatwa kwakwe kunatokana na kudaiwa kuhusika na mauaji ya Katibu wa CCM kata ya Isamilo ambaye aliuawa kwa kuchomwa na kisi ofisini kwake Mei 14 mwaka huu majira ya saa 6:30 mchana kweupe.

xle6gm.jpg

Bihondo akiwa amevali mavazi yake ya umeya.

2nbzhb4.jpg

Katibu wa CCM kata ya Isamilo ambaye ameuawa kwa kuchomwa na kisu ofini kwake.

mzee bihondo yuko wapi siku hizi?
 
Back
Top Bottom