Meseji za mapenzi za wabunge zanaswa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
i
pix.gif
Gazeti lenye alama A kwa habari za uchunguzi, Uwazi, linaweza kuthibitisha heshima hiyo baada ya kubaini barua pepe za kimapenzi 30 za mtu huyo kwenda kwa wabunge ambao baadhi yao wamejibu chanya, wengine wakikataa kuonesha ushirikiano na wachache waliosalia wakiacha kujibu.

Uwazi halijambaini mtu huyo anayewachezea wabunge au lengo lake, lakini lina uthibitisho wa barua pepe alizowatumia wabunge hao, huku akijitambulisha kwa waheshimiwa hao kwamba yeye ni msanii wa filamu na anaitwa Aunt Ezekiel.

Katika kupata mzani wa sakata zima, mwandishi wetu aliongea na Aunt na kumuuliza kama ni yeye ambaye huwatumia barua pepe waheshimiwa, majibu yake yalikuwa ni hapana kwamba hajawahi kufanya hivyo hata siku moja.

Aidha, Aunt alishindwa kuitambua anuani ya waraka pepe wa mtu huyo ambaye hujitambulisha ni yeye ambayo ni auntezekiel12009@yahoo.com na kusisitiza kwamba anayefanya hivyo bila shaka anataka kumchafua ili aonekane mapepe kwa waheshimiwa.

“Siyo mimi, siwezi kufanya hivyo, huyo mtu nadhani anataka kunichafua mimi. Kwanza simjui na hiyo email siyo yangu na sijawahi kufungua email kama hiyo katika maisha yangu,” alisema Aunt na kuongeza:

“Najiheshimu, siwezi kumtumia mheshimiwa email ya kumtongoza. Kwanza nakosa nini mpaka nijiuze kwao? Natamani nimjue mtu huyo na ikiwezekana naiomba serikali inisaidie kumpata ili nimshtaki.”

Katika barua pepe za mtu huyo kwenda kwa waheshimiwa hao, moja ambayo ndiyo ya kwanza, imeandikwa: “Kwa muda mrefu nimekuwa nikitafuta mawasiliano yako lakini sikuweza kuyapata, mpaka nilipofanikiwa kupata email yako. Naitwa Aunt Ezekiel ni msanii wa filamu nchini.

“Mheshimiwa, kwa muda mrefu sana nimekumeil kwa njia ya mtandao. Kifupi nina shida binafsi ya kukutana na wewe, kama sitakuwa nimekukosea naomba nitamke wazi kuwa NAKUPENDA. Kama msichana mkamilifu siwezi kuficha katika hili, naomba unipe nafasi moyoni mwako na uwe tayari kukutana na mimi kwa mazungumzo zaidi.

“Kwa sasa niko nchini Kenya, lakini nataraijia kuwa Dar es Salaam wiki ijayo. Ukitaka namba zangu za simu nitakutumia.

Nakushukuru sana.”
Baada ya barua pepe hiyo, sehemu kubwa ya wabunge waliijibu chanya kwa kutaka kufahamiana zaidi na Aunt Ezekiel huyo feki, wengine wakitoa majawabu ya mkato, huku wachache wakikataa kabisa kutoa majibu.

Moja ya barua za waheshimiwa ilijibu: “Ohoooo, ni huyu Aunt wa magazeti ya udaku au mwingine?”
Baada ya jibu hilo, upande wa pili uliandika: “Ndiyo mimi Aunt unayemjua, si mwingine, ila siyo wa magazeti ya udaku, mimi ni staa wa filamu.”

Mheshimiwa akaendelea kuandika: “Ok, sasa unaniambiaje, unanipenda kweli au unanitania? Kimapenzi au kwa kazi yangu ya siasa?”

Aunt feki akazidi kumwagika: “Nakupenda kwa vyote, kisiasa, muonekano wako. Nikikupata kimapenzi naamini hutojuta.”

Mbunge: Tatizo lenu ninyi warembo mastaa mnapenda sana vijana wa Bongo Fleva, sisi wanasiasa tupo ‘busy’, tutawezana?

Aunt: Nakuweza, halafu mimi sijawahi kuwa na mpenzi wa kibongo fleva, wewe utanifaa ndiyo maana nakutamani siku zote.

Mbunge: Ok, mimi nipo Iringa kwenye vikao vya kamati, nikirudi nitakutafuta, nitumie namba yako ya simu ya mkononi ili nikifika Dar nikupigie tukutane mtoto mzuri.

Wakati mheshimiwa huyo akitoa ushirikiano huo, mwingine anayepatikana zaidi jijini Dar, ingawa jimbo lake lipo mkoa mwingine, alijibu: “Mimi sikufahamu.”

Baada ya kujibiwa hivyo, Aunt feki alizidi kuchokonoa: “Hunijui mimi, mbona nimecheza filamu nyingi tu?”
Mheshimiwa: Nimesema sikujui.

Mbunge mwingine alijibu kwa mkato huku akitilia mashaka barua pepe hiyo na kuandika: “Mmmmm ........ !!!!!!!
Nashukuru kwa upendo wako.!!!!!!!! Hukutumwa ?????????”

Kwa jumla, majibu ya waheshimiwa wengi, ama yalifanana na yale ya mbunge wa kwanza au wa pili, huku wachache wakiacha kujibu lakini majina yao wote yanahifadhiwa kwa sababu maalum.

Kutokana na hali hiyo, Uwazi linawapongeza waheshimiwa wabunge ambao wameonesha msimamo kwa kukataa kumpa ushirikiano mtu huyo kwa sababu iliyo wazi kwamba mhusika hana dhamira njema kwao.

Gazeti hili linatoa muongozo kuwa kama mhusika angekuwa na nia njema, asingeandika ujumbe mmoja kwa waheshimiwa 30, wote akiwataka kimapenzi na kwamba anawapenda sana.

Aidha, gazeti hili linakumbusha kuwa siku za hivi karibuni umeiubuka mtandao unaojulikana kwa jina la HAMAS ambao kazi yake ni kuwalaghai watu maarufu, kuingia nao chumbani kwa mtego wa kufanya mapenzi kisha kuwapiga picha chafu na kuzisambaza kwenye tovuti, blogu, simu na magazeti.

Memba halisi wa mtandao huo hawajajulikana, lakini Uwazi linaonya kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, HAMAS linaweza kuweka kambi kwa wanasiasa, wawachafue na kupoteza sifa zao za kuwa viongozi kwenye jamii.

http://www.globalpublisherstz.com/2008/06/17/kumbukumbu_ya_bongo.html
 
KWANI AUNT EZEKIEL nI LAZIMA AWE HUYU MSANII ANAYEFAHAMIKA NA WENGI? KWANI HAKUNA MTU MWINGINE ANAYEWEZA KUWA NA JINA HILO NA AKAWA PIA MSANII WA FILAMU AMBAYE HAJULIKANI TZ?
 
wabunge wanawaonea wivu wasanii wa bongofleva....

sasa si na wao waimbe basi.
 
Mbunge: “Ohoooo, ni huyu Aunt wa magazeti ya udaku au mwingine?”

Aunt :“Ndiyo mimi Aunt unayemjua, si mwingine, ila siyo wa magazeti ya udaku, mimi ni staa wa filamu.”

Mbunge:“Ok, sasa unaniambiaje, unanipenda kweli au unanitania? Kimapenzi au kwa kazi yangu ya siasa?”

Aunt:“Nakupenda kwa vyote, kisiasa, muonekano wako. Nikikupata kimapenzi naamini hutojuta.”

Mbunge: Tatizo lenu ninyi warembo mastaa mnapenda sana vijana wa Bongo Fleva, sisi wanasiasa tupo ‘busy’, tutawezana?

Aunt: Nakuweza, halafu mimi sijawahi kuwa na mpenzi wa kibongo fleva, wewe utanifaa ndiyo maana nakutamani siku zote.

Mbunge: Ok, mimi nipo Iringa kwenye vikao vya kamati, nikirudi nitakutafuta, nitumie namba yako ya simu ya mkononi ili nikifika Dar nikupigie tukutane mtoto mzuri.

Script imekaa utamu hii!

Haya haraka haraka Geoff nipe Title ya hii muvi; tutaiitaje?

.............................

Producer : Mzizimkavu
Director : Masikini Jeuri & GeoFf
Script: Mwanakijiji
Costumes:
 
Kwa mwanaume rijali ni kawaida awe askofu au mchungaji au mwanasiasa hata mwanaphilosofia kupenda na kufanya mapenzi ni jambo lakawaida haijalisha umeoa au hujaolewa au hujaoa ashki za kimwili zipo
 
Udaku tu! Kwani hao uwazi wanaweza kutuhakikishiaje kua sio wao waliokuwa
Wanaandika emails hizo ili kujitengenezea habari fake
Huyo ndo shigongo mlokole!
 
sasa cha ajabu hapo ni nn wabunge kumtongoza aunt au kwani mbali na ubunge siniwanaume na wana hisia ndomana bunge likianza machangu yanakuwa adimu kweli yote dom
 
Back
Top Bottom