Mkuu wa chuo
JF-Expert Member
- Feb 3, 2011
- 7,608
- 5,269
kweli polisi muda mwingine wanatumiwa hadi wewe Zomba mzee wa saigon wamekutosa, au hawakujua kama wewe ni mzee wa saigon!
Hujui msimamo wangu dhidi ya jeshi la polisi fuatilia michango yangu kwenye mauji ya muuza magazeti Morogoro na Iringa.
Hunisomi vizuri, rejea posts zangu, "Ntasema kweli daima, uongo kwangu ni mwiko".
Iwe isiwe, kuna malalamiko mengine mengi ya upinzani yana ukweli ndani yake.
Nasema hili kwa kuwa nimeshuhudia dhulma zinazofanywa na Serikali kwa macho yangu. Ukweli ubaki kuwa ukweli.
Kuna mtu kaja kunihadithia juzi, kuwa kuna vijana watatu na mzee mmoja wamekamatwa kwa tuhuma ya wizi na wako Polisi kituo cha Wazo Hill na wamekataliwa dhamana kwa sababu tu, tajiri aliyewashtaki amesema wasipewe dhamana.
Sikuamini nilivyoambiwa hayo, ikanibidi jana nitengeneze safari ya kwenda kituo cha Polisi cha Wazo Hill. Naam, nikawakuta kweli hawa watu wameshikwa na wapo ndani kwa wiki nzima sasa na wamenyimwa dhamana. Cha kushangaza zaidi ni kuwa wizi wenyewe wanatuhumiwa si wa kupora wala kunyang'anya, ni wa shoti iliyotokea kituo cha mafuta cha BP Boko, ambacho hakiuzi hata mafuta ya uwiano wa millioni 20 kwa siku.
Nilipofika kituo cha Polisi OCD akakataa kabisa kuniona wala kunisikiliza nilipomona nje ya kituo nikamueleza huku anatembea, kuwa "nakuja kuulizia kuhusu waliokamatwa kwa wizi wa millioni 80". Akanitazama, hakunijibu ndee wala sikio.
Katika kuwaulizia ndugu na jamaa wa "wafungwa" nikaoneshwa kikundi cha kina mama upande mmoja na kina kaka upande mwingine, nikaenda kuwajulia hali na kuwauliza kulikoni? Kisa walichonipa kinanifanya leo hii nikiri kuwa hii Serikali ina mambo inayoyafanya bila sheria na kwa dhulma.
Wale kina mama walinieleza kuwa wameongea na Kova, wameongea na Kenyela lakini swala lao wamekuwa wakipigwa danadana na wote hao. Kisa na sababu kwa kuwa aliyeshitaki ana fedha nae si mwingine bali ni kijana anaesemekana kuwa kaiweka Serikali mkononi kwa fedha zake kwa jina la Badr, mmiliki wa vituo vya GBP.
Cha kusikitisha na kushangza zaidi nilipoongea na wale kina kaka, mmoja wao akasema "mimi nafanya kazi kwa Badr" nimekuja kufatilia namna ya kumwekea dhamana Mzee ambae ni dereva wa gari la mafuta, lakini nimekataliwa, na sijui kinaendelea nini na OCD hataki kuongea na mtu".
Akazidi kunielezea kuwa huyu "Badr" anatumia Polisi kuhalalalisha amma alipwe Insurance kwa kusuka nao hizi kesi za wizi amma huwa anatumia hizi kesi kukwepa kodi. "hii siyo kesi ya kwanza, kama unabisha kamchunguze uone huko nyuma ameshawabambikia wangapi kesi kama hii" alisema huyo kaka, akifikiri mie ni mwandishi wa habari.
Kenyela, Kova, Mwema, Nchimbi, Kikwete. Haya hamuyaoni?
Hivi ni sheria gani inayoweza kumuweka kifungoni mtu ambae hajaua, na kumyima dhamana bila kumfikisha hata mahakamani kwa siku 8 mfululizo?
"Badr" ana ukaribu na hao mapolisi wakubwa wote akiwemo na Mwema, kwa mujibu wa huyo anaefanya kazi kwake ambae kaja mtafutia dhamna dereva aliyepo ndani.
Mawakala wa Badr wanaokwenda na kurudi huko Polisi mmoja anaitwa Mzee Nassor (Nasa) mmoja anaitwa Musa, wamewaambia hawa ndugu jamaa na marafiki, kuwa "nyie nendeni hata kwa Kikwete, sie tunatumia fedha, tuone fedha au kujuana ndio kutashinda".
Natamani majibu ya haya, kutoka kwa wanasiasa na wana harakati wa haki za binaadam, Mdee upo? sio kwako huko? Dili hilo.
Nimeipenda hii,hayaZomba...km kweli umeguswa
Leo Zomba kawa kundi moja na sisi tunaolalamikia dhuluma za polisi? Ndio anayaona leo? Kumbuka usemi wa Father Martin Niemoller wa Ujerumani, tafuta kwenye google ujue aliongea nini!
zomba ni mnafiki,akipewa pilau ataanzisha thread mpya ya kuwasifia polisi..polisi wa tz wataendelea ktuua na hawatafanywa kitu na serikali ya magamba kwa sababu wanawahakikishia kuwepo madarakani...
wakati huo tunafatilia yeye avae t-shirt ya kijani na mimi nitatupia gwanda.lakini muulize je anakubali kuwa serikali ya CCM imewekwa mfukoni?