Meya ailaumu polisi kuogopa vigogo wa 'unga'

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Meya ailaumu polisi kuogopa vigogo wa 'unga'


na Moses Ng?wat, Dodoma


POLISI AIBU TUPU

JESHI la Polisi mkoani Dodoma limetupiwa lawama kwa kushindwa kuwakamata vigogo wa kuuza dawa za kulevya, licha ya kufahamika na taarifa zao kufikishwa kwao na raia kupitia taarifa za ulinzi shirikishi.

Lawama hizo zilitolewa juzi mjini hapa na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jaffari Mwanyemba, kwenye ufunguzi wa mafunzo ya elimu rika kwa ajili ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kikundi cha SAADA.

Alisema hali hiyo imefanya vijana wengi kuathiriwa kutokana na utumiaji wa dawa hizo na kufanya idadi ya vibaka kuongezeka kila kukicha mjini hapa.

Alibainisha kuwa wauzaji wa dawa za kulevya wanajulikana, lakini anashindwa kuelewa kwanini hawakamatwi na hata wakikamatwa wanaachiwa kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha utakaoweza kuwatia hatiani.

“Hata mimi nawajua ila sina ushahidi, nashangaa kwanini hawakamatwi, inaonekana polisi wanazidiwa ujanja na hawa watu kwa kuhakikisha hawakutwi na ushahidi wowote,” alisema naibu meya.

Mwanyemba ameliomba Jeshi la Polisi mkoani hapa kupitia ulinzi shirikishi kupeleleza kwa makini, ili kuwabaini na kuwatia hatiani wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

Pia amewataka wana SAADA ambao kabla walikuwa watumiaji wa dawa ya kulevya kushirikiana na polisi kwa kuwapa mbinu zitakazosaidia kukamatwa kwa wauzaji hao.

Kikundi cha SAADA kilichoanzishwa mwaka jana ni mwendelezo wa shughuli kubwa ambayo ilianzishwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa chini ya dhana ya ulinzi shirikishi, kikundi kina wajumbe 40 ambao ni vijana walioathiriwa na dawa za kulevya.
 
Huyu naona hataki kurudi kwenye manispaa tena kwa njia ya uchaguzi.
Subirini muone kama watamrudisha. Kwa nini???................ kwa sababu kagusa maslahi yetu! Hajui sisi ndio tunaopitisha na kupigia kampeni wagombea ili wachaguliwe? Haya atajiju...
 
Back
Top Bottom