Mengi anguruma mkutano wa Madola

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
Mengi anguruma mkutano wa Madola

Na Jesse Kwayu

30th November 2009

email.png

B-pepe

printer.png

Chapa

comment_bubble.png

Maoni

Mengi1%285%29.jpg

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi.

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, amesema kwamba sekta binafsi ina nafasi kubwa katika kukuza ajira, kushiriki katika vita dhidi ya ufisadi pamoja na kulinda mazingira.
Akizungumza mjini hapa mwishoni mwa wiki katika mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Madola, Mengi pia alisema nguvu za pamoja kati ya serikali na sekta binafsi ndizo zinaweza kusaidia kuleta mabadiliko ya kweli.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini hapa, Mengi pia alisema tatizo kubwa la kutokuendelea kwa Waafrika si umaskini wa kukosekana kwa rasilimali ila fikra zao ambazo alitaka zibadilike.
Alisema kinachotokea kwa Bara la Afrika kwa sasa ni umaskini unaotokana na watu wake kuwa watumwa wa fikra na ili waondokane na hali hiyo na kuweza kutumia rasilimali zao vizuri, ni lazima kwanza wajikomboe kifikra.
Alisema hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa kama mtu hajajikomboa kifikra.
Alisema mdororo wa kiuchumi duniani unaweza kutumiwa na nchi za Afrika na zile zinazoendelea kwa ujumla kubadili hali zao kwa kuongeza thamani kwenye mazao yao ambayo miaka na miaka wamekuwa wanauza kama mali ghafi kwa mataifa yaliyoendelea. Alisema kitendo cha kuuza mali ghafi kwa mataifa ya magharibi ni sawa na kuwa wafadhili kwa mataifa hayo. Alitaka hali hiyo ibadilike.
Mengi alisema rushwa, maarufu kama ufisadi, ni adui mkubwa wa maendeleo ya uchumi na ni lazima vita dhidi yake ihusishe sekta binafsi na serikali kwa pamoja.
Alitaka sekta binafsi ijikite katika kukuza ajira, kupambana na ufisadi pamoja na kukuza ujuzi wa wananchi ili nchi ifanikiwe kujinasua kutoka kwenye mdororo wa uchumi.
Mengi alikuwa mmoja wa wafanyabiashara maarufu kutoka Jumuiya ya Madola aliyepata fursa ya kuzungumza katika mkutano wa Baraza la Biashara la nchi hizo.

CHANZO: NIPASHE
 
sijaona NGURUMO HAPO!
pole sana MSHABIKI wa HUYU MZEE!..............
 
sijaona NGURUMO HAPO!
pole sana MSHABIKI wa HUYU MZEE!..............
mimi sio mshabiki wake wala sio mimi nilieandika hii taarifa nime copy na ku paste tu mkuu usimind ila hapo nadhani sio kwamba kaongea pumba.pole kama imekuUma
 
mimi sio mshabiki wake wala sio mimi nilieandika hii taarifa nime copy na ku paste tu mkuu usimind ila hapo nadhani sio kwamba kaongea pumba
you guys need to digest some stuff b4 you cut and paste!HELL!
ngurumo?au kuuza magazeti?hamna jipya humo....
 
Hey guys!!!

Are we discussing Mengi or as to whether what he have said amounts to Ngurumo?
 
you guys need to digest some stuff b4 you cut and paste!HELL!
ngurumo?au kuuza magazeti?hamna jipya humo....
Alisema kitendo cha kuuza mali ghafi kwa mataifa ya magharibi ni sawa na kuwa wafadhili kwa mataifa hayo. Alitaka hali hiyo ibadilike.
Mengi alisema rushwa, maarufu kama ufisadi, ni adui mkubwa wa maendeleo ya uchumi na ni lazima vita dhidi yake ihusishe sekta binafsi na serikali kwa pamoja.
Alitaka sekta binafsi ijikite katika kukuza ajira, kupambana na ufisadi pamoja na kukuza ujuzi wa wananchi ili nchi ifanikiwe kujinasua kutoka kwenye mdororo wa uchumi.

this is not new but its make sense. even if you hate him dont hate his positive views...are you RA supporter??
 
you guys need to digest some stuff b4 you cut and paste!HELL!
ngurumo?au kuuza magazeti?hamna jipya humo....

Huyu Mzee anakubalika hata kwenye anga za kimataifa, mpe heshima yake bana. Mbona mna wivu wa kike???? Huoni ni fahari mtanzania mwezio kupewa heshima ya kuhutubia katika baraza hilo. Au kwa vile hujamwona huko RA?
 
Comrade...!

You know whom you are talking to?

That was just piece of his mind!...huh!
 
Mengi anguruma mkutano wa Madola

Alisema kitendo cha kuuza mali ghafi kwa mataifa ya magharibi ni sawa na kuwa wafadhili kwa mataifa hayo. Alitaka hali hiyo ibadilike.
Kila siku nasikia huu msemo....Rais, wabunge mawaziri, haya tena na wafayabiashara wakubwa!! swali je nn kinashindikana katika ili? sera zetu? uwezo mdogo? au nn??
 
Kuna audio ya spichi yake? labda wakati anaongea alikuwa anaunguruma kama simba.

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=9ZuoOFBEIus"]Aunguruma[/ame]
 
mbona mnamtosa mtena mzee wa watu........unaamua kumpublish afu unaulizwa unakimbia hoja..............ni majungu?
mimi sio mshabiki wake wala sio mimi nilieandika hii taarifa nime copy na ku paste tu mkuu usimind ila hapo nadhani sio kwamba kaongea pumba.pole kama imekuUma
 
Huyu jamaa hata simkubali hata aseme nini mie naona pumba tu! Huyu jamaa isingekuwa katoka katika koo za kichifu angekuwa Ngumbaru wa ajabu! Ashukuru Mungu sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom