Mengi in "The 20 Most Powerful People In African Business"

hivi kama huyu mzee anasifa kama hivi kwa halipi mishahara ya wafanyakazi wake pale ipp media maana hawajalipwa tangia mwezi february.......
 
Nimeiona hiyo report ila sijaelewa vigezo maana kuna SSB hapa tanzania nadhani ata fit namba za juu kabisa maana hata amevuka mipaka kwenye biashara zake na analipa kodi sehemu zote alipo!!!

Issue ni vigezo Ila kwa kiasi kikubwa inabidi u subscribe mwenyewe huko Forbes na kuwapelekea data zako. Mimi simuoni Reginald Mengi hata kwa matajiri 10 wa Tanzania pekee wala usiende Africa. Sema ana njia nyingi za kuonyesha kuwa ni mfanyabiashara mkubwa kwa vile anaweza kuwaita walemavu wa Dar es Salaam akawapikia pilau na kuwaletea Twanga, then anapiga picha na kuzipeleka huko duniani kuwaonyesha kuwa baadhi ya kipato chake anagawana na maskini
 
Kweli SSB deserves but I would like to see him more on social responsibility also. Labda anafanya but sijawahi sikia SSB anatoa misaada mashuleni or at hospitals. Mengi is influential sababu anajiingiza sana kwenye kusaidia communities na anapata media coverage.
 
Ki article hakina statistics wala figures zozote. Kinatumia non-committal statements kama "One of the most powerful..."

Reginald Mengi

Nationality: Tanzania
Job: Chairman, IPP Group

Mengi is one of Africa's most powerful media barons. Started out as an accountant; made first millions manufacturing ballpoint pens and selling them to big retailers. Today, he heads IPP Group, a diversified media conglomerate active in East Africa. Assets include 9 newspapers, 2 television stations and 3 radio stations. Also owns a Coca-Cola bottling plant in Dar-es Salaam.

Mwisho wa kunukuu!

 
Issue si kuwa katika orodha ya Forbes. Je chanzo cha utajiri wa Mengi kinajulikana? Je yale mabilioni aliyokuwa akidaiwa NBC iliyouawa na shemeji yake Mkapa alilipa au ndiyo huo ukwasi wenye kutia shaka?

Malipo ya wafanyakazi wa Mengi siku zote ni kwa mbango. Au yale yale ya Rostamali alivyokuwa akifanya kabla ya kurejesha namba?
 
Huyu mzee R.Mengi ni mtu wa kupewa suport na wtu wote Tz hata kama viongozi wetu wa nchi wanamfanyia fitina sisi wa-Tz tumuunge mkono ktk hali yeyote, maana ni mtu anayesaidia jamii pasipo kujali imani zao na anahangaika na aina zote za watu hata walemavu, tunaomba watoto wa Mengi waendelee kuiga mfano wa Baba yao maana amejijengea mapenzi makubwa kwa Taifa hili. Huwezi mfananisha na mfanyabiashara yeyote hapa Tz.
100 kwa 100 NAKUUNGA MKONO
 
Well well, lakini chekini source, hiyo ni blog ya mtu binafsi akiandikia forbes. Hajaeleza influence za watu hawa amekusanya vipi na ku-asses vipi kupata list. Not that i doubt the people's clout and influence, but take it with a pinch of salt. I think he was looking more at creating a balance across the african continent.
Over 7,000 views and only 3 comments on that article?
 
alafu kweli!!!!!!!!! bakhressa vipi, au ndo hataki kujionesha???

Mengi deserves it. Hongera zake.

Lakini wako Wabongo wengi wenye asili ya Kiasia ambao wameachwa kwenye list ya Forbes. Wako kina Mohamed Enterprises,yuko Yusuf Manji,Sabodo,n.k.
Pengine ni muhimu kujua Forbes wametumia vigezo gani kuchagua hiyo orodha yao.

Nakumbuka siku moja nilikuwa nazungumza na mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya kiasia na tukagusia habari ya mvutano wa Manji na Mengi. Yule m-asia alinishangaza kwa kusema maneno yafuatayo,''Hii Mengi bana iko pesa mingi na yeye nafanya biashara zake kisomi,ogopa sana hii Mengi.Yeye hapana longolongo kwenye biashara zake." Mimi nikabaki mdomo wazi!

Mtu kama Manji pesa zake ni za kimchoro mchoro. Nakumbuka habari moja kwamba alinunua jengo la PPF kwa bilioni kadhaa,kama sikosei it was less than 10b/= ,akarikarabati jengo hilo hilo kwa some few bilioni,not more than 30b/= halafu akawauzia tena haohao PPF kwa bilioni zaidi ya 80! Kuna maswala ya EPA na Kagoda,n.k

Kwahiyo inaonekana hata wafanya biashara wenzake wanajua Mengi yuko juu. Most of Indian-origin businessmen wanafanya biashara zao kiujanja ujanja kwa maana ya kukwepa KODI aidha kwa kuwahonga maofisa wa TRA au kupita njia za panya.Most of these guys wana uraia wa nchi 2 au 3 kwa hiyo wakti mwingine si rahisi kujua ni Raia wa Tz,UK,USA au Canada.
 
Ndugu zangu watanzania tunabidi tujivunie maendeleo ya mtanzania mwenzetu Mr. R Mengi, list iliyotolewa na Forbes ya " The 20 most powerful people In African business man". Mr Mengi ni mtanzania aneyetutoa na kuipa Tanzania sifa nzuri, sio kila saa tunaongela habari za mafisadi.

NOTE: Watu 20 wametoka nchi 8 tu

Hao wengine yawezekana ni kweli wanapesa zaidi yake lakini labda hawalipi kodi au shughuli zao ni za utata utata
 
kweli mr Reginald Abraham Mengi ni mfano wa kuigwa kwa wafanyabiashara wazalendo anajitoa sana
 
Huyu mzanzibari kisomo chake duni ingawa ana pesa kwa hiyo influence yake haijulikani kwani hakutani na matajiri wenzie wa Africa kwenye vikao vya biashara.

Naafikiana na ulichozungumza, ila tone uliyotumia "Huyu mzanzibari kisomo chake duni....." haipendezi. Nisingependa hili lipite hivihivi tu bila kugusiwa. Kutokwenda kwake shule hakupaswi kuambatanishwa na Uzanzibari wake, haipendezi. Huyu ni kama Mengi, ni watu safi wenye utajisri usioambatana na ufisadi na michango yao kwa Taifa haina mfano, kwa hiyo tunapowazungumzia tuwazungumzie kwa heshima. Tufike mahali tukue na tuwe na uzalendo na tujifunze kupenda vyetu hasa vilivyo vizuri na ikiwezekana tuvulinde badala ya kuvikejeli kwa lugha za kihunihuni tu. JF inasomwa na watu wa aina mbalimbali nikimaanisha dini, makabila, umri, gender, racial, elimu kwahiyo tuwe makini kidogo kwakuwa ubaguzi ni ubaguzi tu haufai hata chembe na tuupige vita kama UKOMA. Samahani kama nimekukosea lengo langu ni kuwekana sawa kwakuwa perceptions za wanaoandika na wanaosoma zinatofautiana.
 
Ndugu zangu watanzania tunabidi tujivunie maendeleo ya mtanzania mwenzetu Mr. R Mengi, list iliyotolewa na Forbes ya " The 20 most powerful people In African business man". Mr Mengi ni mtanzania aneyetutoa na kuipa Tanzania sifa nzuri, sio kila saa tunaongela habari za mafisadi.

NOTE: Watu 20 wametoka nchi 8 tu

Mimi ni kati ya watu wanaoamini kwamba 'gazeti la forbes huwa halifanyi utafiti wa kutosha' maana kwa miaka yote sikuwahi kumwona Mubarak na recently imegundulika ana utajiri unaomzidi Bill Gates, so where do 'big boyz' fall in its list?
 
wengine hawajatajwa maana biashara zao ni za kificho hawaziweki wazi kwa hiyo waandaa orodha hawakuweza kupata reliable information kuweza kuwajumuisha katika orodha.

naomba kuwasilisha
 
Article imesema most powerful people in african business siyo mambo ya hela. Ni mtu anavyokubalika kwa jamii kibiasharakwamba anafuata maadili. Kama unataka biashara yako ifanikiwe ndio unataka ushirikiano wake sasa hawa watu wenye asili ya kihindi au kiarabu maranyingi kwa wa Afrika wanaonekana tu watu wakutunyonya
 
Issue si kuwa katika orodha ya Forbes. Je chanzo cha utajiri wa Mengi kinajulikana? Je yale mabilioni aliyokuwa akidaiwa NBC iliyouawa na shemeji yake Mkapa alilipa au ndiyo huo ukwasi wenye kutia shaka?

Malipo ya wafanyakazi wa Mengi siku zote ni kwa mbango. Au yale yale ya Rostamali alivyokuwa akifanya kabla ya kurejesha namba?
Mkuu elewa hiyo siyo list ya The Richest People bali The Most Powerful People
 
Back
Top Bottom