Mengine ya Upinzani yana Ukweli... Polisi wanatumiwa

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
Iwe isiwe, kuna malalamiko mengine mengi ya upinzani yana ukweli ndani yake.

Nasema hili kwa kuwa nimeshuhudia dhuluma zinazofanywa na Serikali kwa macho yangu. Ukweli ubaki kuwa ukweli.

Kuna mtu kaja kunihadithia juzi, kuwa kuna vijana watatu na mzee mmoja wamekamatwa kwa tuhuma ya wizi na wako Polisi kituo cha Wazo Hill na wamekataliwa dhamana kwa sababu tu, tajiri aliyewashtaki amesema wasipewe dhamana.

Sikuamini nilivyoambiwa hayo, ikanibidi jana nitengeneze safari ya kwenda kituo cha Polisi cha Wazo Hill. Naam, nikawakuta kweli hawa watu wameshikwa na wapo ndani kwa wiki nzima sasa na wamenyimwa dhamana. Cha kushangaza zaidi ni kuwa wizi wenyewe wanaotuhumiwa si wa kupora wala kunyang'anya, ni wa shoti iliyotokea kituo cha mafuta cha GBP Boko, ambacho hakiuzi hata mafuta ya uwiano wa millioni 20 kwa siku.

Nilipofika kituo cha Polisi OCD akakataa kabisa kuniona wala kunisikiliza, nilipomuona nje ya kituo nikamueleza huku anatembea, kuwa "nakuja kuulizia kuhusu waliokamatwa kwa wizi wa millioni 80". Akanitazama, hakunijibu ndee wala sikio.

Katika kuwaulizia ndugu na jamaa wa "wafungwa" nikaoneshwa kikundi cha kina mama upande mmoja na kina kaka upande mwingine, nikaenda kuwajulia hali na kuwauliza kulikoni? Kisa walichonipa kinanifanya leo hii nikiri kuwa hii Serikali ina mambo inayoyafanya bila sheria na kwa dhulma.

Wale kina mama walinieleza kuwa wameongea na Kova, wameongea na Kenyela lakini swala lao wamekuwa wakipigwa danadana na wote hao. Kisa na sababu kwa kuwa aliyeshitaki ana fedha nae si mwingine bali ni kijana anaesemekana kuwa kaiweka Serikali mkononi kwa fedha zake kwa jina la Badr, mmiliki wa vituo vya GBP.

Cha kusikitisha na kushangaza zaidi nilipoongea na wale kina kaka, mmoja wao akasema "mimi nafanya kazi kwa Badr" nimekuja kufatilia namna ya kumwekea dhamana Mzee ambae ni dereva wa gari la mafuta, lakini nimekataliwa, na sijui kinaendelea nini na OCD hataki kuongea na mtu".

Akazidi kunielezea kuwa huyu "Badr" anatumia Polisi kuhalalalisha amma alipwe Insurance kwa kusuka nao hizi kesi za wizi amma huwa anatumia hizi kesi kukwepa kodi. "hii siyo kesi ya kwanza, kama unabisha kamchunguze uone huko nyuma ameshawabambikia wangapi kesi kama hii" alisema huyo kaka, akifikiri mie ni mwandishi wa habari.

Kenyela, Kova, Mwema, Nchimbi, Kikwete. Haya hamuyaoni?

Hivi ni sheria gani inayoweza kumuweka kifungoni mtu ambae hajaua, na kumyima dhamana bila kumfikisha hata mahakamani kwa siku 8 mfululizo?

"Badr" ana ukaribu na hao mapolisi wakubwa wote akiwemo na Mwema, kwa mujibu wa huyo anaefanya kazi kwake ambae kaja mtafutia dhamna dereva aliyepo ndani.

Mawakala wa Badr wanaokwenda na kurudi huko Polisi mmoja anaitwa Mzee Nassor (Nasa) mmoja anaitwa Musa, wamewaambia hawa ndugu jamaa na marafiki, kuwa "nyie nendeni hata kwa Kikwete, sie tunatumia fedha, tuone fedha au kujuana ndio kutashinda".

Natamani majibu ya haya, kutoka kwa wanasiasa na wana harakati wa haki za binaadam, Mdee upo? sio kwako huko? Dili hilo.

Latest Development;

Nimeongea na mmoja wa ndugu wa watuhumiwa kwa simu mudaa huu huu, anasema walikwenda leo hii Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wakiambatana na wakili, walipofika huko wameambiwa hilo faili la hao watuhumiwa lilikwenda kwao na toka jana waliwaeleza Polisi kuwa hao watuhumiwa hawana kesi ya kujibu na waachiwe.

Polisi inaendelea kuwashikilia dhidi ya maagizo hayo kwa kuwa tu bwana mkubwa Badr hajasema waachiwe.

Latest Update:

Watuhumiwa 3 wamewachiwa leo kwa dhamana, mtuhumiwa mmoja hana mashtaka ya kujibu, kawachiwa huru.

Kesi imebadilishwa badala ya Millioni 80 imekuwa Elfu 80!.

OCD wa Wazo Hill kahamishwa kituo.

RPC Kinondoni na RCO wabishana kuhusu hili sakata!


Nimeongea kwa simu na mmoja kati ya ndugu wa watuhumiwa, anakuja kunielezea kwa kirefu jinsi hii nyuzi ilivyosaidia. Nikipata habari kamili ntakuja ifungulia nyuzi.

 
Iwe isiwe, kuna malalamiko mengine mengi ya upinzani yana ukweli ndani yake.Nasema hili kwa kuwa nimeshuhudia dhulma zinazofanywa na Serikali kwa macho yangu. Ukweli ubaki kuwa ukweli.Hivi ni sheria gani inayoweza kumuweka kifungoni mtu ambae hajaua, na kumyima dhamana bila kumfikisha hata mahakamani kwa siku 8 mfululizo? Natamani majibu ya haya, kutoka kwa wanasiasa na wana harakati wa haki za binaadam, Mdee upo? sio kwako huko? Dili hilo.
Kuwa objective kunaleta michango ya mawazo iliyo mizuri zaidi. ungekuwa hivi siku zote ungeona members wanaleta maoni mazuri.
 
@Moderator, naomba badili "Yan" iwe Yana.
 
Mwenye nguvu mpishe mzee hiyo mbona unajua au umejisahaulisha kimakusudi pole kwa kuona dunia halisi.
 
Mpaka yakukute mwenyewe ndio unajua sio?ndio Ukome

kila siku tunapiga kelele wanyonge wanavyoonewa na POLICCM, TBCCM na serikali yenu Chama cha Magambaz lakini wewe unabeza, Thank God yamekukuta na Mungu hamfichi mnafiki

Nadhani kuanzia sasa utakuwa umeanza kuelewa maana ya kuvua gamba na kuvaa gwanda ni nini.
 
Zomba,
Mambo ya utawala wa kisheria na haki si ya upinzani peke yake. Tunachotaka sisi ni kuona kuwa sheria zinaheshimika na hakuna mtu aliye juu ya sheria hata kama ana hela kiasi gani. Bila hicho kitakachofuata ni anarchy. Haki kwa wenye fedha na majina na dhuluma kwa wanyonge na wasiojulikana. Hii siyo Tanzania aliyotaka kutujengea Mwalimu Nyerere. Kwa pamoja tunaweza kuirudisha Tanzania kwenye mwelekeo stahiki.
 
zomba Kwa kweli hizi ni habari za kweli na hii imekua nu tabia ya wafanyabiashara wengi hasa Wahindi ambao wamekua wakitumia polisi kuhakalisha kulipwa mabilioni na kampuni za bima ama kuwadhulumu wafanyabiashara wakubwa wa nje wanaowaletea bidhaa kuziuza nchini na wengine ili kukwepa kodi.

Upo mfano wa Kampuni moja iitwayo Lotus Africa ambayo inamilikiwa na Wahindi wawili mtu na mkewe, ambapo mume alifanya wizi mkubwa na kukwepa kodi katika kampuni ya Midcom akiwa mfanyakazi na fedha ndio akaanzisha kampuni zake Uganda, Kenya na sasa Rwanda. Huyu mhindi anaitwa Venkath na mkewe anaitwa Sandya na kwa kweli mimi nilimshitukia tokea mwaka jana nikaachana naye lakini nasikia kila mwezi anatoa taarifa polisi kuwa ameibiwa. Hii ni hatari maana sasa Jeshi la polisi linatumika kukandamiza raia wake kwa maslahi ya wachache tena baadhu hata si raia wa Tanzania na wamekuja hapa nchini wakiwa hawana kitu na sasa wanawaleta wenzao na kuanza kushirikiana kuiba na kuwaumiza Watanzania. Mifano iko mingi sana jamani na wengine hata vibali vyao vya kuishi ni vya magumashi
 
Last edited by a moderator:
Zomba,
Mambo ya utawala wa kisheria na haki si ya upinzani peke yake. Tunachotaka sisi ni kuona kuwa sheria zinaheshimika na hakuna mtu aliye juu ya sheria hata kama ana hela kiasi gani. Bila hicho kitakachofuata ni anarchy. Haki kwa wenye fedha na majina na dhuluma kwa wanyonge na wasiojulikana. Hii siyo Tanzania aliyotaka kutujengea Mwalimu Nyerere. Kwa pamoja tunaweza kuirudisha Tanzania kwenye mwelekeo stahiki.

Uko sahihi Jasusi, hapa hakuna chama na wanaoumia utakuta wengi ndio hao wanaojiita eti ni CCM.
 
Kwa kweli Tina umetoa mwanga na hapa waandishi wana hoja nzuri sana ya kuchunguza a kuangalia kodi wanazolipa hawa wenzetu ambao wanakuja na kutumia watumishi mafisadi na kuanza kunyanyasa wazalendo.

Tusikubali maana kuiba wanatuibia na bado wanatesa wenzetu.
 
Taratibu utaelewa na bado kitambo kidogo utavua gamba..its just the matter of time wait and see..
sio kujiita karibu wote hao wanaonyanayswa ni CCM lakini watalalamika pembeni na baadae watachangishana pesa na kuwapa polisi badala ya kwenda kwenye maeneo yao na kulalamika na ikibidia kuwabana viongozi waliowachagua na kuwaambia ukweli kama wanashindwa kuwatetea watawanyima kura. silaha kubwa ya wwnyinge ni kura zao
 
Funguka, ukiamua kufunguka utayaona na kuyasikia madudu mengi sana yanayofanyika ndani ya hii Serikali dhalimu.
 
Back
Top Bottom