Meno ya Tembo yageuzwa makopa

ITSNOTOK

Member
Jul 19, 2011
44
10
Kuna habari kwamba kuna basi la Buffalo linalofanya safari zake kutoka Dar es salaam kupitia Lindi, Mtwara Mpaka Tunduru lilikamatwa mwaka jana (2011) Masasi likiwa na Meno ya Tembo. Baada ya kukamatwa inasemekana kesi ilifunguliwa pale Masasi (Mtwara) na baadae kuhamishiwa Mtwara.
Taarifa ambazo zimesambaa kwa wakazi wa Masasi hivi sasa ni kwamba, askari walifanya makosa kukamata basi hilo kwa kuwa hayakuwa meno ya Tembo bali yalikuwa makopa (mihogo iliyokaushwa kwa ajili ya kusaga unga).

Kutokana na hilo, serikali inatakiwa kulipa hasara yote iliyopatikana kutokana na basi hilo kusimama kufanya kazi.

Vinavyowachanganya wakazi wa masasi ni hivi:
1. Askari wameshindwa kabisa kutofautisha meno ya Tembo na Mihogo(makopa)!
2. Basi limekaa muda mrefu sana kituo cha polisi, bado wasijue wameshikilia mihogo (makopa) badala ya meno ya tembo!
mwisho wa siku hawajaelewa .......

Note: si rahisi kutaja chanzo cha habari, ila fika masasi uliza wakazi, fika kituo cha polisi uliza basi la buffalo linafanya nini kituoni, fika mahakamani uliza kesi ya meno ya tembo katika basi la buffalo,- ilikuwa ni katika uongozi wa Nape Nauye (DC Masasi)
 
Kwa hiyo? Nape ndiye aliyebadili meno ya tembo na kuwa makopa au una maana gani? hueleweki unajuwa?
 
Hio nimeikuta mtwara na mtu mmoja muhusik mkuu aliniambia kazi yote ya kubadili meno ya tembo kuwa makopa ilifanyika kilwa, kuna vibibi huko noma, hata una kesi ya kuua au madawa ya kulevya wanabadili na ukaonekana huna hatia, hii sayansi ya mbwantu iko sana pwani ya kuanzia mkuranga hadi mtwara.
 
Back
Top Bottom