Mengine ya Upinzani yana Ukweli... Polisi wanatumiwa

Sasa Kikwete hayuko madarakani na serikali yake? grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr

Yaani hapa nazungumzia mawaziri na manaibu wao. Unajua mkuu hii serikali ukiichunguza kwa umakini ina malengo mazuri sana ya kututoa kwenye umaskini. Lakini kwa bahati mbaya viongozi ikiwa ni pamoja na mawaziri ndiyo wanaoharibu kila kitu. Mimi kwa kweli sina tatizo na serikali ila ninaona maadui zetu wakubwa ni mawaziri.
 
Yaani hapa nazungumzia mawaziri na manaibu wao. Unajua mkuu hii serikali ukiichunguza kwa umakini ina malengo mazuri sana ya kututoa kwenye umaskini. Lakini kwa bahati mbaya viongozi ikiwa ni pamoja na mawaziri ndiyo wanaoharibu kila kitu. Mimi kwa kweli sina tatizo na serikali ila ninaona maadui zetu wakubwa ni mawaziri.

sasa serikali kwani si ni watu? na watu hao wengine si ni mawaziri? au mawaziri ni mawaziri wa serikali gani kama siyo hiyo hiyo yenye "malengo mazuri"?
 
sasa serikali kwani si ni watu? na watu hao wengine si ni mawaziri? au mawaziri ni mawaziri wa serikali gani kama siyo hiyo hiyo yenye "malengo mazuri"?

Nadhani hapo ndiyo sehemu ambayo watu wengi huwa wanachanganya sana kwa kudhani kuwa serikali na mawaziri ni kitu kimoja. Kuna tofauti kubwa tu kati ya mawaziri na dhana ya serikali. Serikali ni kitu 'abstract' ambacho kinahold matajarajio na ndoto za wananchi kwa umoja wao wakati mawaziri ndiyo wale watu wanaopaswa kuaccomplish mitazamo ya serikali. Kwahiyo kushindwa kwa mawaziri kutelekeza 'ndoto' za serikali ndiyo kunapelekea taifa kwa ujumla wake kushindwa kupata mafanikio ya mipango yake. Kwahiyo nasimama kwa mtizamo wangu kuwa sina tatizo na serikali ila nina ugomvi mkubwa sana na mawaziri--na Rais wa nchi bila shaka--kwa kushindwa kutekeleza adhma ya serikali.
 
Funguka FF funguka, ukiamua kufunguka utayaona na kuyasikia madudu mengi sana yanayofanyika ndani ya hii Serikali dhalimu.
FF mtoto wa Kariakoo leo ameshuhudia na kudhihiri utendaji 'nadhifu' wa serikali 'sikivu' ya JK..this is hilarious..
 
umekuwa siku zote ukishabikia na kutetea watu kunyanyaswa, kuteswa na hata kuuwawa ukiweka mbele itikadi za kichama na dini ... mfano ... Marehemu Mwangosi (RIP) alipouwawa kikatili na polisi ulikuwa unahaha kwenye threads zote ukiwatetea polisi ... sasa nimeamini kwamba Shida haina mwenyewe

kwa kuwa imani yangu inasisitiza kuhusu upendo na ndiyo amri kuu, inafundisha kusamehe, kutolipiza kisasi, kutokuwa na chuki dhidi ya wengine, kutokumuombea mtu mabaya na kuwa na busara wakati wa matatizo, kuheshimu utu wa binadamu mwingine na kutohukumu hapa duniani ... basi naomba nichukue fursa hii kukupa pole na haya yaliyowapata na ninawatakia mafanikio mema, .... tupinge dhuluma hii kwa pamoja ... Tanzania ni moja na sisi ni wamoja
 
By Zomba
Iwe isiwe, kuna malalamiko mengine mengi ya upinzani yana ukweli ndani yake.

Nasema hili kwa kuwa nimeshuhudia dhulma zinazofanywa na Serikali kwa macho yangu. Ukweli ubaki kuwa ukweli.
Naona saa ya ukombozi inakaribia kama hata kina Zomba sasa wamefumbuka macho na kuona dhulma za serikaali hii. A luta Continua; Mapambano yanaendelea!
 
Naona saa ya ukombozi inakaribia kama hata kina Zomba sasa wamefumbuka macho na kuona dhulma za serikaali hii. A luta Continua; Mapambano yanaendelea!
Well said Mkuu, yafaa Zomba aelewe kuwa hata sisi tulikuwa makada wa CCM tena wapiganaji wa mstari wa mbele; lakini tulibadilika tulipobaini matatizo.
 
Nitasema kweli daima, uongo kwangu mwiko!
Nitasema kweli daima, fitina kwangu ni mwiko.
Nakubaliana na wewe zomba juu ya observation yako. Polisi kama taasisi kwa sasa ina underperform.

Viongozi wa Idara hii muhimu ya dola inabidi watambue kuwa hakuna siri y milele, ukweli ukujulikana kwa wananchi utaua moyo wa ushirikiano ambao umekuwepo kwa miaka mingi.

Mfano wa Polisi jamii ni mafanikio ya ushirikiano huo.
 
Last edited by a moderator:
Polisi wetu wakati mwingine hata kama hawajatumiwa rasmi huwa wanajitumikisha wenyewe kutokana tu na uoga! Ni polisi wachache sana wenye uthubutu wa kufuata sheria endapo wanaamini sheria hiyo itamuathiri kwa namna moja au nyingine mtu mwenye influence fulani kwenye jamii! Nakumbuka miaka kadhaa iliyopita nyumba ya Jenerali Ulimwengu ilivunjwa na kuibiwa vitu kadhaa.

Moja ya vijana ambao walikamatwa ni ndugu yangu! Tulifanya jitihada kubwa kumtolea dhamana kijana yule lakini tuligonga mwamba kisa tu polisi walimuogopa Jenerali Ulimwengu; kitu ambacho sizani kama kweli Ulimwengu aliamrisha kufanya hivyo! Kijana yule alikaa rumande kwa miezi kadhaa ingawaje hapakuwa na ushahidi wala mazingira ya kumtuhumu achilia mbali kumtia hatiani! Alikuja kuachiwa miezi kadhaa baadae baada ya Ulimwengu mwenyewe kuipotezea kesi hili kwani hata mahakami alikua hatokei(si yeye wala mwanasheria wake)!

Hivyo basi, tatizo kuu linalowakumba polisi wetu ni uoga na kutojiamini ingawaje ni kweli wakati mwingine inakuwa ni baada ya kushinikizwa kutotekeleza wajibu wao. Na hili linachangia zaidi kutokana na ukweli kwamba askari wengi vituoni hata shule zao ni za kutia mashaka hivyo kukosa weledi wa nini hasa polisi anatakiwa kutekeleza wajibu wake! Manake siamini endapo askari kwenye vituo vya polisi wangekuwa na uelewa na weledi wa kutosha bado wangeweza kutii maagizo yasiyo halali ya wakuu wao.
 
Hiyo ndio polisi inavyo fanya kazi siku hizi ni pesa mbele!

Hakika umeona tukio dogo tu kuna matukio mengi yana fanywa na jeshi la polisi ni ya kusikitisha sana, wana nyanyasa raia kupitiliza.
 
Mpaka yakukute mwenyewe ndio unajua sio?ndio Ukome

kila siku tunapiga kelele wanyonge wanavyoonewa na POLICCM, TBCCM na serikali yenu Chama cha Magambaz lakini wewe unabeza, Thank God yamekukuta na Mungu hamfichi mnafiki

Nadhani kuanzia sasa utakuwa umeanza kuelewa maana ya kuvua gamba na kuvaa gwanda ni nini.

Nitasema kweli daima, uongo kwangu mwiko!
 
Back
Top Bottom