Umem discredit Masha based on maneno ya Mengi (umesema kama hizi habari ni kweli basi Masha fisadi) halafu hapo hapo ume kandya maneno ya Mengi kwamba anatatufa populatity. Kama maneno ya Mengi nayo ni discreditable sasa wawezaje kuyatumia kumhukumu Masha ?
Kwanza habari za siku Mwanamke wa Kiafrika, unapotea mno kwenye mapambano na kuibuka siku za ushindi, huna mpango!
Mengi amefanya udaku kwa kudokezadokeza identity ya "waziri kijana" akiogopa, akishindwa kujiamini kuanisha anatachotaka kusema. Ndio nilivyomaanisha, aache kuwa wussy na mdaku.
Wote uanza kwa kuita udaku. Clinton & John Edwards na wengine wengi walianza hivyo kwa kusema ni udaku lakini mwisho wakaishia kuja na definition za ajabu ajabu za ubazazi wao.
Naomba ukumbuke dalili ya mvua ni mawingu na panapofuka moshi kuna moto. Unaweza ukawa na data lakini likija suala la technicalities za kortini kuhusu defamation unakuta umebanwa mbavu. Mengi anawanasheria wazuri natumai wameasesi mazingira yote na kuamua atoke kama alivyotoka. Kaa chini fikiri kisha utajua kwamba Mengi anajua analolifanya.
Mwombe radhi Mengi katika hilo!