Wanasheria wa Reginald Mengi wakutana na waandishi wa habari na Kumjibu Rostam Aziz

Status
Not open for further replies.
majibu

1. atachukua hatua gani na wakati jk mwenyewe anawalinda
2. hao wengine watanao hajawataja kwa ajili hana document zao zilizokamilika na wanajificha nyuma ya mapapa
3. taifa haligawanyiki waindi ni kidogo na wezi na hii ni fact
wacha unafiki wewe mbona jana ukutuma maswali ya rostam

WEWE MNAFIKI NAMBA MOJA. kwani hukuyaona maswali? lazima kila mtu atoe? lazima kila mtu amuulize RA na Mengi asiulizwe? Unajibu wewe ni Mengi? hakuna haja ya kuwa upande wa mtu tunataka waumbuana wajitetee ndio tuamue nani ni nani sio mnarukia majibu. UPUUZI mtupu kama JK anawalinda mbona Mengi yuko msitali wa mbele kumpigia debe kuwa anafanikisha mapambano ya ufisadi wakati kakamata mafisadi DAGAA? TUNAWATAKA PAPA na NYANGUMI WAJISAFISHE WENYEWE, MSITUINGIZE VITANI SISI EBOOOOOOO
 
Binafsi naona hii ni mipasho watuamnie tu wameanzisha vikundi vya taarabu..., Jana RA leo RM vita hii itaendelea weeeeee mwishowe naona utakuwa mbaya kwa mmojawapo sijajua ni nani na siombi iwe hivyo ila nahisi tu
 
..kwa upande wangu, sitishwi na wanaopigishana kelele, Mangi na Manji, bali natishwa na wanaokaa kimya kama ma 'don' wa mafia.

Pia kusema ukweli, mzee Mengi ni mtu mwenye inferiority complex ya ajabu, hivyo kitendo cha kuvurumishiwa makombora ya jana, kimemprovoke, atajibu kwa ukali, kwa hasira na anaweza kujikuta pia anatema na utumbo.

Kwa ushauri wangu wa bure, Mzee wetu Mengi ushauri, asiendelee kujibizana na mafisadi papa ili kuilinda heshima yake.

Kitendo pekee cha kuwataja kwa majina ni japo kinyume cha sheria, ni cha ushujaa wa ajabu kumfanya awe shujaa wa taifa, sasa asiuharibu huo ushujaa kwa kuipiga zaidi hii ngoma yake, mwishowe itampasukia.

Well said pasco juu ya kimya cha JK na wapambe wake.

Hata hivyo Mengi hatakiwi kukaa kimya. Actually, Mengi anatakiwa kuongeza mapigo maana kama, alivyosema Gen. Collin Powell, ukitaka kushinda vita ni muhimu kupeleka mashambulizi yako kwa nguvu sana kuanzia mwanzoni.

Mangi Mengi ni vema hivi sasa akatoa data alizo nazo halafu atumie vyombo habari pamoja na vyake alivyosingiziwa hapo awali kuvitumia vibaya, ili kuwambua hawa mapapa halafu tuone waTZ watakuwa upande upi. Go Mengi.
 
Kwenye Jerry Springler kuna sehemu huwa wanaachia wagomvi wazichape kidogo. NATAMANI IWE HIVYO waachiwe kidogo watoboe siri za uchafu wao alafu ndio DOLA iiingilie kati.

Hapa una maanisha dola gani, bunduki au risasi zitumike?, kama dola mbona tayari ipo ndani ya mchezo. Wewe unafikiri kauli za kina Simba na Mkuchika ni za nini, RA yupo upande wa dola, Hapa Mengi ndiyo aangalie kwani jamaa wamejipanga kummaliza. With people's power Mengi will be stronger than ever.
 
RM nae atanunua muda TBC kujibu mapingo ya RA ili asikiki dunia nzima maana siku hizi tbc inapatikana kwenye dstv. ITV bado ni local....

sipati picha ze komedi orijino watavyo watowa week hii ....aah churaaa
 
Mara nyingine vita vya mafahali vyaumiza nyasi. Tusije kudhurika wadanganyika ambao tumeibiwa sana so far...hawa wote kuna sehemu wanashare common interest. Pengine inside their kingdom, wamegawanyika. Na maandiko mengi yanena any divided kingdom will fall. Nahisi sasa ufisadi, uliogubikwa na wivu pamoja na makundi yawaopata na kukosa sasa wameamua kujeruhiana. Uzuri sasa tunaanza kujua nafasi ya kila mtu mpaka mabosi waliokuwa hawaguswi na wanaonyenyekewa na wakubwa wengi serikalini. Ngoja tuendelee kuyaona.
 
Ni jambo jema mtu kama Mengi Kukutatana na waandishi wa habari. Tunajua wazi hatatoa hotuba za kisiasa kama watu wengine wanao angalia ukaribu wa uchaguzi mkuu ujao. Atatoa hotuba ya Kiuchumi, huenda wote watakaokuwa wanajamii ya IPP watapata mishahara mipya ili ufaninisi wa kazi uwe mzuri.
Nahisi watanzania hawakupata mishahara mipya hapo majuzi ya MEI Mosi, na leo kama atakuwa na la kusema basi ni kuwaongeza mishahara wale wote wa IPP na badhaa zake kupanda bei ilihali iwe mlinganyo uwe sawa na nyongeza ya mshahara.
Watanzania tufunge mikanda pia kwa Bajeti ijayo, kwani uchaguzi nao uko karibu na tunahitaji usimamizi katika majimbo yaliyoongezeka katika kipindi cha Mh, Dr. Kikwete.

Chonde chonde tusifanane na jirani zetu katika kupigania madaraka, wakati sisi ni jamii ya Ujamaa Na Kujitegemea.
Emmanuel

Nairobi- Kenya
 
Huyu mzee alitutabilia tutaifunga Simba 2 -1 matokeo yake yalikuwa 2-2, ila anajisifu alitabili maafa ya Mbagala.

Tapeli tu huyu, anatabiri baada tukio kutokea! Tena alisema B Mkapa atapewa cheo kikuubwaa sana duniani mwezi wa nne mwaka huu wote tutashangaa. Mbona imepita hatujashangaa!
 
Kuna habari kwamba Mengi atakutana na waandishi wa habari leo Jumatatu saa 7 mchana.
Samahani kama nitawakwaza watu, hivi waandishi wa habari na wahariri wao wanaoalikwa kwenye hizi press conference huwa wanaripoti kila kitu mpaka mawazo yao. Vizuri sana, tatizo langu ni MBONA HAWARIPOTI MAMBO YA VIBAHASHA? mfano jana waligawiwa vibahasha sijui vya kaki au vyeupe hawajatuhabarisha kulikua na nini! hebu mtuambie mwafichani?
 
Sidhani kama Mengi alikurupuka kuwataja Mapapa bila ya kuwa na data. Kama leo ataongea itakuwa ni kuziweka data wazi ili kazi ibakie kwa JK na watendaji wake.

A good move in deed. Hakuna kusubiri joto la stori za RA likatua.
Nyie ndio mnawaponza hawa wazee kwa kukazania jicho kwa jicho.

Mimi nimeangalia conference zote mbili, kwa mawazo yangu RA alijiandaa na kama ni mahakamani ametoa utetezi ambao ni more convincing kuliko Mengi. Watu wa RA walifanya kazi nzuri ya kumwandalia mashambulizi yake.

Mengi awaachie hiyo kazi washauri na wataalamu wake kutayarisha majibu pamoja na documents zote, yeye kazi yake iwe na ku deliver.
 
Hapa una maanisha dola gani, bunduki au risasi zitumike?, kama dola mbona tayari ipo ndani ya mchezo. Wewe unafikiri kauli za kina Simba na Mkuchika ni za nini, RA yupo upande wa dola, Hapa Mengi ndiyo aangalie kwani jamaa wamejipanga kummaliza. With people's power Mengi will be stronger than ever.
Nina maana ya DOLA kama hujanielewa BASI. Mengi naye ni mtuhumiwa hapa, may be with people like YOU, NOT ME, mimi niko juu ya mti naangalia mwisho wake.
 
Huyu Peter Noni ni nani mkuu, mwanga kidogo?

nyadhifa zake
Director for Strategic Planning and Performance Review BOT
Planetel Communications Limited ( 16% vodacom TZ) - lakini sasa hivi ameuza kwa mirambo ltd (who is mirambo ???)
 
Manji alidai fidia ya Tsh. 1/= kutoka kwa Mengi, je ameshapewa?

Kweli Mafisadi wana vituko, Tsh 1/=?????
 
Mtanzania,

Unajua inafikia wakti nahisi kutokwa machozi kwa namna mambo yanavyoenda ndivyo sivyo!

Unajua iko hivi: Mengi anashauriwa na wana JF wenzetu na hata Rostam alichokiongea jana kaandikiwa na mwana JF mwenzetu. Tunaelekea wapi?

Pls mnaowashauri hivi, jaribu kuwaonea huruma, mnawachanganya kabisa, wanavyofanya sivyo (labda kama mmedhamiria kuwamaliza kabisa!)

Mkuu Invisible,

Hata mimi hii inanichanganya kabisa. RA yule bubu kule bungeni hawezi kutayarisha zile documents za jana. Naamini kuna watu wenye uwezo Watanzania wenzetu wamemsaidia, pia huenda kuna mkono wa serikali ambayo imesaidia kutoa nyaraka.

Mengi naye anasikiliza mawazo ya kundi la watu wenye hasira, zinaweza kuwa hasira za kweli kwasababu nchi inaibiwa. Lakini wakati wa mapambano, ukitaka kupoteza vita basi tanguliza hasira mbele. Ni muhimu kuwatumia watu nje ya circle yake ili wamshauri, watu ambao wanaona pande tatu za shilingi na wala sio mbili.

JF jumba la fikra limegeuka kuwa uwanja wa mapambano, tumegeuka kutumiwa katika vita vya mapapa na manyangumi. Wakipatana wanatugeukia sisi Sangara na Chato na kutumeza. Tahadhari kwenu!

Upande mmoja unaniambia basi imetosha lakini mwingine unaniambia ongeza popcorns sinema ndio kwanza trailer imeisha, nami nashawishika kuongeza popcorns, halali mtu hapa!
 
Nyie ndio mnawaponza hawa wazee kwa kukazania jicho kwa jicho.

Mimi nimeangalia conference zote mbili, kwa mawazo yangu RA alijiandaa na kama ni mahakamani ametoa utetezi ambao ni more convincing kuliko Mengi. Watu wa RA walifanya kazi nzuri ya kumwandalia mashambulizi yake.

Mengi awaachie hiyo kazi washauri na wataalamu wake kutayarisha majibu pamoja na documents zote, yeye kazi yake iwe na ku deliver.
Nadhani Mengi alikuwa anatafuta platform ya kuanzia sasa inabidi aanze na mmoja mmoja atueleze ni nini anajua kuhusu kuhusishwa kwao na wizi ili nasi tupate picha halisi, ni kweli tayari tunajua hawa ni manyangumi wa ufisadi sasa Mengi aweke ufisadi kwa ufisadi.
Ila alijitahidi kuamsha huu moto upya na kuwa mbichi tena.
 
majibu

kukopa sio dhambi, na wala kampuni kufilisika sio dhambi
RA jana amethibitisha kwamba mengi hela zake ni mikopo benki na hii ndio njia kuu inayotumiwa na wafanyabiashara wote duniani

je source ya hela za RA ni hipi?
au huu ni utajiri wa Peter Noni?
je RA anauhusiano gani na Peter Noni?

Mbona kama umejibu maswali tofauti mzee? Mimi nimeuliza kuhusa accounti ya nje ya Mengi na kujisafisha kwa kwenda mahakamani atafanya lini? Rostam alitaja vitu vingi sana zaidi ya mikopo, mbona umechagua hapo tu?
 
majibu

kukopa sio dhambi, na wala kampuni kufilisika sio dhambi
RA jana amethibitisha kwamba mengi hela zake ni mikopo benki na hii ndio njia kuu inayotumiwa na wafanyabiashara wote duniani

je source ya hela za RA ni hipi?
au huu ni utajiri wa Peter Noni?
je RA anauhusiano gani na Peter Noni?
Semilong,

Ukienda kukopa huku unajua hutarudisha ni wizi. Kwa Tanzania huko nyuma mtindo huo ulikuwa unatumika sana.

Ninachojua mimi karibu kila mfanyabiashara mkubwa alikuwa anafanya hivyo, kwahiyo japo ni kosa lakini huwezi kulinganisha na wale wezi wa EPA.

Mimi japo naona sio sahihi lakini nitakuwa tayari kumpa Mengi the benefit of the doubt kwenye hili la NBC. ILa la CIS inabidi kama ni kweli arudishe hizo pesa ili ziweze kusaidia watu wengine pia.
 
Hehehe
picha ndo kwanza lamalizia trela bado main course haijeanza.
Nitasikitika sana endapo rais niliyempigia kura atashindwa kurejesha heshima ya serikali na kuacha mambo yaende ovyo.

wait a minute...

Isije ikawa hii ni promo ya kututoa ktk main line ya ufisadi ili ionekane kumbe vita yenyewe ni illusion. I am trying to think loud here....
 
majibu

kukopa sio dhambi, na wala kampuni kufilisika sio dhambi
RA jana amethibitisha kwamba mengi hela zake ni mikopo benki na hii ndio njia kuu inayotumiwa na wafanyabiashara wote duniani

je source ya hela za RA ni hipi?
au huu ni utajiri wa Peter Noni?
je RA anauhusiano gani na Peter Noni?
Source ya utajiri wa Rostam ni Biashara haramu ya utumwa aliuza familia yake iliuza ndugu zetu, na sasa anawaibia wajukuu zao.
Utumwa na wizi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom