Messi vs Ronaldo: Nani zaidi?

Inategemea mnatumia vigezo gani katika ku-rank nani ni zaidi ya mwingine lakini ukweli kwa maoni yangu Messi ni zaidi with ball control ya hali ya juu, chengazenye uhakika na confidence anapokuwa na mpira. Ronaldo anakuwa na papala sana kutaka kuanza mbio hata bila ya kuangalia anakimbilia wapi na ndio maana anaishia kukutana na MUNDA za mabeki kama akina Ashley Cole..
 
Kana ka Nsungu,Putin & others GUNNERS you always hate that boy RONALDO
but is the one who win CHAMPS league for UNITED desspite of mising penalt
AT THE MOMENT RONALDO YUKO JUU najua MOYONI unakubali but problem ni ushabiki wako wa ARSENAL
 
Angalia statistics award
CHRISTIANO RONALDO
TEAM HONOURS WITH MAN UNITED
Barclays Premier League: 2006-2007, 2007-2008
Runner Up: 2005-06
FA Cup: 2004
Runners Up: 2005, 2007
Carling Cup: 2006
FA Community Shield: 2007
UEFA Champions League: 2008

HONOURS WITH PORTUGAL
UEFA European Championship 2004: Runner-up
2006 FIFA World Cup: 4th place

INDIVIDUAL HONOURS AND AWARD
Professional Footballers' Association
PFA Players' Player of the Year: 2007, 2008
PFA Young Player of the Year: 2007
PFA Fans' Player of the Year: 2007, 2008
PFA Premier League Team of the Year: 2005-2006, 2006-2007, 2007-2008
PFA Fans' Player of the Month: October 2006, February 2007, November 2007, January 2008

BARCLAYS PREMIER LEAGUE
Barclays Player of the Season: 2006-2007, 2007-2008
Barclays Player of the Month: November 2006, December 2006, January 2008, March 2008
Barclays Golden Boot: 2007–08
Barclays Merit Award: 2008
Football Writers' Association Award: 2007, 2008

MANCHESTER UNITED FC
Sir Matt Busby Player of the Year: 2003-2004, 2006-2007, 2007-2008
Manchester United Players' Player of the Year: 2006-2007, 2007-2008
Manchester United Goal of the Season: 2007-2008

PORTUGAL
Portuguese Sports Personality: 2006
Portuguese Footballer of the Year: 2007

EUROPE
UEFA Team of the Year: 2004, 2007
UEFA Champions League Top Scorer: 2007-08
UEFA European Championship 2004: Team of the Tournament
European Golden Shoe - Soulier d'Or: 2007-2008
European Footballer of the Year - Ballon d'Or:
2nd place: 2007
Onze d'Or
2nd place: 2007
Bravo Award: 2004

WORLD
FIFA World Player of the Year
3rd place: 2007
World Soccer Player of the Year
3rd place: 2007
FIFPro Special Young Player of the Year: 2005, 2006
FIFPro World XI: 2006-2007

LEO MESSI
ARGENTINA NATIONAL TEAM
FIFA U-20 World Cup: 2005
Copa América 2007 second place

WITH FC BARCELONA
La Liga:2004-05, 2005-06
Supercopa de España: 2005, 2006
UEFA Champions League: 2005-2006

PERSONAL HONOURS
Golden Ball: FIFA U-20 World Cup: 2005
Golden Boot: FIFA U-20 World Cup: 2005
Golden Boy: 2005
Bravo Award: 2007[42]
World Soccer Young Player of the Year: 2006[43], 2007[44]
Olimpia de Plata: Argentinian Player of the Year: 2005
FIFPro World Young Player of the Year: 2006
FIFPro World XI: 2007
EFE Trophy: Best Ibero-American Player in La Liga: 2006-2007[45]
Best foreign player in La Liga: 2007[46]
Copa America Best Young Player: 2007[47]
France Football Player of the Year:
3rd place: 2007
World Soccer Footballer of the Year:
2nd place: 2007[48]
FIFA World Player of the Year:
2nd place: 2007[49]
SI Latino's 2007 Sportsman of the Year: 2007[50]

Messi award nyingi kazipata akiwa Junior Player
Hata Barca walivyochukua CHAMPS LEAGUE alicheza game 6 na kufunga goli 1 but Ronaldo kacheza game 11 na kafunga magoli 8 na assist 1 na ndio TOP SCORER
 
Umeweka vizawadi hata vingine havijulikani LOL.

Sikia, hamna mtu anasema Ronaldo sio mchezaji mzuri. Ila kwa Messi hafiki. Jana imedhihirisha nachokwambia.

Essien sio beki namba 2 na ni mfupi. He can get away with it in England kwasababu ma winga wabovu wa timu nyingi. Ila ikija kwenye top 4 teams, huwa anahangaishwa. Ila akikaa midfield ni bonge la mchezaji.

Kuhusu ubitozi wa Ronaldo. Kakosa penalti kwasababu alijifanya mtu wa kuruka majoka hadi uwanjani. Au sijui alikuwa anaruka moto, halafu anasita anajipangusa majivu?

Ashukuru tu JT aliteleza, maana Van de uSaa alikua kasharuka kuelekea amsterdam kuvuta vimsokoto lol!!
 
mtasema mtachoka midomo mali yenu, Ronaldo is waaaaaaaaaay better than Messi, awaambie nani nanyi shoga hamna, jus kidding, its not even right to compare players, at the end of the day mafanikio yao kisoka ndiyo yatakuja kuelezea who is better, i lyk Messi, i think he's skilled player, lakini kuna sababu inayofanya jina la ronaldo liwepo vinywani mwa watu msimu huu unaoishia, and that lad has worked for it, amenikuna sana kama alivyowakuna nyie hadi kuanza kumlinganisha na maradona, lakini CR atajichukulia nafasi yake katika historia ya futbol hasa pale atakapotangazwa mchezaji bora wa Ulaya, na Maradona atabakia kuwa Maradona na same goes for Messi.
 
Umeweka vizawadi hata vingine havijulikani LOL.

Sikia, hamna mtu anasema Ronaldo sio mchezaji mzuri. Ila kwa Messi hafiki. Jana imedhihirisha nachokwambia.

Essien sio beki namba 2 na ni mfupi. He can get away with it in England kwasababu ma winga wabovu wa timu nyingi. Ila ikija kwenye top 4 teams, huwa anahangaishwa. Ila akikaa midfield ni bonge la mchezaji.

Kuhusu ubitozi wa Ronaldo. Kakosa penalti kwasababu alijifanya mtu wa kuruka majoka hadi uwanjani. Au sijui alikuwa anaruka moto, halafu anasita anajipangusa majivu?

Ashukuru tu JT aliteleza, maana Van de uSaa alikua kasharuka kuelekea amsterdam kuvuta vimsokoto lol!!

Enh ndio hafiki... Si tumeona kama Messi kawa "Best Player of the World"??

Hahahahahaha unachekesha kweli wewe!!!!!!!!!!!
 
How old is Messi and How old is Ronaldo? And yet the stats in goals are in Messi's favour.

Messi kacheza misimu mingapi seniors? Na Ronaldo?

in 102 matches
Messi 70 goals
Ronaldo 39 goals

So kafanya kweli kabla ya Ronaldo. Kashinda CL kabla ya Ronaldo.

With Argentina National Team:
• FIFA U-20 World Cup: 2005
• Copa América 2007 second place

Wakati Ronaldo bado anawaza Premiership, dogo alishashinda. Wakati Ronaldo anawaza CL, dogo alishashinda.
With FC Barcelona:
• La Liga: 2004-05, 2005-06
• Supercopa de España: 2005, 2006
• UEFA Champions League: 2005-2006

FIFA world Player kampita Ronaldo mwaka jana.
Personal Honours:
• Golden Ball: FIFA U-20 World Cup: 2005
• Golden Boot: FIFA U-20 World Cup: 2005
• Golden Boy: 2005
• Bravo Award: 2007
• World Soccer Young Player of the Year: 2006, 2007
• Olimpia de Plata: Argentinian Player of the Year: 2005
• FIFPro World Young Player of the Year: 2006
• FIFPro World XI: 2007
• EFE Trophy: Best Ibero-American Player in La Liga: 2006-2007
• Best foreign player in La Liga: 2007
• Copa America Best Young Player: 2007
• France Football Player of the Year:
o 3rd place: 2007
• World Soccer Footballer of the Year:
o 2nd place: 2007

• FIFA World Player of the Year:
o 2nd place: 2007

• SI Latino's 2007 Sportsman of the Year: 2007

Zawadi zote kashinda yuko Juniors eti? LOL!
 
Comments za makocha wakubwa duniani kama kocha wa Madrid na AC Milan na wengine wengi wamekiri kuwa Ronaldo yuko kwenye peak ambayo hakuna mchezaji mwingine amefikia kwa mwaka huu. Kwa hiyo kwa kiswahili kingine ni kwamba Ronaldo is the world's best player of the year. Suala la Messi kusogezwa karibu na Ronaldo ni sawa na kupinga maarifa na ndo maana baada ya vyombo mbalimbali kugundua kuwa Ronaldo anatajwa peke yake kama mchezaji bora wa dunia ndo vikaanza kupendekeza mtu wao kwa ajili ya kuchuana na Ronaldo. Guess what, aliyewekwa hapo kupambana siyo Messi bali ni yule jamaa wa Bayern Munichen ya Ujerumani (nadhani ni Toni) ambaye ni Muitalia.
Ukiachilia mbali hapo, hata Deco mwenyewe anakiri kuwa Messi hayuko kwenye kiwango cha Ronaldo, kwa hiyo ni vema tukajaribu kumuangalia huyo mwingine na si huyu aliyechoka katika umri mdogo (Messi).

Jamaa aliyetaka kumchukua Ronaldo alidai kuwa anajua itakuwa ngumu kwa Fergie kumwachia Ronaldo kwa kuwa anahitaji taji la nyumbani (PL) na la Champions League (CL),na huenda baada ya hapo atakuwa radhi kumwachia.
Kwa hiyo kwa mchakato huo ni kwamba he is a key player inEurope none to compare.
 
Mpo bado mnao-compare Ronaldo na Messi?

Jana kawaonesha ''he is the player from another planet''

One Love One United!!
 
Wakati Barca wanachukua CHAMPS league Messi alicheza game 6 na kufunga goli 1 hakucheza hata final
Ronaldo kacheza game 11 na kafunga magoli 8 na kafunga hadi final

Barca wamechukua Laliga 2004-2005 & 2005-2006 MESI alicheza game chache mno
2004-2005-Alicheza jumla ya mechi 9 msimu mzima na alifunga goli 1 kwenye mashindano yote
2005-2006-Alicheza jumla ya mechi 25 na kufunga goli 8 kwenye mashindano yote

Ubingwa wa BARCA ulichangiwa na ETOO,LARSON,RONALDINHO,DECO,PUYOL,BELETI na sio MESI
Mesi kaanza kucheza game nyingi on the last 2 season ambazo barca hawajabeba kombe hata la mbuzi
Messi hajashinda Bal ondor au Player of the year alikuwa no 2 but RONALDO will
win both award this year

Check hizo link kwa information zaidi halafu utapata jibu
http://en.wikipedia.org/wiki/Lionel_Messi
http://en.wikipedia.org/wiki/Cristiano_Ronaldo
 
Wewe utaoza na wikipedia. Ukute hizo kajaza Ronaldo mwenyewe lol.

'Ave ittttt!!

Messi 20 Cool Goals

Messi is always chopping through a minimum of 3 players!!

'Ave ittt

This is how we do it!! BRAAAAAAAP

Nzoka unakuwa kama muhubiri, maana wahubiri wanachagua ile mistari wanayoipenda wao.

Mpeni Ronaldo sifa zake jamani, hata kama hayupo kwenye timu unayoshangilia. Ina maana Nzoka wewe unaweza kubishana hata na watu wanaolijua soka? Maana wote wanasema Dogo Mzuri akiwamo Beckenbauer, Platt, Coppel kwa uchache. Nakupa Mfano; Real Madrid ina maana hawajaona Uzuri wa Messi kwa unavyotaka wewe mpk waende kwa Ronaldo kwa kutaka kuvunja Bank.

Au ndio unatumia data kwa kupima na Carbon 14?
 
Sijasahau hii thread, nilikuwa nawapa muda mpumue heheee!! Maana niliwaambia msubiri Euro ianze. sasa Portugal wametolewa.

Sasa huyo Ronaldo kafanya nini hapo Euro2008? Kwani anafikiri anacheza na madefender wachovu kama Tightas's Bramble?

Na kipindi hiki mmeona Ronaldo anataka kukimbia Premiership. Anajua kaweka rekodi kwa bahati, hiyo rekodi hawezi weka tena!! Anataka akimbilie Madrid!!

We kuntankite, Madrid na Barca ni timu ambazo hawaelewani. Kwahiyo kusema wa-attempt kumchukua Messi ni ndoto!! Mchezaji kuhama moja ya hizi timu kwenda nyingine ni lazima mchezaji mwenyewe a-instigate. Ukute hata hujui Eto'o alikuwa Madrid zamani.

On that note, sijui kama unajua South America kuna mashindano ya WC qualification yanaendelea? Usije ukawa unategemea analysis ya waingereza we hujui unapitwa huko ohooo!!
 
Nakumbuka wakati wa Euro 2000, kulikuwa na maswali na malumbano mengi sana kati ya wadau wa soka waliokuwa wanajiuliza Zinedine Zidane na Louis Figo ni nani mkali zaidi. Hawa wachezaji enzi hizo walikuwa katika kiwango cha juu mno. Niliwafanyia wadau uchambuzi yakinifu kuwaelezea hawa wafalme wawili wa enzi hizo na kuonekana dhahiri kuwa nani alikuwa zaidi.

Moja ya kitu ninachokumbuka, vyombo mbalimbali vya kimataifa baada ya ile michuano walikuwa wanacomment kuwa Louis Figo ni mchezaji bora kabisa katika Euro 2000, ILA UKIMUWEKA ZIDANE PEMBENI. Maana yake ilikuwa ni kwamba, wakati Figo ndio alikuwa The world best footballer, Zidane alikuwa katika level nyingine baada ya ubest, sasa kwa kiingereza hakuna neno linalomchambua mtu aliye zaid ya best. Maana kuna good, better na best. Labda extremely best !!! Ilikuwa kila Zizzou alipokuwa anacheza, commentators walikuwa wanatafuta maneno ya kumfit km, wonderful, classic, excellent, extraordinaly na mengineyo ya mfano huu…

Sasa, nirudi kwenye mada kuu. Wakati dunia nzima saizi ya wapenzi wa kandanda aka soka ikiwa inajiuliza ni nani mkali kati ya Crhistiano Ronaldo na Leonel Messi, mimi nikiwa kama mchambuzi niliyebobea katika soka la kimataifa nakuletea kwa kina uwezo wa hawa mastar wawili wanaoishika dunia ya soka kwa sasa.

Nitafanya outlining ili nieleweke vizuri. Hapa nitaweka point kumi na mbili muhimu za kuwalinganisha halafu mwisho nitaconclude. Nikianza na Christiano Ronaldo,

CR ana sifa zifuatazo,


  1. Physical appearance (urefu 1.86m au 6.1ft) inampa advantage kama mchezaji katika position yoyote.
  2. Anaweza kutumia miguu yote miwili vizuri kabisa, hii inamfanya amudu kucheza nafasi nyingi bila tabu yoyote.
  3. Ana uwezo mkubwa wa kutumia kichwa. Hii inamfanya aweze vizuri kufunga magoli ya kichwa hapa pointi ya kwanza (urefu) pia inamwongezea hii advantage.
  4. Ana uwezo mkubwa wa kupiga faulo. Ikiwa ni pamoja na kuwa ni mpiga penati mzuri achilia mbali penati kadhaa muhimu ambazo ashawahi kukosa.
  5. Ana uwezo mkubwa wa kuipasua ngome ya wapinzani, hii nikiwa namaanisha ni mwepesi wa kupiga chenga na pia ana spidi kali inayomfanya awe tishio kubwa kwa wapinzani
  6. Anauwezo mkubwa sana wa kufunga magoli akitokea upande wowote wa uwanja na kwa mguu wowote. So far ashafunga goli 22 za Laliga katika mechi 19, msimu uliopita alifunga magoli 26 katika Laliga pia 4 za champ ligi. Mpaka sasa Ronaldo ashafunga magoli 65 katika mechi 64 akiwa Madrid.
  7. Ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa pembeni, pia anauwezo mkubwa wa kucheza km mshambuliaji wa kati. Pia CR anaweza akacheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho. Hii inamfanya awe flexible sana na formation nyingi za kiuchezaji.
  8. Ni mzuri sana wa kupiga pasi za mwisho. Kwenye statistics so far kwenye Laliga ametoa pasi 6 na pia kwenye UCL ametoa pasi 2.
  9. Ni mwepesi wa kuflustrate timu yake inapokuwa down, hii inamfanya asiweze kuwika katika mechi ngumu. Hii inamfanya awe amefunga mara chache sana anapocheza mechi ngumu.
  10. Hajaonyesha kiwango chochote cha ajabu akiwa na timu yake ya taifa.
  11. Pamoja na kuwa anatumia miguu yote, CR si mzuri sana akiwa anashambulia akitokea kushoto.
  12. Hana uwezo kabisa wa kusaidia defence ya timu yake.

Nikija kwa Leonel Messi.


  1. Physical appearance yake (urefu 1.69m au 5.58 ft) haimpi advantage kubwa ya kucheza namba nyingi uwanjani na ndio maana alivyoanza soka na Barca alitumika zaidi kama winga wa kulia.
  2. Anauwezo mkubwa sana wa kutumia mguu wa kushoto, ni mwepesi sana, hii inamfanya kutoonekana udhaifu wake wa kuwa na uwezo mdogo sana wa kutumia mguu wa kulia.
  3. Uwezo wake wa kutumia kichwa ni mdogo kwa sababu ya kimo chake, ila kutokana na wepesi wake mara chache amekuwa akifunga magoli makali sana kwa kichwa, km goli la 2 na Man U fainali ya UCL 2009 aliweza kuruka juu na kuwaacha magiant Vidic na Ferdinand na pia alishafunga goli kwa kuruka juu na kuusindikiza mpira kwa mkono katika mechi na Espanyol, ni goli sawa kabisa na alilofunga Maradona maarufu kama mkono wa mungu.
  4. Si mpigaji wa mara kwa mara wa faulo, ila mara kadhaa amekuwa akifunga kwa faulo. Pia si mpigaji wa penati, imetokea mara chache sana kwa Messi kupiga penati.
  5. Ni extremely dangerous anapokuwa na mpira, anauwezo mkubwa sana wa kupiga chenga, ni mwepesi sana na pia anapokuwa na mpira ni vigumu sana kwa mabeki kujua anachotaka kukifanya, kama kutoa pasi, kupiga shuti au kupiga chenga. Hii inafanya awe hatari mno hata anapobaki na mabeki hata kama ni wawili au watatu.
  6. Ana uwezo mkubwa sana wa kufunga akitokea upande wowote wa uwanja, ila kwa kutumia mguu wa kushoto. Ana goli 18 za Laliga katika mechi 19, msimu ulioisha alifunga magoli 34 katika mechi 34 za LaLiga, alifunga magoli 48 katika michuano yote na Barca na pia ameshafunga magoli 6 ya UCL ktk mechi 6 msimu huu.
  7. Japokuwa Messi anatumia sana mguu wa kushoto, ila anauwezo wa kucheza namba zote za mbele. Anauwezo wa kucheza kama kiungo wa pembeni, ni hatari sana anapokuwa anashambulia tokea kulia, pia anauwezo wa kucheza nyuma ya mshambuliaji, mshambuliaji wa mwisho au kama attacking midfielder. Ni hatari sana anapokuwa anacheza kama kiungo wa kushambulia, nyuma ya mchambuliaji mmoja au wawili.
  8. Ni mpiga pasi za mwisho bora kabisa katika ulimwengu wa sasa. So far ana pasi za mwisho 13 katika Laliga.
  9. Messi yupo humble, ni mchezaji aliyetulia asiye na makeke, na hata timu yake inapozidiwa si rahisi kumuona ameflustrate.
  10. Messi pia bado hajaonyesha uwezo mkubwa kwenye timu ya taifa.
  11. Japokuwa hatumii kabisa mguu wa kulia, Messi ni hatari sana anaposhambulia kutokea kulia. Hii imefanya udhaifu wake wa kutotumia mguu wa kulia usionekane.
  12. Si mzuri kabisa kwenye kusaidia defence.

