Mengi adai Polisi wahusika kutaka kumbambikizia mwanae madawa!

I have no comment nasubiria nisikie statement kutoka jeshi la polisi na wao watasemaje especially i wanna hear from SAID MWEMA, yaani kama ni movie basi ndio imeanza halafu movie yenyewe ina PART 1 hadi PART 4
 
Bwana Mengi nakupa pole sana kwa hayo yaliyokukuta.
Kwa mtazamo mpana mimi naona ni dalili chache tu za serikali iliyokosa uwajibikaji na strick adherence to codes of conduct.
Nimeanza kuhisi wafanyakazi wa serikali na taasisi nyeti za serikali kujichukulia majukumu mikononi mwao wenyewe na kufanya yale yasiyopasa kwa sababu imekosekana ile SAUTI kali ya karipio kutoka kwa mkuu wa nchi, sub-ordinates wake all the way down!

Matokeo yake, nchi yetu inaendelea kuwa horera!

Mengi ndoa yako na CCM ina walakini, ulitakiwa kugundua toka mwanzo kuwa CCM ni genge, jifunze chukua hatua na pole pia!

Wewe una uwezo, sijui kama angekuwa ni mtu mwingine mnyonge ingekuaje. Pengine kuna wengi tu tumeambiwa walikuwa na madawa but in reality walibambikiwa!

Mwananchi, muda wa kubadili madudu haya ni mwishoni mwa mwezi huu!
 
Pole sana Mengi, lakini ndo kawaida ya hawa watendaji wetu
Jiulize umekwakosea nini hasa kipindi hiki cha uchaguzi?

Maana hii nimakusudi tu!
 
Going Forward, IGP haraka sana awasimamishe kazi au kuwahamisha hao polisi hapo uwanja wa ndege huku uchunguzi wa ndani ukiendelea. Ikibainika walichukua rushwa sheria ichukue mkondo wake kama mfano kwa Polisi wengine.

Hii ni aibu kwa taifa, pale 'usalama wa raia' wanapohusika na kashfa nzito kama hii.

IGP Mwema, hii ni nafasi ya kufuta doa jingine ndani ya jeshi lako la Polisi.
 
mengi did the ryt thing....watanzania tukubaliane nae na tumsupport kwa hili....amna mwenye ujasiri wa kuwataja mafisadi
 
Hivi kama watu wa system wameshanunuliwa, wewe unafikiri haki utaipata kirahisi hivyo? Wacha tuu afanye alivyofanya , hakuna wa kumuamini kwa sasa..
 
ndugu zangu

Hilo suala kama liko kwenye vyombo vya dola tuache vifanye kazi zao kama inavyotakiwa kufuatana na sheria za nchi tulizo nazo kama amefanya kosa pia wacha vyombo vifanye kazi zake

Liko kwenye vyombo gani vya dola?, ndo kawaambia waende, umeshasikia wameenda?. Kwa hiyo ndg Shy hakuna tatizo kuliongelea hili swala kwa sheria yoyote..
 
Kama umefuatilia taarifa ya bw Mengi juu ya njama za kumhujumu, kupitia mtoto wake, utagundua kuwa ule mpambano kati ya Mafisadi papa na Mengi umechukua sura mpya.

Anyway, mi nilichojifunza ni kuwa huu mtandao wa Tanzania-Mafia (mafisadi papa), una nguvu kubwa hapa nchini (kama nilivyowahi kueleza), na ndio unaoendesha dola. Wana uwezo wa kumfanyia mtu chochote, kwani kama walipanga kutumia Bilioni 3 kumhujumu Mengi kupitia kwa mtoto wake, na kama waliweza kuwanunua watu wakubwa katika vitengo vya polisi na madawa ya kulevya, then hawa sio watu wa kawaida na ni hatari kwa taifa letu. Kwa upande mwingine, Mengi ameendelea kudhihirisha kuwa naye ni maji marefu, na kuwa ana 'usalama wa taifa' wake ambao bila shaka ni mahiri kuliko huu usalama wa taifa wa nchi.

Swali moja ni kuwa, wapambanapo hawa wakubwa, anayeumia ni nani?
 
Going Forward, IGP haraka sana awasimamishe kazi au kuwahamisha hao polisi hapo uwanja wa ndege huku uchunguzi wa ndani ukiendelea. Ikibainika walichukua rushwa sheria ichukue mkondo wake kama mfano kwa Polisi wengine.

Hii ni aibu kwa taifa, pale 'usalama wa raia' wanapohusika na kashfa nzito kama hii.

IGP Mwema, hii ni nafasi ya kufuta doa jingine ndani ya jeshi lako la Polisi.

