Metakelfin banned in Tanzania

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Taarifa toka TFDA ni kuwa dawa aina ya Metakelfin inayotumiwa na wengi kwa ajili ya matibabu ya Malaria isitumike kuanzia sasa mpaka itakapotolewa taarifa nyingine. Hii ni baada ya kugundua batch kubwa ya dawa hizi nyingi zikiwa bandia (fake).

Kwa yeyote ambaye anazo anashauriwa ASIZITUMIE.

Ni kwa taarifa tu

Habari yenyewe hii chini:

i312_TFDA.JPG

Margareth Ndomondo-Sigonda akitoa maelekezo kwa vyombo vya habari juu ya namna ya kutambua dawa feki.

MAMLAKA ya Chakula na Dawa(TFDA) imeagiza watu wote na wale wanaouza dawa ambao wana dawa ya malaria aina ya Metakelfin kurejesha waliponunua ili kuzipeleka Laborex Tanzania kwa uchunguzi zaidi.

Dawa hizo zimeelezwa kuwa nyingi zilizopo mtaani ni za bandia na hazikidhi viwango vya kemikali inayotakiwa kutibu malaria.

Pamoja na kuagiza dawa hizo kurejeshwa kwa wahusika pia TFDA imepiga marufuku kwa muda uingizaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya dawa ya kutibu Malaria aina ya Metakelfin hapa nchini hadi hapo itakapotangazwa tena.

Dawa hizo inasemekana hazijawahi kuidhinishwa na mamlaka hiyo kuingizwa nchini.

Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Margareth Ndomondo-Sigonda (pichani) alisema katika kipindi hiki wagonjwa hasa wanaotumia dawa za SP ambao ni wajawazito wanashauriwa kutumia zenye viambata vya Sulpadoxine na Pyrimethamine kama inavyoelekezwa katika mwongozo wa kitaifa kuhusu tiba ya malaria.
 
Mimi nina wasiwasi kuhusu hiyo habari ya TFDA. Nchi hii ina ufisadi mkubwa sana kila mahala, kila sector. Inawezekena kuna watu fulani wanataka kupenyeza dawa zao za malaria (au wamesha penyeza) na hivyo kuwahonga TFDA ili watoe tahadhari hiyo kuhusu metakelfin!

Narudia, ufisadi ulivyojikita humu nchini unahatarisha nchi kwelikweli!
 
Maneno yako kweli kabisa lakini ni bora kuchukuwa tahadhari kwanza halafu ufisadi kama upo utadhihirika tu. Nadhani tunao wengi waliopo kwenye fani hii ya madawa nao watatupa maelezo kamilifu na kama kuna mafisadi juu ya hili basi wawekwe bayana.
 
..malaria inazidi kututesa tu, hata hivyo sijui ni dawa gani inafaa sasa. Nilikuwa nameza hiyo metakalfin!
 
Mimi nina wasiwasi kuhusu hiyo habari ya TFDA. Nchi hii ina ufisadi mkubwa sana kila mahala, kila sector. Inawezekena kuna watu fulani wanataka kupenyeza dawa zao za malaria (au wamesha penyeza) na hivyo kuwahonga TFDA ili watoe tahadhari hiyo kuhusu metakelfin!

Narudia, ufisadi ulivyojikita humu nchini unahatarisha nchi kwelikweli!

Nakubalina nawe kabisa mkuu,
Nchi hii haiishi miradi ya wakubwa na inapotokea mikanganyiko kibao hutokea kama huu.
 
Wakuu,

Taarifa toka TFDA ni kuwa dawa aina ya Metakelfin inayotumiwa na wengi kwa ajili ya matibabu ya Malaria isitumike kuanzia sasa mpaka itakapotolewa taarifa nyingine. Hii ni baada ya kugundua batch kubwa ya dawa hizi nyingi zikiwa bandia (fake).

Kwa yeyote ambaye anazo anashauriwa ASIZITUMIE.

Ni kwa taarifa tu

Mkuu mbona metakelfin na dawa nyingine za jamii yake ambazo zinajulikana kama SP zilishafutwa Tanzania toka December 2006? Kuanzia Jan 2007, dawa zinazoruhusiwa kutumika kutibu malaria ni mbili tu. Alu kwa malaria ya isiyo kali (i.e tiba ya awali) na quinine kwa malaria kali au tiba ya rufaa. Kwa hiyo nashangaa kusikia kuwa kuna watu walikuwa wanatumia metakelfin au aina nyingine ya SP. Sitashangaa kwa mambo yalivyo hovyo nchini kwetu kwamba kuna watu ambao bado wanaotumia hata chloroquine iliyofutwa toka 2001.
 
Duu hiii ni hatari. Anyway taarifa nzuri. Lakini hivi kule vijijini kabasa inakuwaje maana hata alternative inakuwa tabu na kama mtu ni mgonjwa basi tena inabidi aendelee kujidunga tu hivyo hivyo. Tatizo jingine bongo uuzaji wa dawa umekuwa wakiholela holela na biashara hii imeonekana kulipa sana ndio maana viduka vipo vingi na vinauza dawa kubwa bila presciption yoyote ilimradi mtu anapesa yake anapewa.

Kushindwa kwa udhibiti ndiko kunakochangia wajasiliamali kutengeneza dawa feki. Kinachotushinda sisi nini mbona huku ugaibuni kununua dawa ni issue sana hata kwenye private chemestry. Huwezi uziwa dawa bila prescription ya Doctor. Pamoja kuwa wanafanya biashara hawakubali kukuuzia dawa bila presciption. Je hawa wameshiba pesa au? Bongo kunanini?

Anyway watu wanaweza tumia dawa za kichina labda haziko feki
 
Mkuu mbona metakelfin na dawa nyingine za jamii yake ambazo zinajulikana kama SP zilishafutwa Tanzania toka December 2006? Kuanzia Jan 2007, dawa zinazoruhusiwa kutumika kutibu malaria ni mbili tu. Alu kwa malaria ya isiyo kali (i.e tiba ya awali) na quinine kwa malaria kali au tiba ya rufaa. Kwa hiyo nashangaa kusikia kuwa kuna watu walikuwa wanatumia metakelfin au aina nyingine ya SP. Sitashangaa kwa mambo yalivyo hovyo nchini kwetu kwamba kuna watu ambao bado wanaotumia hata chloroquine iliyofutwa toka 2001.
Ingawa dawa aina ya SP (kama metakelfin na fansidar) hazitumiki tena kutibu malaria, zimeendelea kutumika kwa ajili ya prophylaxis ya malaria (kinga) mfano kwa akina mama wajawazito. Dawa fake implication yake ni kuendelea kuwa na high rates za malaria in pregnancy- mwishowe kifo kwa mama, mtoto ama matatizo mengine yahusianayo. Asante kutujulisha invisible.
 
"Mimi nina wasiwasi kuhusu hiyo habari ya TFDA. Nchi hii ina ufisadi mkubwa sana kila mahala, kila sector. Inawezekena kuna watu fulani wanataka kupenyeza dawa zao za malaria (au wamesha penyeza) na hivyo kuwahonga TFDA ili watoe tahadhari hiyo kuhusu metakelfin!

Narudia, ufisadi ulivyojikita humu nchini unahatarisha nchi kwelikweli!....."

*****************************************

Zak: Nakubaliana nawe kabisa. Katika Tanzania hii iliyojikita katika ufisadi inakuwa si rahisi kujua ni taarifa zipi zinazotolewa na wakuu wa serikali au taasisi zake ni za kwa masilahi ya taifa na zipi ni kwa masilahi yao binafsi! Tumefika mahala pabaya na pa hatari sana!
 
Maisha yenu yatakuwa magumu sana mkiwa mna-question kila kitu hivyo.
 
Thanks Invisible, but you raise a very partnent issue here.

Thats why I always argue that, nchi zetu za dunia ya tano tuna matatizo makubwa kila sector.

Ukiangalia haya madawa na bidha feki primarily zinatoka INDIA NA CHINA. Sasa hivi Africa tumeshakuwa official damping site ya wachina na wahindi. Hawa jamaa wameshatugeuza kwamba sisi ni dampo lao, lakini kwa vile wanajifanya wako camp moja na sisi linapokuja swala la kuwashambulia westerners tunajifanya tuna solidarity nao. Kifupi, hizi bidhaa feki they dont come in our countries by accident! Hawa wachina na wahindi wanataka kucreate employment za watu wao cheaply and they can only succeed with doing that to Africa.

Hivi jiulize, Leo US au Western Europe wagundue shehena za bidhaa feki (ofcourse at times vinaingia) lakini nakwambia hao wachina na wahindi watahaha! And they cant do it..wanaogopa na wana-stand ku-loose wakifanya huo ujanja ujanja...Leo ukienda mpaka kijijini ni bidhaa feki ya Mchina..kuanzia ndala za Yebo Yebo..mpaka Television!

Yaani sijui waafrika tulilaaniwa na nani, kwa sababu ukweli ni kwamba hata hawa wachina na wahindi wanajifanya ni marafiki zetu kwa sababu wanahitaji resources zetu (after all wazungu walitumia hiyo hiyo tricky), wakishapata chao watatimka watatuacha na umasikini wetu. Sijui tutajifunza lini kugundua kwamba TUNATUMIWA TUU! I can assure you Mchina analijua hili..ndo maana leo anawakumbatia akina Mugabe na BASHIR...(exactly what westerners did). LAKINI kinachouma ni kwamba, Mpaka leo sisi black skinned people hatujapata somo. Kwamba dunia ya leo..usimwamshe aliyelala. China anafurahi tuu..maana anakula na kipofu.

Sasa sijui China wakishatimka..tutaenda wapi..well maybe..Southern America!

At times, Cheap is expensive.

So sad and pathetic!
 
You said it all...
 
Yaani inasikitisha sana, vitu feki vikiingia mpaka kwenye madawa, ni hatari mno.
Kinachosikitisha ni kuwa,hawa TFDA wao ndo walitaarifiwa na raia mwema, sasa sijui kazi zao hasa ni nini?? Yaani isingekua huyo raia mwema kuwapa taarifa, tungeendelea kubugia sumu tu matumboni mwetu.

Oooh God, have mercy on us.
 
Third word particularly Tanzania, We are testing grounds!!!!! Utawala umekubali haya na umaeamua kulea haya!!! Chinese and Indians wameshatuona hovyo. Jamani ni nani asimame atusemee kama si viongozi wetu!!!!! Mzee Mwanakijiji alitoa thread "CCM inaongozwa na nani". Nafurahi wengi wamechangia constructively. Je sasa "Watanzania wanaongozwa na nani" au "Nchi inaongozwa na nani". Kinachotua ni sumu nyingi tunazokula ndani ya madawa na vyakula ambavyo havina ukaguzi wa kutosha, but we have the the called TFDA (Tanzania Food and Drug Authority). Kwanza hawa TFDA waanzie kule Arusha kwenye kile kiwanda kinachotegeneza mafuta wanayoita ni SUNOLA(eti ya Alizeti). Haya ni mafuta ambayo yanatokana na kuchukua mafuta ya maji yaliyo expire (Muzah Oil wanajua wanachokifanya na yule mhindi) halafu yanapelekwa Arusha yanaweka kwenye mitambo halafu mhindi anachukua mashudi ya alizeti anamwaga hayo mafuta juu yake halafu anakamua upya na kaaharufu ka alizeti kanakuwepo then yanarudishwa sokoni. Inaniuma sana. Je tujiulize je serikali siku hizi hawachomeki vijana wake kwenye ajira muhimu za private ili kupata uhalisia wa mambo kama ilivyokuwa zamani? Au wapo ila ufisadi ndo umetawala??? Hayo mambo yamekuwa yakifanyika kwa muda mrefu sana na tunaangamia, kila kukicha magonjwa ya presha na moyo yanaongezeka, cha kushangaza hata kwa watoto wadogo.

Jamani ni wakati umefika sasa tuanze kujali maisha yetu.

Wahindi wote walio na viwanda vya mafuta asilimia kubwa hawatumii mafuta wanayozalisha bali hijitengenezea ya kwao special!!!! Wanahakikisha wamemaliza kizazi cha watanzania na nchi jirani ili waweze kutawala kwa urahisi.

Usalama wa taifa mliomo humu ndani ya forum, mna kazi kubwa sana ya kufanya. Please, ofisi yenu ijipange sawasawa, kuna crimes nyingi sana Tz na nyie mmelala tu. Please, amkeni huo usingizi wa pono.
 
Yule Mama wa TFDA jana kwenye vyombo vya habari,anatuambia hata kwenye duka pekee lililoruhusiwa na wao kuuza hizo dawa,nako wamekuta dawa feki.
Tutaponea wapi kwa mtindo huu??
 
..malaria inazidi kututesa tu, hata hivyo sijui ni dawa gani inafaa sasa. Nilikuwa nameza hiyo metakalfin!

Unameza baada ya kuelekezwa na daktari?
Self medication is harmful!

Taarifa hizi zitangazwe kwenye simu za mikononi kwa njia ya sms ili wananchi wengi wazipate. Hii ni hatari sana.

Duh!
Nilitaraji TDFA tayari wangekuwa wameweka hii ALERT kwenye website yao.
Ingesaidia sana, mfano umesikia habari mtaani ambayo si kamilifu, ukaamua kutizama website yao kwa habari husika kupata uelewa mzuri na hata nyingine zilizowahi kutangazwa.
 
Back
Top Bottom