Mental health[with a light touch]

uporoto01

JF-Expert Member
May 23, 2008
4,700
1,415
Statistics show that 1 in 4 people has some kind of mental disorder however small,so look at three of your best friends if they are okay than its probably you.
 
Nina wasiwasi huyu jamaa ni daktari wa magonjwa ya akili,kwani hawa ndo wenye matatizo ya kumuuona kila mtu ana tatizo katika akili yake.
 
Statistics show that 1 in 4 people has some kind of mental disorder however small,so look at three of your best friends if they are okay than its probably you.

Za leo ndugu, kwa nini umeseme hivyo, unaweza kutupa sababu zilizokupelekea kusema hivyo kama wewe ndie sie mgonjwa wa akili.
 
According to statistics, watu wanne kupanda juu yaani kuanzia Lorain, ni jina la LAGATEGE, so inamaanisha ukianzia chini kwenda juu jina la nne ni la lagatege so inawezekana kati ya hao watu wannne ni yeye ndio mwenye mental disorder...!
 
This is according to reseach done on five continents[10 countries]-american medical journal[sep 2002].I added the socond part for humour[refer-with a light touch].
 
na utafiti huo utathibitishwa hapa hapa, utawaona wengi wanajitokeza wakiwa na mamatizo ya akili
 
Tatizo kubwa nadhani ni kwamba ugonjwa wa akili una negative connotation. Mtu akiambiwa ana malaria, haiwezi kuona kama ni tusi. Lakini akiambiwa ana tatizo la akili anakuwa mkali. Na hata ukiangalia post zilizotangualia hapo juu, mtu ni rahisi sana kumnyooshea kidole mwingine kwamba ana tataizo la akili.

Lakini ukweli wengi wetu tuna matatizo ya akili. Wengine ni madogo madogo tu kwa mfano yanayojionyesha kwenye mtu anayehamaki kwa vitu vidogo, au uoga uliopitiliza. Lakini wengine ni makubwa kama mazezeta, ama wanaoonekana kuokota makopo na hata kuua bila kujua.

Na ukweli pia ni kwamba matatizo ya akili yanaharibu maisha ya wengi tu, na wengi bila hata kujua. Na matatizo mengi ya haya yana matibabu. Lakini kwa sababu una-associate matatizo ya akili na kichaa uliyemuona anaokota makopo, mtu ukiambiwa kichaa unakuwa mkali kidogo.

Na ukweli kabisa ni kwamba watu wenye matatizo ya akili hupata shida sana. Tungekuwa tunalijua hilo pengine watu wasingekuwa wanathubutu kumcheka mtu wanayemwita kwamba ni kichaa. Mtu yoyote, saa yoyote akili inawezaenda mrama. Na ikitokea hivyo utapenda usaidiwe na sio kuchekwa.

Mifano wa matatizo ya akili

Matatizo ya akili yapo aina nyingi sana. Hapa nitajaribu kutoa mifano michache ambayo pengine itaweza kutupa mwanga kidogo kuhusu akili kwenda mrama. Na pengine itasaidia ukiambiwa na dakitari una tatizo la akili usipate hasira kwa sababu ni matatizo ya kawaida ingawa usipopata tiba yana athari kama magonjwa mengine kwenye maisha yako. (Nitayaita kwa kimombo kwa sababu kiswahili ama yote tunayaita kichaa, ama tuna majina ya dalili tu za magonjwa haya.)

Obsessive-Compulsive Disorder
Tatizo hili linahusiana na woga. Mtu anakuwa muoga sana wa kitu fulani, na anatumia muda wake karibia wote kufanya kila analoweza kuhakikisha kile kitu hakimpati. Na anakuwa na taratibu kabisa ya jinsi gani ya kufanya, step by step.

Mtu anaweza kuwa anaogopa sana kuugua magonjwa ya tumbo, na kwa kujua kwamba kunawa mikono kunapunguza uwezekano wa kuugua, basi anakuwa anaosha mikono yake muda wote, kiasi kwamba kama wewe ni ndugu yake ama mwenza wake, na hujui kwamba huyu mtu anatatizo, unaweza kukereka. Akishikana na mtu mkono, lazima atafute bomba na sabuni anawe. Akifungua mlango kwa kushika handle ile, anaenda kunawa. Akiingia nyumbani cha kwanza ni kunawa. Na kunawa huku si kunawa tu, ni kwa kujsugua hasa. Kwenye movie moja (sikumbuki jina) kuna dada alikuwa na tatizo hili, na alikwa anasugua mikono mpaka inaanza kutoa damu ndio anaacha. Sio ngumu kufikiri kwamba hii inatokea hata kwenye jamii yetu. Na ukimuuliza hakufichi anakwambia anataka mikono yake iwe safi. Sasa mbaya ni pale anapokuwa na wasiwasi kwamba hata sabuni anayotumia ni chafu ... Matokeo yake mtu kama mtu anaweza akawa anaogopa hata kutoka nje, kama ni kazi ataacha, kama ni watu ndio hatataka kukutana nao. Kwa sababu hataki kuchafuka.

Mtu huyo anakuwa anakosa amani kabisa pale anapokuwa hajafanya hiyo ibada yako. Kwa mfano akashikana mkono na mtu halafu asipate bomba la kunawa ujue kila kitu kingine kitasimama. Hata kama ni kuacha mkutano aende nyumbani kunawa atafanya hivyo ...

Bipolar Disorder
Hili ni tatizo la moods ama temper. Mtu huyu moods zake zina-swing all the time. Mtu saa nyingine anaraha kupita kiasi, kila kitu kinafurahisha, maisha ni mazuri, na kila mtu ni rafiki, kila kitu kinachekesha, etc. Baada ya muda kila kitu ni opposite, na kila mtu ni adui, na kila kitu kinaudhi.

Ukiona mtu mara kwa mara anaswitch moods isivyo kawaida, au bila sababu za msingi, kuna uwezekano ana BD. Sasa hivi atakuwa anacheka na wewe, mara analia umemuangalia vibaya ...

Premenstrual syndrome (PMS)
Ni kundi la dalili za kisaikolojia ambazo hutokea kwa wanawake wengi walio kwneye umri wa uzazi. Mdada anaweza kujisikia anakereketwa na hasira bila sababu maalum ya msingi, kukosa raha, nakadhalika.

Dalili hizi ni tofauti kati ya mwanamke na mwanmke, na uzito wake huwa tofauti kati ya mwanamke na mwanamke pia. Wengine PMS haiwazuii kuendelea na shughuli zao za kila siku. Lakini wengine inaweza kuwa mbaya kiasi cha kutoweza kufanya hivyo.

Premenstrual dysphoric disorder (PMDD) ni PMS kali sasa. Madada anaweza akawa analia bila sababu maalum, kuwa na hasira, kukosa raha kupitiliza, kushindwa ku-concentrate, kichwa kuuma, moyo kwenda mbio, kujisikia kuchoka, kupata hamu ya mapenzi zaidi, kupanic-panic, nakadhalika.

Huwa inatokea kila mwezi, na yaweza kupotea siku chache baada ya hedhi.

Kama wewe ni mwanamme, utashangaa unafokewa tu bila sababu ya msingi. Mara umetimuliwa tu bila kosa. Mara analia tu from no where kwamba umpendi tena.

Schizophrenia
Sasa huyu nadhani ndio baba wa kichaa. Na wengi tukisikia ugonjwa wa akili, schizophrenia ndio inakuja kichwani.

Dalili zake ni kama kusikia sauti zinakuongelesha (auditory hallucinations), kuona maono ya vitu visivyopo (visual hallucination), kuwa na imani zisizoendana na ukweli (delusions), kusema hovyo na kufikiri hovyo (disorganized speech and thinking).

Hiyo unaweza kuiona kama ni list tu ya dalili. Na ukiwa darasani, unakariri na kutema kwenye mtihani ili upate maksi. Lakini hawa watu huwa wanapata shida sana.

Kwa visual hallucination kwa mfano, imagine unaona mijitu ya ajabu ajabu inakuja inataka kukuua. Unayakimbia na kupiga kelele kuitete nafsi yako. Lakini watu wengine wote wamekaa tu wanakutazama, kwao wewe unakichaa, mwehu, lakini wewe unayaona kabisa haya makitu ...

Mdogo wangu amesomea udaktari (mimi hapana, mi mzushi tu) akanipa story moja iliyotokea hapa TZ. Mama moja amepelekwa mahakamani kwa kumuua mtoto wake kwa kumkatakata tumbo na kisu.

Inaweza kuwa rahisi kumhukumu maisha au kifo. Lakini hebu sikia upande wake. Yeye alikuwa anamuogesha mtoto wake, sasa akaanza kuona kanyoka kako chini ya tumbo la mtoto (ka-uume). Akakimbilia kisu, akakata na kutoboa tumbo. Mara akawa anaona manyoka yanazidi (utumbo), ndio akazidi kuyashambulia. Mtoto hawezi pona hapo. By the time anaona nini kimetokea, ndio anazidi kuchanganyikiwa. Anajua alikuwa anauwa manyoka, sasa nini kimetokea kwa mtoto wake?

Kwa auditory hallucination, mtu anaweza akawa anasikia kabisa kwamba wewe na mwenzako mnapanga kumroga. Na ninavyosema kusikia na maanisha kusikia. Na anasikia discussion yenu nzima. Sasa huyo mtu akikuwakia unamuita kichaa lakini amekusiki mnapanga kwenda kumroga.

Mtu mwingine anakuwa anasikia sauti ya mtu ambaye ndio anakuwa anamshauri. Sasa wewe ukimuona unasema huyu ni kichaa anaongea pekeyake. Lakini, amini tu kwamba huwa anaongea na mtu. Saa nyingine anamsikiliza huyu mtu na kumuamini kupita kiasi. Sasa mbaya ni pale huyu mtu anapokuwa anamshauri vitu vibaya. Chukulia wewe ndio rafiki yake, halafu huyo mtu akamwambia kwamba leo wewe utakuja kumuua. Ukienda kumtembelea kuna uwezekano akakutokea na pange. Ni rahisi kwako kusema amechanganyikiwa, ni kichaa. Lakini kwake yeye ni jinsi ya kujitetea na kulinda uhai wake.

Na kama auditory hallucination ikijichanganya na visual hallucination, anaweza akawa anakutana na huyo mtu kabisa. Ndio, kwenu huyu mtu hayupo, lakini kwake yupo. Wala haiusiani na uchawi ndugu, maana huwa tunapenda kupata explanations rahisi-rahisi. Ni kwamba ubongo unakosea kufanya kazi sawasawa.

Kama unataka kuelewa vizuri dunia ya mtu mwenye schizophrenia ilivyo, tafuta movie inayoitwa "A Beautiful Mind". Inazungumzia maisha ya kweli ya mtu anayeitwa John Forbes Nash, ambaye ni mathematician mzuri na mshindi wa Nobel (kwenye economics nadhani). Na ana hicho mnachokiita kichaa. Story yake ni nzuri kwa sababu ni mmoja wa watu wachache sana ambao wameweza kupigana na kichaa chao bila ya kutumia dawa (ingawa muda mrefu wa maisha yake ulipotea bure, na isingekuwa hivyo kama angetumia dawa). Kwamba alifika mahala akaweza kutofautisha mambo ya kweli na hallucinations; kwa mfano kujua kama anayemwona mbele yake ni mtu wa kweli au ubongo wake umemtengenza. Story ya maisha yake ipo kwenye hiyo movie, na kwenye kitabu chenye jina hilo hilo. Na inakupa picha nzuri ya ulimwengu wa tunaowaita vichaa, ambayo si rahisi kuipata.

John Nash alipokuwa chuo, kwa mfano, alikuwa na roomate wake, wanaishi pamoja, kuongea, nakadhalika. Lakini jirani zake wanamshangaa John Nash mbona anaongea peke yake huko chumbani muda wote? Na ukweli ni kwamba hakuwa na roomate: Visual + Auditory hallucinations zimepandiana baba. Baadaye sana kwa msaada wa mke wake ndio akaanza kuelewa kwamba kuna vitu anaviamini ambavyo havipo kabisa.

Chakufanya ...

Ukijihisi unatatizo la akili, au ukihisi ndugu yako anatatizo la akili, ni muhimu sana kucheki na wataalamu mapema. Jinsi ambavyo tatizo linafanyiwa kazi mapema ndio jinsi uwezekano wa kupata msaada mzuri unakuwepo.

Matatizo mengine ya akili yakicheleweshwa yanakuharibia maisha kabisa.

Na kwa wale wanaopenda kukimbilia kuwanyooshea vidole wenzao kwamba wanamatatizo ya akili, ningewashauri mwende pale muhimbili, wodi ya wagonjwa wa akili. Tumia muda kidogo tu pale, ongea na watu. Ukipata mgonjwa mmoja wa kuongea naye, ongea naye ukiwa open minded kabisa. Nina uhakika utajifunza mengi sana ambayo huyajui kuhusu jinsi ubongo wako unavyofanya kazi.

Na pengine unaweza kugundua hata wewe una-kaugnjwa kako ka akili.
 
Here in 2020 I like this why are there no replies ,nataman sana hii chat sbb ninawasi wasi juu yangu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom