Kwa style hii hawa ndugu zetu wanaweza wakawa ni janga la dunia
Mkuu Pasco, idadi ya watu ikiongezeka na makabila yao nayo yanaongezeka?Mkuu Petrol, zoezi la sensa ni la lazima sio option kama uchaguzi, its a must hakuna room ya kusema anayetaka!.
Mimi nawaunga mkono ndugu zetu Waislamu ili kikiongezwa hicho kipengele cha dini na cha kabila tutakipenyeshea hapo hapo angalau tujue wale Wahdzabe waliokuwa 250 sasa wamebaki wangapi. Miaka ya 80 iliwachukua kinguvu watoto wao 4 na kuwasomesha boarding mpaka la 7 hakuna aliyefaulu, lakini wote wanne wakapelekwa Pugu na kusomeshwa mpaka form four, wote walipata Div. 0!. Wakarudishwa kwao msituni ili kupeleka civilization kwa ndugu zao ikiwa ni pamoja kuwajengea nyumba za kisasa na kupewa nguo na vifaa vya kisasa!. Baada ya mwezi mmoja serikali ilirudi kuwatrace ilikuta vile vitu vyote walivyowapa viko pale pale walipoviacha na yale makazi yakiwa kama yalivyo na more surprising hata zile nguo za wale wasomi 4 nazo walizivua na kuziacha!.
Hivi tutaendelea kuwategemea wazungu mpaka lini?. Wazungu watuhesabie tembo wetu, Mama Jane Goodhall atuhesabie sokwe wetu!, sasa hata makabila yetu nayo ndio tusuburi wazungu watuhesabie?!.
Tulipopata uhuru tulikuwa na makabila milioni 12 na makabila 120, kwa wastani wa watu laki moja kila kabila, sasa tunaenda milioni 50 kwanini tusijue na makabila!.
Mfano wangejua kabila linaloongoza kwa procreation ni kabila gani ili elimu ya uzazi wa mpango iwe concetrated huko na makabila gani yana hatari ya kufutika ili yaingizwe kwenye 'endagered species' ili kuyalinda!.
Wangapi kati yenu mnajua Watindiga wamebaki wangapi?, Wahadzabe, Wasandawi, Wataturu Wabalungi, Wakonongo etc. etc.
Kuna ubaya gani kujua tunawapagani wangapi, Hindu, Budha, Bahai, Baniani, Waislamu wa Ahamadiya, Waislamu wa Shia, Waislamu wa Sunni, Waislamu wa Ismailia, Waislamu Makadiani etc?. Kuna ubaya gani?.
Kama rais wa kwanza wa Tanzania alikuwa Mkatoliki, Mkapa nae ni Mkatoliki, Membe, Dr. Slaa na Magufuli nao ni Wakatoliki wanaosubiria kupangishwa pale nyumba nyeupe!, kuna ubaya gani tukiwajua wako wangapi, na Anglicana wangapi, Walutheri, Waadvetisti Wasabato, Memonite, Walokoke etc. etc. Hivi kuna ubaya gani?.
Acha kupotoka kama sio kupotoshwa .Idadi ya watu huendana sambamba na eneo ya mraba wanapoishi hivyo si kweli kwamba kujua waisilamu/wakristo wakijulikana ni wangapi eneo fulani itasaidia kujua ukubwa wa msikiti/kanisa.mfano eneo ya 100000 m[SUP]2 [/SUP]linatarajiwa liwe na watu 100 na kuwepo na huduma za jamii zinazoendana na idadi ya watu hao.Kaka kama sentensi yako ilivyoanza basi nawe umeteleza. Ustawi wa jamii unahitaji kujua idadi ya watu kwa mujibu wa itikadi zao otherwise wanavyopima viwanja wasingepima maeneo ya kufanyia ibada. haiingii akilini wewe kama mtaalam upime eneo la kuweka kanisa mfano AGP uweke sehemu ya kuabudu wafuasi wa AGP 30 nawakati wao wenyewe wako 400. jamani mbona elimu zetu mbona hazitubadilishi? tatizo ni nini
Kwani Chadema wamekubali matokeo ya Tume ya Uchaguzi?
Yaani wewe ni mweupe kichwani sijapata kuona, si kila lisemwalo na waislam basi wewe upinge hata kama huna hoja.
soma hii sensa ya india iliyoweka na dini, soma matokeo yake kisha nambie je, hauhitaji kufanya intervention kwa baadhi ya maeneo, kielimu, kiafya, kiuchumi ili kuwainua wananchi wa taifa kiujumla?
http://censusindia.gov.in/Ad_Campaign/drop_in_articles/04-Distribution_by_Religion.pdf
jibu swali langu kwanza,hapo hakuna cdmKwani Chadema wamekubali matokeo ya Tume ya Uchaguzi?
Kaka msg umeisoma ukiwa na mtizamo hasi, na hili ni tatizo siyo kwako tu bali hata kwa wenzako wengi. Msg haichochei kitu isipokuwa ni taarifa ya kiimani inayowahusu waislam, wewe kama siyo muislam hiyo msg haikuhusu na wewe jipange kuendelea na sensa. madai ya waislam ni ya kimsingi na hakuna hoja ya kuyafanya yaonekane kama hivyo unavyodhani. acha msg serikali imesha pewa taarifa ya kimaandishi kuwa kama sensa haitoweka vipengele muhimu basi mhesabiane nyinyi wenyewe wengi wakristo. Ni aibu kubwa sana kwenu kwani mitandao yenu mnajitangaza mko wengi sasa mwahofia nini kwa kipengere cha dini kuwekwa? Mrudieni Mungu, otherwise mtapotea.
Kaka msg umeisoma ukiwa na mtizamo hasi, na hili ni tatizo siyo kwako tu bali hata kwa wenzako wengi. Msg haichochei kitu isipokuwa ni taarifa ya kiimani inayowahusu waislam, wewe kama siyo muislam hiyo msg haikuhusu na wewe jipange kuendelea na sensa. madai ya waislam ni ya kimsingi na hakuna hoja ya kuyafanya yaonekane kama hivyo unavyodhani. acha msg serikali imesha pewa taarifa ya kimaandishi kuwa kama sensa haitoweka vipengele muhimu basi mhesabiane nyinyi wenyewe wengi wakristo. Ni aibu kubwa sana kwenu kwani mitandao yenu mnajitangaza mko wengi sasa mwahofia nini kwa kipengere cha dini kuwekwa? Mrudieni Mungu, otherwise mtapotea.
[/COLOR]Mkuu Pasco hapo umeteleza ,kila jambo linafanyika kwa malengo. Jambo lolote ambalo linagharimu rasilimali kubwa (fedha na rasilimali watu) kwenye utekelezaji wake lazima malengo yake yaanishwe kwa ufasaha wa hali ya juu sana.Sensa inayofanyika inamalengo yake ,studi kwa maana ya utafiti ishafanywa na kufanya majaribio mbalimbali ya variables wanazotaka kuzitumia ili wapate majibu sahihi.Hizo takwimu za variables nyingine kama dini,kabila wameona hazitakuwa na mantiki kwa malengo ya takwimu za kimaendeleo/usatawi ya wa jamii.
Huwezi ukawa unataka majibu ya jinsi gani ya kuboresha huduma za afya ama kuongeza idadi ya shule kwa kujua waisilamu/wakristo wapo wangapi ama wapare wapo wangapi kulinganisha na wanyakyusa,huu ni ufinyu wa mawazo.Wao wameona kujua umri,jinsia ,wasiojiweza zina mantiki zaidi kiutafiti.Sensa inafanyika wakishatoa takwimu -mfano watanzania tupo milioni 60,hao wanaotaka kujua kuwa waisilamu/wakristo wapo asilimia ngapi mbona ni rahisi.Makanisa na misikiti wanautaratibu wao wa kuainisha majina ya waumini wao wa watafanya mahesabu rahisi.Sisi ambao hatuendi msikitini/kanisani idadi yetu itajulikana kwani kwenye hizo list zao misikitini/makanisani hatutaonekana.Hizo takwimu za kidini ni kwa manufaa ya waumini na wafuasi wa dini hizo.
Huu ushabiki unaofanywa na hawa baadhi ya viongozi wa dini sio wa kufumbia macho hata siku moja.Inamaana na wewe unashabikia maendeleo yaletwe na serikali kwa misingi ya udini na ukabila!!?.Kijiji nilichozaliwa kulikuwa na waisilamu na wakristo -sherehe zikifanyika iwe Idd ama Xmas watoto tulikuwa tunajuika pamoja,wazazi wetu walikuwa hawana shida na hilo.Hata katika shughuli za maendeleo mfano kujenga shule,kuchimba visima,kuchimba barabara nk. shughuli hizo zilikuwa zinafanyika kwa ushirikiano bila kujali huyu ni mwisilamu/mkristu.Siku za ijumaa waisilamu walikuwa haendi kwenye shughuli hizo na vile vile j'pili wakristo hawaendi ,hii ilitokana na misingi ya utaifa iliyokuwepo.
Leo hii wametokea watu wenye uelewa finyi wa maendeleo kwa kuweka maslahi binafsi kwa kupenyeza hizo ajenda zao kwenye taasisi za dini.Mwislamu/Mkristo haitaji kujua waislamu/wakristo wenzake wapo wangapi kwa yeye kupata elimu bora ama huduma bora za afya,anachotaka kukijua ni rasilimali za nchi yake zinamfaidishaje yeye na wanajamii wenzake kwa ujumla. Mama ntilie kilio chake ni kuona anapatiwa mahali safi pasipo na adha anapofanya biashara yake ,haitaji kujua waisilamu/wakristo ni wangapi.Huu ushabiki utatuopeleka pabaya sana,kizazi hiki kinategemewa kuwa ndio kitakacholeta mabadiliko kwenye nchi hii ,sasa kama tunageuka kuwa washabiki wa mambo kama haya napata wasiwasi.Tunatakiwa tuweke nguvu kupambana na adui yetu mkuu anayehujumu rasilimali ya nchi yetu kwa kuungana na sio kujigawa kwa misingi ya ukabila ama udini.