IGP mwenyewe awajibike hii ni kashfa kwake na kwa jeshi zima la police. Hivi vyombo vyote vya usalama lazima vifumuliwe navyo baada ya uchaguzi.
 
Kama umefuatilia taarifa ya bw Mengi juu ya njama za kumhujumu, kupitia mtoto wake, utagundua kuwa ule mpambano kati ya Mafisadi papa na Mengi umechukua sura mpya.

Anyway, mi nilichojifunza ni kuwa huu mtandao wa Tanzania-Mafia (mafisadi papa), una nguvu kubwa hapa nchini (kama nilivyowahi kueleza), na ndio unaoendesha dola. Wana uwezo wa kumfanyia mtu chochote, kwani kama walipanga kutumia Bilioni 3 kumhujumu Mengi kupitia kwa mtoto wake, na kama waliweza kuwanunua watu wakubwa katika vitengo vya polisi na madawa ya kulevya, then hawa sio watu wa kawaida na ni hatari kwa taifa letu. Kwa upande mwingine, Mengi ameendelea kudhihirisha kuwa naye ni maji marefu, na kuwa ana 'usalama wa taifa' wake ambao bila shaka ni mahiri kuliko huu usalama wa taifa wa nchi.

Swali moja ni kuwa, wapambanapo hawa wakubwa, anayeumia ni nani?

Kikwete kwa kuwakumbatia mafisadi waasia na waarabu
 
Mkuu tunashukuru saana kwa hii clip maana wengine tulimiss taarifa ya habari lakini hata hivyo simulizi za watu waliyoiona haina tofauti na ya kwako kwahiyo post yangu itaendelea kusimama km ilivyo ila kuna maswali ya ziada;
1. Hao watu walijuaje km mtoto wa Mengi atasafiri?
2. Inamaana hii ndiyo safari yake ya kwanza?
3. Kwanini leo na si siku nyingine anazosafiri?
4. Mengi anazungumza kwenye taarifa yake kuanzia siku ya tarehe 25/sept namna gari lilivyopaki, je na yeye alikuwa anawinda au wanawindana? Hapa kuna tatizo kati ya hawa watu wawili.
5. Mengi anashindwa nini kuchukua hatua na kukimbilia kwenye vyombo vya habari? Km ameshawahi kushinda kesi kadhaa kupitia mahakama zetu kwanini asiende huko akaliseme na hili?
6. Anatamka kuwa kuna mtu hufanya malipo na ilibidi arudi kufanya hayo malio, je anawezaje kutoa ushahidi wa kiasi cha fedha km huyo mtu na yeye ni mtuhumiwa?

Mkuu, I apeal to your sense of reason.
Uliyoyaandika hayana logic au common sense.
1 Wanajuaje mtoto wa Mengi anasafairi-Mkuu unatoka Sikonge nini ambako mtu anadandia gari usiku usiku bila kuaga majirani?Have you ever heard of booking?Hiyo ni information tosha
2 Ina maana ndio safari yake ya kwanza-mbona hueleweki hapa, waongea kama umetoka usingizini
3 Kwa nini leo si siku nyingine-kwa makakati uliowekwa na hali yenyewe ya nchi, this might have been an appropriate time ya kumfix Mengi
4 Kuanzia tarehe 25/9/2010 mengi anapata hizi taarifa , anawinda na kuwindwa?-Mkuu nona hapa ndio unonyesha ujuha wako wa kutoelewa mambo.Ni dhahiri Mengi siyo korokoroni hiyo hii info amepatiwa.Amepatiwa na nani is not theissue hapa ila mipango yote imekuwa recorded.Na Mengi hakukurupuka kuongea.Try to be analytical.
5 Mengi kwenda mahakamani-kesi ya nyani umepelekee ngedere, come on!!!! The case would have never seen the daylight!Mahakama kubwa ni hii ya wananchi
6 Kwa mahali hapa naona mkuu kama wewe aidha hauko hii bongo au hao mafisadi wanaiendesha nchi hii kwa remote control hujawahi kuwasikia, kwa hili nakupa pole tu , you are beyond salvage.

Hata hivyo ni vema Polisi wakaliweka hili jambo bayana kabla wananchi hawajakosa imani.
 
Kama umefuatilia taarifa ya bw Mengi juu ya njama za kumhujumu, kupitia mtoto wake, utagundua kuwa ule mpambano kati ya Mafisadi papa na Mengi umechukua sura mpya.

Anyway, mi nilichojifunza ni kuwa huu mtandao wa Tanzania-Mafia (mafisadi papa), una nguvu kubwa hapa nchini (kama nilivyowahi kueleza), na ndio unaoendesha dola. Wana uwezo wa kumfanyia mtu chochote, kwani kama walipanga kutumia Bilioni 3 kumhujumu Mengi kupitia kwa mtoto wake, na kama waliweza kuwanunua watu wakubwa katika vitengo vya polisi na madawa ya kulevya, then hawa sio watu wa kawaida na ni hatari kwa taifa letu. Kwa upande mwingine, Mengi ameendelea kudhihirisha kuwa naye ni maji marefu, na kuwa ana 'usalama wa taifa' wake ambao bila shaka ni mahiri kuliko huu usalama wa taifa wa nchi.

Swali moja ni kuwa, wapambanapo hawa wakubwa, anayeumia ni nani?[/QUOTE]

zitaumia mahakama kuu kwa kusikiliza kesi zisizokwisha. Tutaambiwa mahakama imetumia sh.300 milioni kwa kuendesha kesi ya hao wakubwa then baadae tutaambiwa wameamua kumalizana nje ya mahakama!!!
 
Kama umefuatilia taarifa ya bw Mengi juu ya njama za kumhujumu, kupitia mtoto wake, utagundua kuwa ule mpambano kati ya Mafisadi papa na Mengi umechukua sura mpya.

Anyway, mi nilichojifunza ni kuwa huu mtandao wa Tanzania-Mafia (mafisadi papa), una nguvu kubwa hapa nchini (kama nilivyowahi kueleza), na ndio unaoendesha dola. Wana uwezo wa kumfanyia mtu chochote, kwani kama walipanga kutumia Bilioni 3 kumhujumu Mengi kupitia kwa mtoto wake, na kama waliweza kuwanunua watu wakubwa katika vitengo vya polisi na madawa ya kulevya, then hawa sio watu wa kawaida na ni hatari kwa taifa letu. Kwa upande mwingine, Mengi ameendelea kudhihirisha kuwa naye ni maji marefu, na kuwa ana 'usalama wa taifa' wake ambao bila shaka ni mahiri kuliko huu usalama wa taifa wa nchi.

Swali moja ni kuwa, wapambanapo hawa wakubwa, anayeumia ni nani?
Anyeumia of course ni Mtanzania wa kawaida...

Kama hawa jamaa wanaweza kujifanyia kila wanachotaka, basi destiny yetu inaamuliwa na hao watu!...!

Nawashangaa wachangiaji wenzetu hapa ambao hawaumizwi na mbinu za hawa mafisadi waasia na waarabu kuwanunua hadi watendaji wa juu kabisa kwenye serikali yetu!...Ni jambo baya sana na la kusikitisha!

Huo uthubutu wa Mengi tu ni jambo kubwa sana...Kwanini tusianze kwa kutambua hilo?
In any way, mimi namu'admire sana Mzee Mengi, maana ndiye MWANAUME peke yake Tanzania hii anayeweza kuwajuza watanzania juu ya nguvu ya hawa wageni, hasa watumiapo fedha kutuibiaa, kutuhujumu kutoka kila angle, na kutufanya tuendelee kuwaabudu kila iitwayo siku!!

Long Live Mzee!
 
Jeshi la polisi kwa ujumla lina matatizo makubwa sana na linahitaji kufutwa
 
Vyombo vyetu vya sheria vina matatizo sana, hilo halina ubishi..Lakini Mengi yumo ndani ya genge la mafisadi pia, sio malaika kama anavyotaka kuonekana kutumia vyombo vyake vya habari...
Reginald Mengi – feted by Mwinyi, snubbed by Mkapa, he is now preoccupied with blackmailing JK for a chair in his kitchen cabinet. Narcissistic to the core, he plays Kingmaker, taking the responsibility for the misfortunes of the recently fallen politicians and basking in the public undressing of Mkapa, which he is engineering using his media. Mr. Mengi holds court at his house to plot the unfolding of political events like an old Spartan general. Why? To prove masculinity and enhance an appearance that he is bigger, more important and richer than he actually is.[/
source: Political crisis in Tanzania?? « Tarishi Hauwawi
 
vyote ulivyonavyo si mali yako umepewa na mungu na vitumie kwa kumuenzi yeye daima,radio,tv,magazeti,ulikuwa kimya mzee hadi jana ulipowakumbusha watz story ya mafisadi papa na uharamia wao,karibu mzee mengi tena kwenye uwanja wetu wa mapambano kuelekea uhuru wa kweli wa watz,usigeuke nyuma kwani utakuwa jiwe la chumvi,tumevipiga vita vilivyo vizuri,mwendo tunakaribia kuumaliza huku tukilinda imani kwa watz,pamoja tutashinda
 
pole sana mzee mengi ila haya ni mapito na mungu alikuwa nawe na ndio maana mafisadi wanaendelea kushindwa na mungu wetu mwenye nguvu anawaumbua mchana kweupe.halafu leo hii mtu anasimama mbele ya umati wa watanzania masikini wanyonge anamnadi fisadi kwamba anafaa ashindwe katika jina la yesu hatufai kabisa wala hatumwihitaji tena .hii inaonyesha ni kwa jinsi gani hata chama tawala kitakavyotumia mabavu kuiba kura hili limetudhihirishia wazi kabisa hata ile issue ya KIJANA WETU JERRY MURO ALIBAMBIKIZWA MAFISADI MUOGOPENI MUNGU MAANA IPO SIKU MTATAKA KUFANYA HAYA NA HAMTAWEZA TENA .KIKWETE KAZI KWAKO SASA NA SERIKALI YAKO YA MAFISADI
 
Mmiliki wa IPP Ndugu Reginal Mengi amwalipua maafisa kadhaa wa vyeo vya juu kwa kupokea mulungula ili kumbambikiza mwanae madawa ya kulevya na alikuwa asafiri kwenda India tarehe 26/9/2010.

Maafisa hao wa vyeo vikubwa amesema wamelipwa na "tajiri" mwenye ofisi Nyerere Rd na wote waliahidiwa $40,000 kila mmoja na wamekwisha pokea nusu ya kiasi hicho ($20,000) kila mmoja.

Maafisa hao ni Zonal Crimes OfficerNd Mkumbo, Ofisa wa kuzuia mihadhatrati, Nd Nzowa na ofisa mmoja wa Interpol.

Vile vile kuna vijana wa kampunu moja ya simu na wengine pale DSM Airport waliopewa kila mmoja Tshs 15 mil.

Hii taarifa ni kadri ya HABARI za saa mbili jioni leo 12/10/2010.

Mengi amwaomba hawa maofisa wajiuzulu na amewachallenge wamfungulie mashtaka ya kuwa chafua majina yao.

Sasa wananchi lazima watajiuliza hivi majambazi wakubwa wako upande gani? na imani yetu kwa polisi baada ya sakata la Zombe itakuwa wapi?

wapendwa katika bwana Hizi game ziko sana pale airport,,pole sana mengi nahisi MUNGU ulie nae usimwache best..at least umejua nchi ilivyo sasa...huyu kamanda nzowa wa madawa ya kulevya anahusika na upuuzi mwingi sana pale airport..labda kwa kifupi tu amekuwa akiwafukuza mapolisi engi sana wanaokuwa kimbelembele hasa pale mzigo wa mtu unapokuwa unasafarishwa kibaya zaidi anapenda kulaq mwenye sio unakkuta ameweka vijana wake 3 na mapolisi wenye sare wapendwa wanampokea nje wanamwingiza pale ndani wanakuwa wameshacheza game na wale jamaa wa machine pale kati na pale juu so ukifika mzigo wanaupitisha yaani yule mwenye mzigo anapita kama jakaya kikwete imagine hadi zile karatasi za IMMIGRATION polisi wa madawa ya kulevya wanawaandikia wakifika juu wanahakikisha ameingia last check point wakitoka nje kila polisi hana si chini ya million 1.5..ilikuwaje kuna sku mmoja wa mapolisi alipofika nje akupewa mgao aliotangaziwa nahisi wazee alikula cha juu kila mtu aliekuwepo hapo alisikia na yule kaka ilimchukua siku tatu tu kuendelea kuwepo maeneo ya airport..so haya mengi jamani kwanza nampa pole..unaweza kuona we kama umesingiziwa issue kubwa kam hi unamkibizia MUNGU ati mungu ndie anajua ...wewe NZOWA WEWE laana yako hii na MUNGU atakaudhibu ndugu yangu acha kumsingizia mungu jamani huyu mungu kila kitu mpaka lini???AIRPORT INANUKA WAPENDWA INANUKA KABISA NA SASA HIVI WALA AWAOGOPI UNAKUTA WANAAWAPOKEA PALE NJE NA KUINGIA NAO NDANI MPAKA WAMEFIKA JUU ...HUU CI UPUUZI..HUYU NZOWA AMEKULA HELA NYINGI SANA ZA MADAWA YA KULEVYA NA AUKIONA MTU KAKAMATWA BASI HUO MZIGO AJAKATIWA FUNGU..KUNA WAKOMORO FULAN WALIPITISHA BANGI PALE KAMA MNAKUMBUKA ILITOKEA GAZETINI WAKAKAMATWA WAKAPELEKWA PALE KURASINI ILIWACHUKUA WIKI 3 TU ILEMKESI IKAFILIA MBALI MPAKA LEO HII WANAPANDA NA KUSHUKA DAR WANAVYOTAKA ...NI MATATIZO MATUPU.....
 
Back
Top Bottom