Meno ya tembo 1241 yakamatwa bandari ya Zanzibar

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Kwenye habari ya leo saa 2.00 usiku, ITV wameonesha meno yapayo 1241 yakiwa
yanasafirishwa kwa njia haramu bandari ya Zanzibar.

Imeongezwa kuwa polisi walishtukia magunia hayo yaliyokuwa na dagaa na ndani yake yakiwa yamefichwa mano hayo.
Mwandishi ameeleza pia kuwa bandari ya Zanzibar haina vifaa vya kisasa hivyo wahujumu uchumi hawa huwa
wanapita hapo sana.

Mmoja alikuwa ni mchina na ndo mmiliki na mbongo mmoja alikuwa anafatilia mzigo huo.

Walionekena maaskari wakichoma choma kwenye magunia hayo kwa vyuma ambavyo naamini ni
kama vya kujitengenezea. Nimeshangaa sana! Hiyo ndo Tz! Ila tujiulize yafuatayo:
  • hao tembo walikufa wangapi?
  • lini waliuliwa?
  • mali asili walikuwa wapi?
  • mzigo wote huo umetokea wapi?
  • kina nani wamehusika?
  • ni mangapi yamekuwa yakiibwa kwa siku, mwezi au mwaka?
INAUMA SANAMTU KUUA TEMBO WOTE HAO ILI ATOE MENO (PEMBE ZA NDOVU)
 
shamba la bibi hili!wachina,waarabu na wahindi wanapora maliasili zetu kwa kutudanganya wa bongolala kwa vi laki 2!
 
shamba la bibi hili!wachina,waarabu na wahindi wanapora maliasili zetu kwa kutudanganya wa bongolala kwa vi laki 2!

Lakini mkuu kuna haja ya kuwawajibisha kwa mbinu za kuibusha hisia za nguvu ya umma
 
Tunalea, tunawanyima wafugaji wetu eneo la kufugia na sisi ataufaidiki chochote na wanyama! Nasikia pia Selou nayo imeuzwa
 
Kazi kweli kweli! Halafu eti wanasema kuna kitengo cha usalama wa wanyama pori. Wezi wakubwa!
 
maswali yako ni mazuri sana, hata hivyo naomba nikukumbushe kuwa ufisadi tz umeanzia kwenye mtaa. inaonekana jamaa alitoa rushwa bara kote alikopita akaishiwa kabla ya kutoka pemba. Bara acheni umbumbumbu, nilishangaa sana kona wasomimi wanasukuma gari la jairo unafikiri itawezekana kukomesha uharamia wa rasilimali zetu kwa staili hii.
 
Tembo 1241 wameuliwa ili pembe za ndovu zipelekwe kwa wataiwan sijui wachina emola lini tutakomboka sisi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom