Reginald Mengi Lawyers respond (video), goes to Court; sues Rostam Aziz

Madela.. yaani umenishtua mzee maana check yangu imebounce maana Mengi ameua makampuni yake mengi na sasa hana tujisenti. Ila kambi ya RA siiwezi bwana labda nijiunge na Bakhresa....

Aisee!Kwa Bakhersa nako kuna mlo?Kweli nchi yetu imeendelea na inasonga mbele, milo iko mingi watu kwa ujinga wetu tu tunalaza damu na kubaki tunalalamika.Asante kwa kunitonya ubarikiwe.
 
hii inapakwa rangi kama vile ni suala la vita kati ya hao kina ra na mengi. mi naona kama haikustahili kuwa kama hivyo. hata kama ra angekuwa rm na rm akawa ra bado isingestahili aliyesemwa kuwa fisad awali (ra) aone hiyo sasa ni issue kat yake na mtuhumu (rm).

hii ni kwasabab ra hajachukua kitu cha rm as rm. na huenda matatizo yaliyosababishwa na ufisad wa ra yamemuathri kwa kias kidogo zaid rm na jamaa zake kuliko kilivyomuathiri bib yangu kule kijijin na mie. hii ni kat ya ra na watz kama mie zaid. zilikuwa ni pesa za nchi

anachofanya mengi ni kusema eh jama eh, mnalalamika barabara mbovu? hamna shule? shule zilizopo hazina vifaa vya kufundishia? hospital hamna? vifaa mahospitalin havipo? na nk.? mnajua anayekwiba pesa zenu? mnajua adui wenu? ni ra.

sasa hapo ra anasema na wew unaiba. na pia anasema onyesha kama nimeiba. kwa mazingira yetu vyote viwil havimfanyi mwizi kutokuwa mwiz. havimfanyi fisad kutokuwa fisad. kama na rm anaiba au ni fisad haiwez kuhalalisha ufisad wa yeyote - si ra na wala si rm. na kama rm hana vyombo vinavyoweza kumsaidia kuprove ufisad wa ra hii haimaanishi kuwa yeye ra si fisad. suluhisho ni kuuthibitishia uma wa watz kwa kutumia vyombo vyake lukuki vya habar na vinginevyo kuwa yeye si fisad

anyway rm anaandamwa kwasababu wengine wengi tumejifungia/tumejificha huku tukilalama chin chin oh jamaa katuibia, oh jamaa anatulostisha etc. tunafanya kwa kificho. anayejitokeza ni mmoja mmoja kama rm saa hiz. kwa hiyo anakuwa easy target. wengine tumejifungia na watoto wetu vyumban. tunaona mambo yanakwenda mrama lakin hatuthubutu kutoa pua zetu nje.

ni vizuri rm kusema 'ufisad' wa mengi kama upo. lakin hakika ni vizur pia kusema kwa vip yeye sio fisad. mahakama inaweza kutaka rm aithibitishie mahakama kuwa kwavip ra ni fisad. mtu wa kawaida kama mie nilikuwa nategemea ra mwenyewe aseme kwavip yeye sio fisad

a)Ndugu Mengi badala ya kusimama na kujibu hizo shutuma mwenyewe ametumia surrogates. Mtu unaweza kuhisi kuwa amefanya hivi ili aweze kuji-distance baadae kutokana na hayo yatakayosemwa. Kwa nini hakufanya kama alivyofanya aliyemshutumu ili kama kuna fall out yeyote kutokana na haya imkute yeye na si hao aliowatuma?


sijui kwa nin alitumia watu wengine. siungi mkono ufisad wa yeyote. lakin kutumia watu wengine kuelezea kitu hicho hicho ulichotaka kusema kuna ubaya gan? kama hawakueleweka sawa. kama ra akatuma wanasheria wake na wapambe wengine kutuelezea na kutuletea madocument yatakayokidhi kiu yetu ya kupata ukweli wa yanayosemwa juu yake kuna ubaya?

b) Ndugu Mengi anauliza maswali ya kitoto.

i)Badala ya kusema, tarehe fulani fulani Mheshimiwa Rostam ulikutana na afisa fulani wa benki mahali fulani ambapo mkakubaliana kuhusu mkopo kwa kampuni ya Dowans ambao ulithibitishwa na barua ref: namba fulani fulani na ulilipwa kwa mafungu kdha wa kadha kwenye akaunti kadha wa kadha. Badala yake anauliza generalities.

simtetei mengi. lakin kama mengi alipewa hizo 'info' na watu fulani huoni kuwa ingekuwa vibaya kutoa details za ndani za vikao hivyo? ingekuwa rahis kujua aliyevujisha siri ya kikao hicho kat ya ra na benk.

ii) Badala ya kutuambia kuwa hiyo kampuni ya Caspian unayojivunia, mbona fulani na fulani ndio walioorodheshwa kama wakurugenzi na wewe haumo? Mbona hiyo kampuni inadaiwa na TRA kiasi cha shilingi kadhaa kama malimbikizo ya kodi? Yeye anataka Rostam ndiyo ataje makampuni hayo? Ili iwaje? Kama anayajua, si angeyataja tu ili tuone kama Rostam atakuwa na jibu?

nacho ulichoandika hapo juu unaona kinamfanya ra kutokuwa fisad kama anavyosemwa?

iii) Kama Mengi anajua kuwa Rostam alikuwa anaenda benki kujadili kuhusu Kagoda, kwa nini asiseme tu kuwa tarehe fulani na fulani ulienda benki ukakutana na fulani mkajadili masuala ya Kagoda! Anaogopa nini?

hii ni kama (i) hapo juu. na pia hii haimsafishi ra na maneno mabaya juu yake. au labda unataka kuniambia kuwa kama mengi ana hizo habari zote na akaogopa kuzisema hadharani ndo ra atakuwa sio fisad?

iv) Kama Mengi anajua kuhusu uhusiano wa Rostam na wamiliki wa Richmonds kwa nini asiuweke wazi? Hayo maswali ya polisi ya nini?

watu kibao wanajua mambo yalivyoenda tokea richmond, dowans na ra kusema mwenyewe kuwa anawafaham watu wa dowans. na pia vyombo vya habar vimeshaandika sana kuhusu ukaribu wa pm aliyeachia ngaz, ra na presidaa mwenyewe. sa hutafun mwenyewe ukameza?

cha kufanya sis tukishaona mazingira ya kuibiwa tupige kelele. mwizi huyooo..... tumwache yeye aseme kwanin sio mwiz. tukisema tutafute madokument yanayoonyesha jins walivyokwiba hatutokaa tuyapate, maana, wanayahifadhi wenyewe. tutakachokuwa tunashuhudia sie ni kupungua uwezo wa serikali kulipa mishahara, kushindwa kugharamia elimu ya vijana wake, ukosefu wa dawa hospitalin, barabara mbovu zisizohudumiwa na nk.

Rostam angalau aliweka shutuma zake wazi badala ya kuzunguka zunguka. Nyingine Mengi ameweza kuzijibu na nyingine amekaa kimya. Nyingine, majibu yake yamezua maswali zaidi. Lakini hivi ndivyo ilivyotakiwa. Sio huku kuja na platitudes.

Amandla.........

hatuhitaj mafisad tz hii. ra alikuwa wap siku zote hizo kutuletea ufisad wa mengi? au ndo yale yale umenisemelea na mim nakusemelea? sijaupitia huo ufisad wa mengi lakin inavyoonyesha ra asingeusema kama rm asingesema ufisad wa ra

thank you mengi

mwakatojofu
 
Nafikiri mjadala wa ufisadi unaanza kukosa mwelekeo,kwani tunaanza kushindwa kutofautisha kati ya mkopo na wizi. Mkopaji anadaiwa na hata akipelekwa mahakamani hafungwi ila anaamulia kulipa deni kwa maelekezo ya mahakama, je, mwizi anadaiwa? na inapojulikana kuwa aliiba huwa anaamuliwa kulipa? Tanzania tunadaiwa madeni tangu enzi za TANU na ASP je tulishawahi kuitwa taifa la mafisadi? Unajua USA wanadaiwa dola ngapi na WB?
Kuendelea kuufuga ufisadi kwa kuulinganisha na mkopo ni kuendela kuwa mtumwa na mkimbizi katika nchi yako mwenyewe!
 
Back
Top Bottom