Meseji niliyoikuta kwenye simu ya mke wangu

Mchana huu wa leo mama watoto alinipitia na tukaenda kwenye kiji mgahawa kimoja hapo jirani na jengo la ppf tower.
Pale tukakutana na wafanyakazi wenzangu na hivyo basi mama watoto akawa akibadilishana nao mawazo.
Wakiwa wanaendelea na mazoezi nikawa nimeishika simu ya mama watoto ili nichue namba ya shangazi yangu aliyeko shamba.
Baada ya kuichukua ile namba nikaingia kwenye meseji.
Sina utamaduni wa kukagua simu ya mama watoto, hata yeye analijua hilo lakini leo sijui ni kitu gani kimetuma kufanya hivyo.
Hii ndiyo sms niliyoikuta kwenye simu yake "mi sina la kusema, coz najua hou u make me crazy on bed, roll it babe!"

basi nikajiforwadia kwenye simu yangu, na nikaichukua namba ya huyo mtumaji ambaye anaitwa coleman.
Mpaka naachana na wife sikusema chochote na nikajaribu kuficha machungu yangu ili kati yetu asiwepo wa kujua na kuniuliza ni nini kimetokea.
Sitaki mnielekeze kuwa nimsamehe au nimuadhibu..
Nimeongea hapa ili kutoa donge la hasira na uchungu vilivyonijaa moyoni.

Sikupi pole Mzee kwasababu inawezekana hiyo msg iliingia kwa makosa haikuwa kwa ajili ya Mkeo. Binafsi nilishawahi kutumiwa msg na msichana kwenye simu yangu kwa makosa na ilikuwa ina ujumbe mzito sana kama ingetokea Mke wangu kuiona ingekuwa balaa kenye ndoa yangu mpaka ukoo mzima wangeipata. MSG ilikuwa inasema "JANA UMENIFANYA KOTE HALAFU HELA YENYEWE KUMBE HUNA, USIPONIPA HELA YANGU LEO NAKUJA DAI MBELE YA MKEO".
 
sikupi pole mzee kwasababu inawezekana hiyo msg iliingia kwa makosa haikuwa kwa ajili ya mkeo. Binafsi nilishawahi kutumiwa msg na msichana kwenye simu yangu kwa makosa na ilikuwa ina ujumbe mzito sana kama ingetokea mke wangu kuiona ingekuwa balaa kenye ndoa yangu mpaka ukoo mzima wangeipata. Msg ilikuwa inasema "jana umenifanya kote halafu hela yenyewe kumbe huna, usiponipa hela yangu leo nakuja dai mbele ya mkeo".
jina la mtumaji ni coleman na liko saved kwenye phonebook ya amama watoto
 
Kama hutaki msaada wa mawazo basi tayari umeshapitisha hukumu. Basi tupe hints kuhusu hiyo hukumu. Vinginevyo kutua yaliyo moyoni ni pamoja na kutafuta ushauri + sympathy.

Binafasi nimeguswa sana na pole kwa yaliyo kukuta. Ukiweza kulimaliza hili basi huenda hutakuwa na mtihani mwingine mkubwa maishani. Time and locations are key to healing. Jipe muda na ikiwezekana chukua likizo ukae mahali tofauti ili uweze kulitafakari hili jambo!

Aisee pole ndugu yangu, ndio maana mpaka leo kutokana na matukio kama hayo baadhi ya watu hawataki kabisa kusikia neno kuoa. Inatia uchungu sana ndugu hasa unapotafakari massage hiyo. Lakini kwa upande mwingine tusipende sana kuwekeza kwenye nyumba ndogo 'vidumu', huwa vinachangia kuwa wazito tunapokuwa na wake zetu ama mamet wetu!
 
pole ndugu yangu haya ndo madhara ya maendeleo, usinyamaze mbane vilivyo akueleze, ikibidi tumia tena simu kumjibu huyo coleman ukijifanya ndo mkeo, utajua mengi zaidi, unaweza uliza ni lini nilkumake crazy zaidi?

Only if nawewe hujawahi kumega nje, iwe umeonewa kikweli
 
i dont care kama ametunga ama la... ninachweza kumwambia ni kuwa kama aliandika hapa kutoa hasira its ok... HE can even cry... na la zaidi DISTANCE its a best medicine aende mbali na mazingira yaliyomzoea (namaanisha kuanzia majrani nyumbani, kazini na chochote kile ambacho amezoea kukiona na kukifanya) kwa mda akae huko alerax then akirudi wakae waongeee wakati temper imeshuka ...

+++++++++++++++++
SOMETIMES DISTANCE IS THE BEST MEDICINE....but Know your Direction
kwa maana hiyo, kama akaa Mwenge, ahamie Mbagala spiricho centre kwanza kwa muda??

NO.... fanya utaratibu fasta umkamate huyo jamaa ukiwa na wahuni wanne hivi wapeane zamu tu na picha kibao wapige wakiwa kwenye kilimo mseto. baada ya hapo we rudi home na mamsapu mpeleke dina la maana na ukatekeleze sera kama hakijatokea kitu vile.
 
kwa maana hiyo, kama akaa Mwenge, ahamie Mbagala spiricho centre kwanza kwa muda??

NO.... fanya utaratibu fasta umkamate huyo jamaa ukiwa na wahuni wanne hivi wapeane zamu tu na picha kibao wapige wakiwa kwenye kilimo mseto. baada ya hapo we rudi home na mamsapu mpeleke dina la maana na ukatekeleze sera kama hakijatokea kitu vile.

Hatua kama hizi hazitakusaidia katika maisha yako kwa maana hutaweza kujipima utu wako tena maishani.Mawili - samehe au acha!
 
jina la mtumaji ni coleman na liko saved kwenye phonebook ya amama watoto

Yawezekana kabisa kuwa Coleman ni mtu ambaye yupo kwenye PB ya mkeo, ila chunguza pengine na yeye (Coleman) alikuwa akituma kwa mtu wake ila bahti mbaya ikatelezea kwa mkeo.
Je hiyo sms ndio ilikuwa imeingia au ilikuwa ni ya kitambo?
Kama ni ya muda mrefu ni ya lini haswa?
Ulichotakiwa kufanya ni kutafuta kwe Outbox mkeo alimjibu nini ili upate pahali pa kuanzia.
 
Hii bandiko linaonyesha kuwa siyo wewe uliyepatwa na hilo jambo - Ni story ya kutunga a.k.a kusadikika.

UJUMBE: kwa wale wenye tabia ya kuchonokoa simu za wenzi wao watambue kuwa watakutana na meseji nzuri zaidi ya hiyo!

Mh!!! Naota nadanganywa????
 
Mbona coleman na waife wako wote ni wanajamii na hapa wameshafahamu kila kinachoendelea?

Weka namba ya Mr. Coleman hapa.
 
Hatua kama hizi hazitakusaidia katika maisha yako kwa maana hutaweza kujipima utu wako tena maishani.Mawili - samehe au acha!

WOS.....Mzima lakini, habari za siku?

Ingekuwa rahisi......Kusamehe au kuachana ni best option kama hiyo kitu inamhusu kweli mhusika! ninawasiwasi, ni wachache sana wanaweza fanya hivyo...tuliowengi.....Kisasi + Kuacha!
 
Jamani mlisha ambiwa kuchokonoa chokoa simu za wenzi wenu ni mbaya! Sasa ona hapo ndoa tayari imeshaingia mgogoro!

Kuna mambo ambayo huwa nayasikia kwenye stori zetu za ''vijiweni'' kuhusu wake za watu, kama waume zao wangejua wangejinyonga hadharani!
 
unadhani ni rahisi namna hiyo

Of course the better way is to forgive and forget, kama ataomba msamaha wa kweli kutoka moyoni! Kama hataomba msamaha basi leave and forget! Kinachokichukiza kuliko yote ni kuanza kuanikana kwa ndugu, majirani, marafiki, wazee, etc kwa sababu ya sms! Know and learn how to handle your matrimonial issues without the outside intervention, otherwise utajitwalia kidonda cha mawazo ambacho hakitapona maishani mwako na kwa mwenzi wako! The best way is however, to pray to the one who initiated the Holy Matrimony, God! He is the one who will give you the true peace and patience, not to be regretted! Your partner will truly sorry to you and beg your pardon: "For godly sorrow worketh repentance to salvation not to be repented of: but the sorrow of the world worketh death." (2Cor. 7:10). Stay blessed, all!
 
Kuna jamaa alitumiwa msg kwenye simu yake na hawala yake usiku wa manane basi yule jamaa alikuwa amelala fofofo hajui kinachoendelea mke wake akasikia msg inaingia kusoma 'ile mimba yako niliyokuwa nayo imeharibika' basi zogo hilo mme kaamshwa usingizini mke wake akilia, mke wake akasema kwenye kupenda nje ningekusamehe lakini kwa kutotumia condum sitakusamehe ndoa ikaachika! true story, tusipende kuchokonoa msg za waume/wake ndoa zitaachika kwelikweli.
 
Kuna jamaa alitumiwa msg kwenye simu yake na hawala yake usiku wa manane basi yule jamaa alikuwa amelala fofofo hajui kinachoendelea mke wake akasikia msg inaingia kusoma 'ile mimba yako niliyokuwa nayo imeharibika' basi zogo hilo mme kaamshwa usingizini mke wake akilia, mke wake akasema kwenye kupenda nje ningekusamehe lakini kwa kutotumia condum sitakusamehe ndoa ikaachika! true story, tusipende kuchokonoa msg za waume/wake ndoa zitaachika kwelikweli.
Kwa hiyo unataka kusema bora aendelee kuchokonolewa nje ya ndoa yako kwa miaka kadhaa kama yule MC na wewe uletewe makombo nyumbani kisa hutaki kujua mkeo hutumia msg na nani?.
 
ahahaha...duuu..his story kama ya kusadikika ila mara 1-1 huwa inatokea....nini sasa cha kufanya

1- si vizuri kuchunguzana hasa katika vitu personal kama simu na hata emails (imagine ungekuta sms ya mama mkwe wako kwenye simu ya mkeo ikimwambia aachane nawe atembee nje ya ndoa yako na mtu mwingine/...ungemchukuliaje mama mkwe wako??)

2- kuacha sio best option...nadhani kuuliza au kutafuta ukweli ni busara tosha na ni vizuri ukianza na mkeo then malizia kwa bwana coleman

3- ni vizuri pia kuachia an allowance for love...dont take things for granted kuwa wake au waume zenu ni waaminifu 101%..wengine mmeoana baada ya kugundua mnavyo vitu vya kidunia vya ku-share na sio vitu vya rohoni kidhati kama pendo la kweli

4- kama wewe ni muumini mzuri wa dini zote basi chukulia haya ni majaribu unapitishwa kupimwa imani yako....maana kwa kigezo cha sms ya mapenzi hakuna ushaidi ki-dini na kwa imani nyingi za dini kuweza kumwacha mwenzi wako huyo wa ndoa.

ni maoni tuu wadau
 
hakya mungu kaka pole.

mna mda gani ndani ya ndoa?
mna watoto? wangapi
siku ya kwanza kukutana na mkeo ilikuwa baa, stand,barabarani, kanisan,sokoni, kwao?

kwa kukwa adhabu unaijua wewe basi ila kama ni ushauri basi piga chini maana halua haina kipolo!!
 
mimi siwezi kutana na meseji kama hiyo halafu nikaka kimya,NO WAY
 
Back
Top Bottom