Meridien BIAO

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,201
113,481
Hii benki kwenye mid 90s ilikuja kwa kasi sana. Baada ya muda si mrefu tukaanza kusikia imeanza kusambaratika.

Hatima yake sijui iliishia vipi. Nani anaikumbuka hii benki? Au wengi wenu humu bado mlikuwa shule za vidudu na msingi?
 
Meridian BIAO Bank .... ikiwa pale mkabala askari monument .... sasa hivi ni Tanzania Postal Bank (TPS Bank) ... zamani ilikuwa Tanzania Watch Assembly

kilichojiri ni kwamba Rais wa zamani wa zambia Keneth Kaunda alikuwa na majority shares akaziondoa ndipo bank ile ikaishia kapuni
 
Mkuu nadhani unachanganya na GreenLand Bank!
 
Merdidian Biao Bank ilikuwa pale Sukari House, na ilipofilisika wafanyakazi wake wengi walichukuliwa na Stanbic Bank

Stanbic Bank in Tanzania is a member of the Standard Bank Group of South Africa and was established in May 1995 when the Standard Bank Group acquired the operations of Meridien Biao Bank Tanzania Limited.
 
Hii Benki haikufikisika, Bali ilifukuzwa nchini.
Iliyofilisika ni ya Uganda.

Nakumbuka hii ya hapa walikataa katukatu kua wamefilisika, walidai kua wao hawahusiani na wa Uganda but haikusaidia.
Mwishowe wakawaita wateja wao na kuwaambia chukueni tu hela zenu, lakini hatujafilisika.

Mwishowe watu wakaanza kusema kuna sababu za kidini (sizijui)
 
Haya asanteni ninyi vijana wa 90's enzi hizo sisi wengine tulikua primary tena za chini ya mti tunaenda peku shuleni na ada zetu za noti ya sh 200 na madaftari ya bure................... ila hayo yenu ya mabenki siyajui coz nimeanza kutumia huduma za kibenki mwaka 2000
Asanteni sana ndugu zangu, siku ya leo nimejifunza jambo hili jipya............ Ama kweli JF ni zaidi ya darasa
 
Hii benki kwenye mid 90s ilikuja kwa kasi sana. Baada ya muda si mrefu tukaanza kusikia imeanza kusambaratika.

Hatima yake sijui iliishia vipi. Nani anaikumbuka hii benki? Au wengi wenu humu bado mlikuwa shule za vidudu na msingi?

jengo lake nimeliona majuzi hapa jijini, muulize dakta idris atakupa mkanda mzima wa kilichotokea
 
Nyani Ngabu
Nakumbuka lile tangazo lao kwenye redio: "Meridian Biao Pan African Bank".
Hii benki ilikuwa tawi la bank ya kinigeria (West Africa). kilichofanyika ni utapeli ambao ulichangiwa na ushamba na uzembe wa BoT.
Meridien BIAO walisafirisha dola milion 30 toka Tanzania kwa kisngizio cha kwenda kusaidia matawi yake ya nje, then wakabaki na pesa ndogo sana Tanzania. BoT hawakupaswa kuruhusu ile transfer,huo ulikuwa uzembe on the side of BoT, lakini by then BoT walikuwa wana ushamba wa kudeal na private banks from abroad kwa sababu Meridien BIAO ndiyo ilikuwa bank binafsi ya kwanza ya kigeni.Hata hivyo, rushwa has to be ruled out!
Kabla ya kucollapse Tanzania, benki hii pia ilipata matatizo hayohayo Kenya na Zambia. Kuna uwezekana hawa watu walikuwa wanatumia mwanya wa ushamba wa nchi hizi kufanya utapeli.
 
Last edited by a moderator:

Aha! Nadhani wanigeria ndo hapo walipo pata hela kuanzisha na kufadhili bokoharam, si hawa jamaa kila walipo wanajiendesha kwa hela chafu!! Mfano alshaabab Somalia (uhalamia baharini) bokoharam nigeria (udanganyifu wa kitapeli) Taliban afighanistan na Pakistan ( madawa ya kulevya) heziballah Lebanon (madawa ya kulevya + money laundering ) alqaida duniani kote (money laundering ) pamoja na misaada ya kisisiri kutoka uarabuni na persia.
 
Last edited by a moderator:
Hii Benki haikufikisika, Bali ilifukuzwa nchini.
Iliyofilisika ni ya Uganda.

Nakumbuka hii ya hapa walikataa katukatu kua wamefilisika, walidai kua wao hawahusiani na wa Uganda but haikusaidia.
Mwishowe wakawaita wateja wao na kuwaambia chukueni tu hela zenu, lakini hatujafilisika.

Mwishowe watu wakaanza kusema kuna sababu za kidini (sizijui)

Hii MEridien wakati huo tulisikia kuwa, ilikuwa INAKUJA KASI SANA, na matokeo yake benki za magharibi wakawa na wasiwasi watapitwa sana na hii benki, wakafanya hujuma ili ife, sijui nini kilitokea lakini nilisikia ni hujma za mataifa ya magharibi ndio ile benki ikashia,

Hii GreenLAnd mkuu ni kweli, magharibi na hila zao kama kawaida, wakajidai kuwa kuna magaidi wanaopitisha pesa zao katika beni hii, so wakaitia hila za kupitia sababu za magaidi na kuilazimisha benki ifungwe hapa kwetu na kwengine kote, hawa watu wabaya sana, Ile meridien ilikuwa inakuwa kwa kasi ya ajabu na ilikuwa beni kubwa sana.
 
Ile benki iliyokufa pale ambapo kuna POstal Bank ilikuwa benki ya Uganda kama sikosei
 
Aaaah Mkuu NN. Umenikumbusha mbali sana na hii Greenland Bank. Kasoro kidogo tu watuibie Watanzania. MUNGU MKUBWA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom