Susuviri
JF-Expert Member
- Oct 6, 2007
- 3,713
- 888
Hawa wote ni makada wa CCM na wamenufaika sana na ukada wao. Sitashangaa kama hawataitwa pembeni na kuambiwa waache mchezo wa kitoto. Sitashangaa kusikia kuwa Mengi na Rostam wakitoa joint statement wakisema haya yote yalichochewa na mkono wa tatu. Mengi atafuta kesi na Rostam ataondoa vielelezo vyake au Takukuru watasema tu hakuna ushahidi! Mwaka 2010 wote kwa pamoja watazunguka nchi nzima kumnadi mgombea wa chama chao! Na nyie mliotegemea makubwa mtabaki kugunia chini chini!
Amandla.......
Fundi Mchundo, mi nimejitoa ktk ushabiki huu lakini nimekuwa nikifuatilia maoni na nimeona ya kuwa unachokiandika are my thoughts on this issue. Muda umefika wa kuendelea na mjadala unaoleta maendeleo na kuachana na ushabiki. Anyway, let them have their 15 minutes of fame until the next issue comes up na tutasahau yote...