Kwa kufuatilia hizo pointi 12, naamini utakuwa umeweza kupata picha halisi ya hawa wanasoka wawili wanaowika sasa katika medani ya soka. Katika maeneo mengi uwezo wao unaelekeana, na kama ni kuzidiana ni katika kiwango kidogo.

Pamoja na hayo, Messi ni bora zaidi kwa sababu anaskills ya hali ya juu sana ukilinganisha Ronaldo. Kwakiwango kikubwa, Ronaldo kasi yake ndiyo humfanya awe hatari anapokuwa na mpira, lakini Messi skills yake ndiyo inayomfanya awe hatari sana, maana anapokuwa na mpira huwezi jua anataka kufanya nini, na ndio maana ukiangalia katika upigaji wa pasi za mwisho Messi anatisha mno. Kuna vigezo vingine vingi tu vinavyowahusu, ila kwa kuwa maelezo yanakuwa marefu nimeamua kuishia hapo maana hili si gazeti.
 
nausifu uchambuzi wako kwa sababu sio wa kishabiki na ni wa kitaalamu, umesema kweli messi ni bora, wataalamu wa mpira wanasema
kama angeweza/akiweza kuisaidia timu yake ya taifa kuchukua kombe la dunia atakua level ya akina pele na maradona.
 
siri kubwa ni chimbuko la La Masia pale,hata ukimpeleka Mzee Makalanja pale atawika tu,angalia kina Arteta,Fabregas,Pique,Puyol,Reina,Valdes,Guardiola,Busquets,Iniesta,Xavi,Rodriguez,Carles Busquets nk wengi tu.
 
Nakubaliana sana na wewe lakini pia unapaswa uzingatie impact ya ubora wa timu kwenye kuwika kwa mchezaji, ni vigumu sana kumuona Ronaldo yupo juu ya Mess wakati timu yake naye akiwemo ilipigwa kama imesimama walipokutana na Barcelona.

Real Madrid bado haijafika kwenye level ya ubora wa Barca na hivyo kumbania Ronaldo kupambanishwa kwa haki na Mess, hauwezi kumuona mchezaji amecheza vizuri kama team yake haijacheza vizuri, lakini tumeziona juhudi nyingi binafsi alizozifanya Ronaldo katika msimu huu na kuisaidia sana Madrid kuwa hapa ilipo, may be nayaona haya kwa sababu namkubali sana Ronaldo.
 
Nidhamu. sifa moja wapo anayotakiwa kuw anayo mchezaji bora .

Kama ulivyosema huko juu hata kabla ya viwango vywa uchezaji nidhamu tu uwanjani inampa Messi Ushindi.

Kuhusu chenga sijui kama Ronaldo ni mpiga chenga zaidi ya Messi. Ronalndo ana kasi ya kukimbia na mpira. na kushtua shtua shtua tu.

Man to man kati ya beki na mshambuliji Messi ni mbunifu wa kuwachomoka au kulamba chenga hata mabeki wawili au watatu lakini sio Ronalndo.

Yes kweli Ronaldo ana mashuti na uwezo wa miguu yote kama kama ulivyosema but Messi ni talent ya hali ya juu.


nakubaliana na uchambuzi huu
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom