Meneja wa meli iliyozama Zanzibar akamatwa

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,591
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Omari Hassan Mnkhon ambaye ni Meneja wa boti ya Mv Skagit, kwa ajili ya mahojiano baada ya kubainika kwamba kumekuwa na kasoro za kumbukumbu katika taarifa za hiyo meli. Wakati Jeshi hilo likimshikilia meneja huyo, hadi jana jioni saa 10:30, vikosi vya uokoaji vilifanikiwa kupata maiti 63, huku 29 kati yao ikiwa imetambuliwa majina namba za tiketi na sehemu wanakotoka marehemu.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa meneja wa boti Mkoa wa Dar es Salaam, anashikiliwa ili kuweza kusaidia jeshi la polisi kupata taarifa za kina kuhusu za meli hiyo.

Kova alisema tukio hilo linagusa maeneo mengi ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam ambako safari za meli hiyo huanzia na kuongeza kwamba, wanamshikilia meneja huyo baada ya kukosekana taarifa muhimu juu ya safari za boti hiyo.

"Tunamshikilia meneja wa meneja hiyo ili atusaidie kutupa taarifa za kina, kwani tukio hilo sio dogo na uchunguzi wa kina unatakiwa kufanywa," alisema Kova na kuongeza;

"Jeshi la polisi litafanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka zinazohusika, ili kujua chanzo cha ajali pamoja na kupata taarifa za kina za boti hiyo tangu ilipoanza safari yake," alisema.
 
Walioisajiri ikiwa na viwango duni nao wamekamatwa?

Wale wa hali ya hewa (sijui ndo TMA) nao wamekamatwa?

Wahusika wa bandarini walioiruhusu iondoke huku ime-overload nao vipi?
 
Kila siku tutaishia kusolve matokea ya majanga badala ya ku'concetrate kwenye kuzuia majanga.
Nadhani watu weusi tuna matatizo katika vichwa vyetu sio bure.
 
Lengo ni kumuwahisha mahakamani fasta halafu mjadala utakuwa umefungwa! Kama kawaida, jibu rahisi litakuwa "kesi iko mahakamani ...". Tega sikio.
 
Kwa nini wasianze kwanza kumkamata OCD wa kile kituo cha polisi waliokiri kupata taarifa mapema kabisa kwamba kuna meli inazama ila hawakufika eneo la tukio kwa kuwa ''hawakuwa na mafuta''?. Huenda pia hawana simu ya mezani
 
... Ni nchi ya watu walopewa vichwa ili kufugia nywele, kuweka wave, rasta, curl, etc.
 
Kabla ya kumkamata manager wa meli, nilitegemea Waziri wa uchukuzi Zanzibar na mkuu wa mamlaka ya usafiri majini Zanzibar wawe rumande. Manager wa meli ni mtu wa mbali sana kwenye huu mkasa. Wale walioruhusu meli 'chakavu' kusajiliwa na kupewa kibali cha kubeba watu huku wakijua ni haifai ndio wanatakiwa wawe wa kwanza kuingia mikononi mwa vyombo vya sheria.
 
Mkuu ukisikia changa la macho ndio hili...Hili sakata litazimwa kimya kimya kama la mwanzo.
 
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Omari Hassan Mnkhon ambaye ni Meneja wa boti ya Mv Skagit, kwa ajili ya mahojiano baada ya kubainika kwamba kumekuwa na kasoro za kumbukumbu katika taarifa za hiyo meli. Wakati Jeshi hilo likimshikilia meneja huyo, hadi jana jioni saa 10:30, vikosi vya uokoaji vilifanikiwa kupata maiti 63, huku 29 kati yao ikiwa imetambuliwa majina namba za tiketi na sehemu wanakotoka marehemu.

Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa meneja wa boti Mkoa wa Dar es Salaam, anashikiliwa ili kuweza kusaidia jeshi la polisi kupata taarifa za kina kuhusu za meli hiyo.

Kova alisema tukio hilo linagusa maeneo mengi ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam ambako safari za meli hiyo huanzia na kuongeza kwamba, wanamshikilia meneja huyo baada ya kukosekana taarifa muhimu juu ya safari za boti hiyo.

“Tunamshikilia meneja wa meneja hiyo ili atusaidie kutupa taarifa za kina, kwani tukio hilo sio dogo na uchunguzi wa kina unatakiwa kufanywa,” alisema Kova na kuongeza;

“Jeshi la polisi litafanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka zinazohusika, ili kujua chanzo cha ajali pamoja na kupata taarifa za kina za boti hiyo tangu ilipoanza safari yake,” alisema.

Hata marehemu Jumanne Mwiru nahodha wa Mv Bukoba alikamatwa vile vile na mahakama ikamuona hana hatia kwa sababu kosa halikuwa kwa nahodha bali kwa serikali kutumia meli mbovu wakati ikiwa na taarifa ya kasor hizo toka kwa walioitengeneza (Ubelgiji), na katika hili serikali haikwepi lawama, ningeona jambo la maana kama ukamataji ungeanzia SUMATRA, TBS na WAZIRI Mwenye dhamana ya uchukuzi angekuwa mshitakiwa namba moja , tumeambiwa meli ni mbovu toka inanunuliwa kama ni kweli iliingiaje TZA kuja kutafuna maisha ya watz? Halafu movie za Kova nimekianai kuziangalia wala kuzisikiliza zote hazina actor/actress wazuri
 
Walioisajiri ikiwa na viwango duni nao wamekamatwa?

Wale wa hali ya hewa (sijui ndo TMA) nao wamekamatwa?

Wahusika wa bandarini walioiruhusu iondoke huku ime-overload nao vipi?
Huyu ni bangusilo tu maana kama una gari lako limesajiliwa kihalali, limepita safety na lina liseni zote za kazi ikitokea ajali sidhani kama mwenye mali atakuwa na makosa..Hizo records mnazitaka leo baada ya maafa?..mnatafuta ushahidi ulokwisha potezwa ndio iwe sababu.
Wanaotakiwa kukamatwa ni hawa walioiruhusu meli hiyo ifanye kazi..
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom