Meneja wa Shoprite kizimbani kwa kuwafungia chumbani wafanyakazi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Meneja wa Shoprite kizimbani kwa kuwafungia chumbani wafanyakazi



RAIA wa Kizungu, ambaye ni Meneja Mkuu wa duka la kuuza bidhaa za kusindika maarufu kama Shoprite, amefikishwa kizimbani kwa tuhuma za kuwafungia katika chumba wafanyakazi wa duka hilo kinyume na sheria.
Mtuhumiwa huyo ni Fredrick Skein [33] ambaye alitokea nchini Afrika ya Kusini, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ya jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazomkabili.

Alisomewa shtaka lake katika Mahakamani hiyo na Inspekta Msaidizi wa Polisi, Denis Mujumba mbele ya Hakimu Janeth Kinyage wa Mahakama hiyo.

Mujumba alidai kuwa, mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 12, mwaka jana, katika duka hilo lililopo barabara ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa aliwafungia wafanyakazi hao katika chumba zaidi ya masaa kadhaa kwa sababu ambazo hazikuweza kuelezwa Mahakamani awali hadi kesi itakaposikilizwa.

Wafanyakazi waliofungiwa katika chumba hicho walikuwa watatu na walitambulika kwa jina la Anna Temu, Juma Said na Hassan Kassim.

Hakimu alimwambia mshitakiwa angeweza kuwa nje kwa dhamana kwa kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaoweza kusaini milioni moja kila mmoja na kuwasilisha hati zake za kusafiria mahakamani.

Hata hivyo mshitakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kuweza kuwa nje kwa dhamana, na kesi iliahirishwa hadi hapo Machi 3, mwaka huu, itakapotajwa tena.
 
Hawa wawekezaji wakiwa TZ wana kiburi sana, hii yote hutokana na kujua kuwa hawatafanywa kitu. Nakumbuka wale jamaa wa NIDA Textile walivyompiga mfanyakazi na kumfungia ndani wakisema kuwa alikuwa anaiba majora ya nguo, sijui kesi yake iliishia wapi alipowashitaki. Pia muwekezaji wa Speke Bay Lodge iliyoko karibu na Kijiji cha Mwabulugu, Mwanza. Aliwahi kufungia raia sababu tu walikuwa wanapita na mitumbwi yao eneo la ziwa mbele ya Hotel yake, sasa mpaka eneo la ziwa ni lake?. Hivi viburi vya wawekezaji kuna siku vitawatokea puani.
 
Hawa viongozi wetu wanatufanya kuwa watumwa mkuu mfumwa!!!
 
Hii ndio bongo bwana. Bunge lilikaa chini na kutunga sheria ya kuvutia wawekezaji. What do you expect? Hawa watakuwa wanalindwa mpaka siku tutakaposema basi.
 
asante wawekezaji kwa kuturudisha zama za mijeredi ya wakoloni.
mlipokuja kuomba nafasi ya kuwekeza mlikuja kwa heshima ,mikono uyenu ikiwa nyuma , na vichwa vimeinamishwa chini.
Leo mmetugeuka, mmetukalia vichwani, mwatubebesha mizigo mizito inayozisononesha akili zetu na kuudhalilisha utu wetu.
 
Nakumbuka kuna mmoja aliwatoa resi kamati ya bunge uko mbugani mpaka leo aijulikani alipewa adhabu gani
 
Back
Top Bottom