Mexico: Gari la kufyatua dawa za kulevya kama kombora lanaswa mpakani

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
1474467761012.jpg


Polisi wamelinasa gari la aina yake linaloshukiwa lilitumika kurusha dawa za kulevya kutoka upande mmoja wa mpakani hadi mwingine, kati ya Arizona na Mexico.

Kutokana na uimarishaji wa msako dhidi ya walanguzi, baadhi yao wanasemekana walivumbua mbinu hiyo ambapo mihadarati huingizwa kwenye chombo kilicho kwenye gari hilo, kisha kurushwa kama kombora angani kisha kutua upande wa pili.

Polisi walisema hii haikuwa mara ya kwanza kunasa gari kama hilo katika mpaka wa Marekani na Amerika kusini.

Katika mwaka wa 2012, ilisemekana walanguzi wa dawa za kulevya walikuwa wakitumia mbinu kama hiyo.

Mashirika ya habari yalisema pakiti za bangi, kokeni na aina nyingine za dawa za kulevya zimewahi kupatikana zikiwa tayari zimetua katika upande wa Amerika kwenye mipaka hiyo

My take: Hakika mwanadamu akiamua jambo lake, ni ngumu sana kumzuia
 
Mbona njia ya hovyo kabisa hiyo? Ni kama hatua ya mwisho kwa mtu aliyekata tamaa!! Hiyo ni sawa na kutumia nguvu baada ya akili kukwama.
 
Back
Top Bottom