Merkel ndie mwanamke mwenye nguvu zaidi duniani

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
*25.08.2011*|*02:00 UTC



WASHINGTON

Jarida la Forbes limemtaja kansela wa Ujerumani Angela Merkel kama mwanamke mwenye nguvu kubwa kabisa duniani. Jarida hilo limemueleza Bi Merkel kuwa kiongozi asiyetiliwa shaka wa Umoja wa Ulaya na kiongozi wa uchumi wake halisi duniani.

Orodha ya jarida la Forbes ya wanawake wenye nguvu kubwa duniani inatawaliwa na wanasiasa, wafanyabiashara wanawake na viongozi katika sekta ya habari na burudani.

Waziri wa mambo ya nchi za kigeni wa Marekani, Hillary Clinton, ambaye alikaribia kumshinda rais Barack Obama katika uteuzi wa chama cha Democratic mwaka 2008 kuwania urais wa Marekani, ameorodheshwa wa pili, akifuatiwa na rais wa kwanza mwanamke wa Brazil, Dilma Rousseff. Hii ni mara ya tano kwa kansela Merkel kuongoza orodha hiyo.
 
Hivi hawamuoni mama yetu wa Monrovia? Binafsi kwa kuiongoza ile nchi tena masikini tena ya hapa kwetu afrika na ikawa kama ilivyo leo Liberia iliyotoka ktk machafuko makuu, Ellen Salirf (sina hakika ktk uandikaji jina) ni zaidi ya mwanamke. Waache wachaguane watakavyo.
 
Back
Top Bottom