Tatizo la meno kufa ganzi na chanzo chake

Bakulutu

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
2,541
1,755
Habari Jf members,

Nasumbuliwa na meno yangu yote kufa ganzi kiasi kwamba mara nyingi taya zinachoka kutokana na kuzuia meno yasigusane.

Pia juzi niling'oa jino moja baada yukuonekana limepekechwa,but nilipo mueleza Dk. kuhusu kufa ganzi alionekana kushtuka kidogo,Kasema ngoja nipone jino nililotolewa then nirudi.

Pia naona meno mawili yaliopo usawa wa pua yamekuwa marefu sana kama ya mnyama anaekula nyama sasa naona kama yana sababisha kukosekana kwa balance ya meno!

Please naomba ushauri kabla sijarudi hospitalini.

=======
1590750234389.png

Meno kufa ganzi ni matokeo ya kumomonyoka kwa enameli (dental erosion) na kuifanya kuwa dhaifu na kupelekea jino kufa ganzi kutokana na kumomonyoka kwa enameli.

Hizi ni baadhi ya sababu za matatizo ya meno.

Matumizi mabaya ya mvinyo Mvinyo una kiwango kikubwa cha asidi ambayo huharibu sehemu ngumu ya nje ya jino inayoitwa enameli na kuacha matundu madogo kwenye meno yanayosababisha kuhifadhi vitu vinavyoweka rangi kwenye meno. Mfano; mvinyo mwekundu una chembechembe zinazoitwa ‘chromogens’ pamoja na ‘tannins’ ambavyo huweka rangi kwenye meno. Wanywaji wengi wa mvinyo hunywa taratibu kwa muda mrefu, hivyo kufanya tindikali (acid) iliyomo kwenye mvinyo iharibu meno.

Pia tindikali hiyo husababisha kumomonyoka kwa enameli (dental erosion) na kuifanya kuwa dhaifu. Kama meno yako yameathirika kwa kuwa na rangi isiyokuridhisha na wakati mwingine kufa ganzi kutokana na kumomonyoka kwa enameli na unafikiri imetokana na matumizi ya mvinyo kama maelezo hapo juu, basi punguza matumizi haya na pata ushauri wa daktari wa kinywa na meno kutibu tatizo la ganzi.

Kutafuna kucha Tabia hii inaweza kusababisha sehemu ya jino kusagika, kuwa dhaifu na hata kuvunjika. Pia na matatizo katika viungo vya taya na hivyo kuleta maumivu karibu na eneo la masikio (Temporomandibular joint dysfunction). Chanzo cha tabia hii kinaweza kuwa ni mazoea tu, au msongo wa mawazo na kazi. Ili kuacha tabia hii kata kucha kwa kutumia kifaa maalumu kwa wakati, epuka msongo wa mawazo na jitahidi kuwa na mpangilio mzuri wa kazi zako.

Kusafisha meno kwa kutumia nguvuUsitumie nguvu wakati wa kusafisha meno kwani unaweza kusababisha kuharibika kwa fizi zako na sehemu ya jino inayopakana na ufizi. Tumia mswaki wenye brashi laini na muda wa wastani wa dakika mbili, mara mbili kwa siku.

Kutumia meno yako kama kifaaTabia kama kufungua kizibo cha chupa, kufungua pakiti ngumu kama za maziwa kwa meno, kushika vitu kama sindano, kushikilia au kumenyea nyaya (kwa mafundi wa umeme, betri), kushikilia misumari (mafundi ujenzi) n.k. Kazi ya meno ni kutafuna chakula si kutumika kama kifaa mbadala. Tabia hizi zinaweza kusababisha meno kuvunjika au kujiumiza mdomoni, au hata kumeza vitu hivyo kwa bahati mbaya.

Tabia ya kutafuna vitu vigumu kama mchele Hii husababisha meno kusagika au kuweka nyufa na maumivu au ganzi kwa baadhi ya meno na hata kuvunjika kwa kipande cha jino. Tabia hii huanza taratibu kwa kuiga na baadae kuwa mazoea. Kuwa mbali na vitu hivyo vinavyotamanisha kutafuna kunaweza kusaidia kuacha tabia hii.

Kula vitu vyenye sukari mara kwa mara Kula kashata, ufuta, ubuyu, visheti, biskuti, pipi, keki, bazoka (Big G, orbit, n.k.) mara kwa mara, hasa vile vyenye sukari huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kuoza kwa meno. Mabaki ya vyakula hivi hutumiwa na bakteria (wanaoozesha meno) kutengeneza asidi inayoharibu sehemu ngumu ya nje ya jino na kuacha matundu. Punguza matumizi ya vyakula vyenye sukari, njia mojawapo ikiwa ni kuvitumia vyakula hivyo wakati unapokula milo mikuu mitatu.

Matumizi ya kahawa Rangi ya kahawa huweka rangi kwenye enameli (sehemu ngumu ya nje ya jino) na asidi iliyopo ndani yake huweza kusababisha enameli kulika, hivyo rangi ya asili ya meno kupungua na kuanza kuwa na rangi ya njano kadiri muda unavyopita.

Kutafuna penseli au kalamu Tabia ya kutafuna penseli au kalamu inafanywa na watu wengi hasa wanapokuwa kwenye masomo, au kazi zinazohusisha kuandika na wakati mwingine msongo wa kazi nyingi. Tabia hii inaweza kusababisha meno kusagika kama itafanyika kwa muda mrefu. Kama unatabia hii ni vizuri ukatumia bazoka isiyo na sukari (sugarless gum), kila unapohitaji kutafuna kitu. Matumizi ya bazoka husaidia kuongeza na kusisimua mate kutoka mdomoni hivyo kuimarisha meno na hata kuzuia mashambulizi ya asidi.

Kuvuta sigara Matumizi ya sigara na tumbaku za aina yoyote huweza kusababisha meno kubadilika rangi na kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa fizi. Pia matumizi ya tumbaku yanaweza kukusababishia saratani kwenye ulimi na mdomo. Tumia mbinu mbalimbali kukwepa na kuacha kabisa kuvuta sigara. Pamoja na madhara mengi ya kiafya yanayoweza kusababishwa na uvutaji wa sigara, sigara haina faida yoyote katika mwili na maisha ya binadamu kwa ujumla.

Kutafuna barafu Kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya barafu na vinywaji baridi na vikali, baadhi ya watu hupendelea kutafuna barafu wakati wa kunywa vinywaji vyao. Kutafuna barafu kunaweza kusababisha meno kuvunjika, au kuweka nyufa zisizoonekana. Hii huweza kusababisha kupata maumivu au hali ya kufa ganzi wakati wa matumizi ya vitu vya baridi au vya moto. Pia barafu iliyovunjika inaweza kuwa imechongoka na kuweza kusababisha kidonda kwenye fizi na ulimi. Inashauriwa badala ya kutafuna barafu, iache iyeyuke mdomoni, kama wewe unapendelea raha ya ubaridi wa barafu mdomoni kwako.

Kusaga na kutafuna meno (Bruxism) Kusaga na kutafuna meno ni tabia inayohusisha msuguano wa meno unaotokea wakati wa usiku au hata mchana hivyo husababisha meno kusagika, kulika na kuweka nyufa ndogo ndogo kwenye sehemu ngumu ya jino na kuumwa kwa misuli ya uso na viungo vya taya. Pia meno huweza kupata ganzi mara kwa mara na kupata shida ya kutafuna. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kutumia kizuizi kinachoitwa “night guard” wakati wa usiku na ushauri nasaha kutoka kwa daktari wa afya ya kinywa. Ganzi kwenye meno inaweza kutibiwa kwa kupaka dawa maalumu inayozuia ganzi pamoja na kutumia dawa ya meno inayopunguza ganzi (toothpaste special for sensitive teeth)

Matumizi ya chupa za lishe kumlazia mtoto Hii itamfanya mtoto awe anategemea kulala akiwa na chupa mdomoni–ya juisi, maziwa au lishe yoyote. Matumizi ya chupa hizi bila mpangilio yanaongeza uwezekano wa kuoza meno kwa kasi (rampart caries). Inashauriwa chupa hizi zitumike kwa matumizi ya lishe tu, si kitu cha kumbembelezea mtoto ili alale usingizi.

Kutoga ulimi, mdomo, mashavuKutoga ulimi kunaweza kusababisha kuvuja kwa damu nyingi pale mshipa mkubwa wa damu utakapotobolewa. Pia kidonda kisipotunzwa vizuri huweza kupata maambukizi na kushindwa kupona kwa wakati. Kipini cha urembo kinachowekwa kwenye ulimi, mdomo au mashavu kinaweza kusababisha jino kuvunjika pale kiking’atwa kwa bahati mbaya– au kutengeneza nyufa ambazo zitakuwa zinauma na hata kusababisha ganzi kila unapokula kitu cha baridi, moto au hata hewa ya baridi ikiingia mdomoni.

Matumizi ya tembe za kulainisha koo (throat lozenges) Tembe hizi mara nyingi huwekwa kiwango kikubwa cha sukari hivyo kukuongezea hatari ya kuoza kwa meno. Tabia ya matumizi ya chembe kama kiburudisho ni hatarishi kwa afya ya meno. Matumizi yasiyo sahihi, ni matumizi ya mara kwa mara yasiyohitajika. Tembe hizi zikitumika kwa muda mfupi hazina madhara yoyote kwenye meno.

Kutafuna popoo, tambuu na mirungi
Hii hufanya meno kuwa na rangi isiyopendeza, meno hupoteza uimara wake na kutengeneza nyufa, mdomo kutoa harufu mbaya, huongeza uwezekanao wa kupata ugonjwa wa fizi na ina kilevi kinachosababisha uteja (addiction). Matumizi ya vitu hivi hujenga tabia ya mazoea (addiction) ambayo inahitaji ushauri nasaha na matibabu kutoka kwa madaktari wa saikolojia.

Wadau wengine wenye tatizo la meno kufa ganzi:

Heshima wakuu,
Mimi ninatatizo la jino moja tu la mbele kupata ganzi ninapokunywa maji ya baridi au ninapo vuta upepo. Please naomba mwenye ushauri hapa jamvini anisaidie.
----
Wapendwa habari!meno yananisumbua saana kiasi kwamba mpaka sasa nimeshatoa matano na mengine bado yananiuma na kufa ganzi,na wasi wasi yataisha yote hata kabla sijazeeka. Nimetumia dawa nyingi za meno kama dynacare,forever bright,sensodyne na nyingine nyingi sikumbuki majina yake.

Nikianza kutumia dawa mpya yanatulia sisikii maumivu kabisa lakini baada ya kipindi furani kupita hali inarudi pale pale.

Nashindwa kuelewa kama pipi nilizokua namung'unya sana nikiwa shule ndio sababu ya haya yote maana nilikua napenda saana pipi muda wote ipo mdomoni labda wakati wa kulala.mwenye solution plz nijurishe.thanx
----
Naomba kuuliza kwa wataalamu wa meno. kuna hili tatizo la meno kufa ganzi(yaani meno kuwa kama yalikula maembe machachu kisha kkuma na kushindwa kutafuna chakula).

Hivi hili tatizo linatibika na kuisha au ni life time problem? naomba kujua tiba yake ni nini mbali na matumizi yasiokwisha ya dawa ya meno ya sensodyne.

Michango ya wadau:
Kwa kitaalamu hilo tatizo linaitwa hypersensitivity, mara nyingi huwa linatokea hasa pale ambapo ,mmhusika anatumia mswaki ambao kitaalamu hautakiwi kwa matumizi ya meno.

Yaani mswaki wenye brash ngumu ambao hujilia kuondoa lea ya nje ya jino yaani enameli , na mara nyingi huwa inatokea hasa kwenye shingo ya jino ,pale ambapo ufizi unaanzia , sehemu hii pamoja na lea ya ndani ya jino yaani dentine, inavitundu vidogo dogo sana ( stomata poles) ambavyo huruhusu upenyo wa kitu chochote chenye tindikali ,umaridi ,pamoja na umoto kupenya kiurahisi na kusababisha hali ya ganzi.

Lakini pia hali hii huwatokea watu ambao , wanapolala usiku huwa na tabia ya kutafuna meno na hivy kuondoa ile lea ya juu ya jino (enamel) lakini pamoja na hayo pia huwatokea watu ambao meno yao yanakuwa wiki , hasa kutokana na ukosefu wa madini , calcium, fluoride,
TIBA
Mwone daktari akujuze kama kuna meno yaliyotoboka
Zingatia namna ya upigaji mswaki hasa muda usizidi dakika 15.
Daktari atafanya matibabu yameno yako kulingana na yalivyoathirika.
Mwisho daktari atakuelimisha ni dawa gani inafaa kwa meno yako.
----
Safi umeeleza vizuri ,enamel layer ya kwanza kwenye jino inakuwa imeanza kuwear out ,the sehemu ya jino inayofuata inakuwa sensitive
hii husababishwa na acidic food sometimes kuna kuwa na dental carries
hard toothbrush na nguvu nyingi hukwangua meno pia na kuexpose dentine ,TIBA njoo kwa dentist kujua tatizo ili upate tiba sahihi ,kwasasa tumia SENSODYNE AMA colgate sensitive .karibu ekenywa hospital Magomeni mwembe chai 0762291006
\t

m
 
Go to a dentist he will do a thorough examination after a proper history taking then he can be in a good position to help with your problems, there should be underlying cause for the numbness, also with the elongation of teeth there are several causes including Truma, disease of the gum, (periodontitis),some of systemic diseaaes and others.

ADVISE

Go back to a dentist immediately
 
Thax sir,i will go back soon.
 
Heshima wakuu,
Mimi ninatatizo la jino moja tu la mbele kupata ganzi ninapokunywa maji ya baridi au ninapo vuta upepo. Please naomba mwenye ushauri hapa jamvini anisaidie.
 
Wapendwa habari!meno yananisumbua saana kiasi kwamba mpaka sasa nimeshatoa matano na mengine bado yananiuma na kufa ganzi,na wasi wasi yataisha yote hata kabla sijazeeka. Nimetumia dawa nyingi za meno kama dynacare,forever bright,sensodyne na nyingine nyingi sikumbuki majina yake.

Nikianza kutumia dawa mpya yanatulia sisikii maumivu kabisa lakini baada ya kipindi furani kupita hali inarudi pale pale.

Nashindwa kuelewa kama pipi nilizokua namung'unya sana nikiwa shule ndio sababu ya haya yote maana nilikua napenda saana pipi muda wote ipo mdomoni labda wakati wa kulala.mwenye solution plz nijurishe.thanx
 
Ukiwa unasubiri watalaam chukua maji yaliyo chemshwa yakapoa weka chumvi halafu utumie pamoja na hizo dawa za memo kusugulia meno.
 
Naomba kuuliza kwa wataalamu wa meno. kuna hili tatizo la meno kufa ganzi(yaani meno kuwa kama yalikula maembe machachu kisha kkuma na kushindwa kutafuna chakula).

Hivi hili tatizo linatibika na kuisha au ni life time problem? naomba kujua tiba yake ni nini mbali na matumizi yasiokwisha ya dawa ya meno ya sensodyne.
 
Me nilikuwa na ilo tatizo nilipoenda hstpl kucheki nikaambiwa limetoboka, tangu nilipozba hadi leo ni miaka 4 niko fresh nadunda
 
Kuna dada mmoja alinipa dawa ya kusukutua meno
ni nzuri kama uko bongo pm nikuambie anavyopatikana.

naomba kuuliza kwa wataalamu wa meno. kuna hili tatizo la meno kufa ganzi(yaani meno kuwa kama yalikula maembe machachu kisha kkuma na kushindwa kutafuna chakula). hivi hili tatizo linatibika na kuisha au ni life time problem? naomba kujua tiba yake ni nini mbali na matumizi yasiokwisha ya dawa ya meno ya sensodyne.
 
Pole sana, nenda kwa daktari wa meno akakague meno yako ili kujua kama hakuna tatizo na hayajachimika hasa kwenye muunganiko na mzizi kutokana na namna unavyopiga mswaki!
 
Hata mimi hili tatizo huwa linanisumbuaga wakuu, likishanza huwezi kabisa kutafuna vitu vigumu kama maindi ya kuchoma au krips n.k
 
Wataalamu nimewahi kwenda mmoja akasema hakuna tatizo yaani meno yako safi hayajaaribika bali yamelika leya ya juu ndio maana yaana kuwa sensitive. akashauri kutumia sensodyne forever, tatizo hii dawa ikizoea meno haisaidii tena tatizo linajirudia.
 
kuna dada mmoja alinipa dawa ya kusukutua meno
ni nzuri kama uko bongo pm nikuambie anavyopatikana.
We ungetuambia ili tupate msaada hata wa namba za simu. haya matatizo sio ya kupigia ramli, naomba uweke hadharani please.,:A S-cry:
 
Back
Top Bottom