method mogella 'fundi'

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
alikuwa kijana mtanashati,mweupe na mrefu wa wastani.
Safari yake ya soka ilianza mwanzoni mwa miaka ya tisini pale chuo cha ufundi arusha technical college.
Alisajiliwa na timu maarufu ya AICC arusha na baadae kuhamia timu ya ndovu ya mjini arusha pia.

Ndovu ambayo ilikuwa ikicheza ligi daraja la kwanza ilimuwezesha kijana huyu kusajiliwa na timu ya simba sc na baada ya misimu kadhaa alichukuliwa na wapinzani wa simba timu ya dar young africans.akiwa yanga alijipatia umaarufu mkubwa kwa uwezo wake uwanjani na alipewa jina la utani ''fundi''

kwa wapenzi wa soka la nje method mogella ungeweza kumfananisha na kiungo kama andre iniesta au xavi wa barcelona fc.

Mara ya mwisho nilikaa na mchezaji huyu kwenye kiosk cha HH nje ya uwanja wa shekh amri abeid,pembeni yake alikuwepo winga machachari aliyehamia yanga kutoka simba.huyu aliitwa thomas kipese aka uncle tom.

Baada ya hapo sikumuona tena method mogella lakini niliendelea kumsikia akiwika kupitia radio tanzania dar es salaam.

Ghafla taarifa za kifo za mwanandinga huyu zilitolewa kwa kusema alifariki huko nchini afrika ya kusini.mazingira ya kifo chake hayakuwekwa wazi mpaka leo hii.

Mwenye historia nzuri ya nguli huyu wa soka tanzania atuwekee kwa faida ya kizazi hiki na kizazi kijacho.

RIP MOGELLA "FUNDI"
 
Alipata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa huko Arabuni, huu ndio ulikuwa mwanzo wa kujijua kama juu mgonjwa. Vipimo vya awali kabla ya kuanza kucheza soka huko vilionyesha hakuwa fiti tena.

Taarifa fupi ilitolewa kama anasumbuliwa na macho. Tatizo hili alidumu nalo hadi mwisho wa uhai wake.
 
Mogela, alikuwa na uwezo wa kucheza namba zote isipokuwa kipa, l used to love him, nilisikitika sana niliposikia kafa kwa goma
 
Alipata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa huko Arabuni, huu ndio ulikuwa mwanzo wa kujijua kama juu mgonjwa. Vipimo vya awali kabla ya kuanza kucheza soka huko vilionyesha hakuwa fiti tena.

Taarifa fupi ilitolewa kama anasumbuliwa na macho. Tatizo hili alidumu nalo hadi mwisho wa uhai wake.
namkumbuka kwaupenzi wake wa chapati na mchuzi wa nyama.mara ya mwisho niliingia nae uwanjani na .ile basi la yanga.alikuwa kijana mwenye hekima sana.
 
Mogela, alikuwa na uwezo wa kucheza namba zote isipokuwa kipa, l used to love him, nilisikitika sana niliposikia kafa kwa goma

sinauhakika kama alikufa kwa ngoma nadhani alipata kifo cha ghafla,siamini katika hizi rumours ngoja wanajf waliomjua zaidi watujuze.
 
namkumbuka kwaupenzi wake wa chapati na mchuzi wa nyama.mara ya mwisho niliingia nae uwanjani na .ile basi la yanga.alikuwa kijana mwenye hekima sana.
Namkumbuka marehemu, kwa kila alipokuwa anapata nafasi alipita pale TCA kumsalimia rafiki yake wa kike.
 
Daaaa! Ofkoz natoka machozi ,mmenikumbusha mbali ile mbaya
 
Si kweli kwamba alikufa akiwa afrika kusini,Method Mogella alikufia nyumbani kwa baba yake na ilikuwa ni siku chache tu baada ya kurejea kutoka uarabuni.Alienda uarabuni kwa ajili ya kusakata kambumbu lakini alirudishwa kutokana na matatizo ya afya.
 
Method alikuwa mchezaji mzuri hata alipokuwa sekondari pale Mtwara Tech. Wakati huo kalikuwa katoto kadogo lakini ball control yake ilikuwa ya nguvu sana. Mi nimecheza naye umisseta.
 
Si kweli kwamba alikufa akiwa afrika kusini,Method Mogella alikufia nyumbani kwa baba yake na ilikuwa ni siku chache tu baada ya kurejea kutoka uarabuni.Alienda uarabuni kwa ajili ya kusakata kambumbu lakini alirudishwa kutokana na matatizo ya afya.
mkuu kuna utata sana kuhusu kifo chake.
 
Alipata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa huko Arabuni, huu ndio ulikuwa mwanzo wa kujijua kama juu mgonjwa. Vipimo vya awali kabla ya kuanza kucheza soka huko vilionyesha hakuwa fiti tena.

Taarifa fupi ilitolewa kama anasumbuliwa na macho. Tatizo hili alidumu nalo hadi mwisho wa uhai wake.

Huyu jamaa was really fundi and was very fit uwanjani. Sijui aliiga tabia ya super coach maana enzi hizo super coach alikuwa anaifundisha yanga. Yule alikuwa anafundisha kila kitu. RIP Method Mogella. RIP Super coach
 
Mogela, alikuwa na uwezo wa kucheza namba zote isipokuwa kipa, l used to love him, nilisikitika sana niliposikia kafa kwa goma

Super coach alikuwa "fundi" wa mambo mengi sana...RIP. Mogella alipata kufundishwa naye akiwa Yanga ya kina Gulamali(RIP).
 
Nimekaa na Method Mogella pale TCA ingawa tulikuwa tukisoma field tofauti. Tulishuhudia jinsi STAR anavyozaliwa katika dunia ya michezo. Jamaa alianza kubadilika ghafla kwa kila kitu mara baada ya kuchukuliwa kutoka timu fulani ya Namanga na kuanza kuchezea AICC.

Kabla ya hapo, alikuwepo kijana mwingine ambaye na yeye ni Merehemu Salehe Sonda (Mpare mwenye asili ya Kisukuma). Huyu jamaa alikuwa na shabaha sijawahi kuona. Katika mechi zote nilizoona akicheza, sikuwahi kuona mpira wowote aliopiga zaidi ya mita 1 kutoka kwenye nguzo ya goli. Haikujalisha yupo mbali kiasi gani na hii ikiwa na maana magoli yake yote, alifunga yakiwa yameingia si mbali sana kutoka kwenye mlingoti wa goli. Marehemu Sonda kabla hajaja Tech. College Arusha, alikuwa mchezaji wa SIMBA SPORT CLUB enzi Husein Tendwa anakufa.

Marehemu Method Mogella pamoja na kuja kuwa STAR, alibaki kuwa mtu yuleyule tuliyekuwa tunamfahamu. Nakumbuka mara mbili kuonana naye Dar baada ya kuwa amemaliza Chuo. Mara ya kwanza nilimuona Ilala akitokea Kariakoo akielekea Buguruni, na nikasikia mtu ananiita kwenye Bus. Mwanzo sikujali sana nani ananiita ila mwisho niliposikia jina langu ndiyo nikaangalia na kucheck vizuri nikamuona Mogella.

Mara ya pili ilikuwa kwenye jengo la Simba. Alitoka juu na kunikimbilia kuja kunisalimia. Nilishangazwa sana na hii kitu na hasa ukichukulia jamaa alikuwa tayari ni STAR pale Tanzania. Jamaa alikuwa BINADAMU na alibaki kuwa BINADAMU ingawa tayari alishakuwa mtu maarufu sana. Nimekutana na watu wengi sana wakisema "jamaa alikuwa best wangu sana."

Jamaa kwa habari nilisozisikia ni kuwa alienda Uarabuni na huko akarudishwa kwa matatizo ya afya na kutoka hapo ndiyo ukawa mwisho wa STAR wetu Method Mogella. Lazima nikiri kuwa pana wakati nilikuwa Dar na nikaishiwa pesa, nilisikia uchungu sana kumkosa huyu jamaa. Nilikuwa na imani kuwa angelikuwa hai, basi ningelimtafuta walau akanipa nauli ya Daladala.

Wee unayemfahamu nduguye, basi mwambie kuwa ni wengi tutamkumbuka sana Kaka yake Method na lazima wawe PROUD na ndugu yao ingawa ni siku nyingi hatunaye tena.

RIP SALEHE SONDA. RIP METHOD MOGELLA.
 
Ni kweli kifo chake kilikuwa cha utata sana na habari za mwanzomwanzo kabisa za kifo chake zilkuwa jamaa Kajiua, maana baada ya kufail vipimo vya Afya uarabuni, Method alirudi Tanzania akiwa kama alivyoenda (yupo fit) ukimwangalia na alichosema yeye mwenyewe ni Macho ndiyo yalimwangusha, lakini haukupita muda akawa amefariki, ndio hoja za Ngoma na kujiua zilipopata kasi
 
@Sikonge, huyu ndugu yake ambaye ni Rafiki yangu ni Filotey Mogela ambapo ni Method Mogela ndiyo aliongea na Gulamali ili mdogo wake asajiliwe na Yanga, ingawa Filotey naye ana kipaji kikubwa sana lakini hakuweza kupata nafasi ya kutosha kuoneaha kipaji chake maana alisajiliwa ule msimu ambao Yanga walichukuwa ubingwa wa Afrika Mashariki na kati Kampala wakiwa na kina Lunyamila.

Ndipo ikamlazimu Filotey Mogela aondoke Yanga na aende Mlandege Zanzibar akiwa na Wily Mtendamema ambako alin'gara ipasavyo katika ligi ya Zanzibar, na kuna kipindi nilikuwa nikienda Zenj nikimtafuta katika zile nyumba waliyopangiwa na club yale mapokezi unayopewa unajuwa kabisa kwamba jamaa ana heshima kubwa anga zile.
Ila sasa Filotey ameshaacha soka la ushindani ni mtu huwa anatusaidia kufanya mazoezi ya viungo siku za weekend baada ya Joging ya asubuhi.
 
avatar39556_2.gif





Kaka nimeipenda hii avatar yako...ni kama naona watu wazima wanalia.
 
Sikonge, umemwelezea vizuri sana marehemu Method Aniseth Mogella aka Fundi, Kiraka. Jamaa nilikuwa naye JKT Oljoro kwa muda fulani kabla ya kuhamia Ruvu JKT. Hii deal aliifanya Makame Rashid wakati huo akiwa Mkuu wa JKT ili awe karibu na Simba SC. Jamaa alikuwa poa sana yaani ni BINADAMU haswa kama Sikonge alivyosema.Alikuwa ni kipenzi changu kwa jinsi alivyoweza kumudu nafasi mbalimbali uwanjani.Kama wengi walivyoandika, alipata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa Uarabuni yeye na Constantine Kimanda lkn baada ya vipimo akagundulika ana 'matatizo ya afya' hivyo akarudi/akarudishwa nyumbani. Alikuwa anashinda sana kilinge cha Salamander na marehemu Hamis Gaga. Baada ya muda tukasikia akasajili Malindi ya Zanzibar kwa dau la 2M, ambalo lilikuwa kubwa kipindi hicho (1994). Hazikupita siku tunasikia kafariki na ilisemekana alijioverdose baada ya kugundua 'anaumwa'. Maziko yake yalifanyika pale maeneo ya msimbazi centre na ni siku ambayo Taifa Stars ilikuwa inacheza na Sudan kama sikosei....wachezaji walilia sana na hasa Gaga na Kizota walishindwa kujizuia kabisa...RIP Method Mogella
 
Dah RIP Method Mogela "Fundi"..........kama alikufa kwa ngoma basi....hii ngoma ni noma kwa kuchagua......maana chain yake niliyoifahamu vema......toka kipindi hicho!.......ningeshasikia mengi I guess.......
 
Back
Top Bottom