Meneja atupwa jela miaka 250 - Mfano wa Kuigwa

Tatu

JF-Expert Member
Oct 6, 2006
1,100
313
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi mkoani Kagera, imemhukumu Meneja wa Shirika la Posta tawi la Biharamulo mkoani Kagera, Claud Masali (52), kifungo cha miaka 250 baada ya kupatikana na makosa 50.

Hukumu hiyo iliyosomwa kwa zaidi ya saa tatu na kuvuta hisia za wengi, ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Kagera, Wilbard Mashauri, baada ya kuridhika na upande wa mashitaka kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Mtuhumiwa huyo alidaiwa kuwa wakati akiwa kazini katika tawi hilo, kwa nafasi yake, alisababisha hasara ya sh milioni 25.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Mkaguzi wa Polisi, Jumanne Ibrahim na Mrakibu wa Polisi, Obeid Mhandi, walidai mahakamani hapo kuwa mkuu huyo wa Posta, alitenda kosa hilo Septemba 11, mwaka 2004 kwa nyakati tofauti, akiwa mtumishi wa shirika hilo.

Walitaja baadhi ya makosa hayo kuwa ni pamoja na kuingiza mahesabu ya uongo kwenye vitabu vya mahesabu, kughushi na kuiba fedha za shirika kwa kuongeza sifuri mbele pindi mteja alipotumiwa fedha ‘Money Fax’.

Walidai kuwa mkuu huyo bila kujali, alitumia wadhifa wake kuliibia shirika lake ambapo kwa kila mteja aliyetumiwa fedha, alikuwa akilazimika kuongeza sifuri mbele na kuonekana ni zaidi, na kiasi kilichokuwa kikibaki, alikuwa akichukua yeye na kuingiza mfukoni mwake.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, kati ya makosa hayo 50, atatumikia kifungo cha miaka mitano kwa kila kosa, hivyo kulazimika kutumikia kifungo cha miaka 250 jela, lakini adhabu hizo zitakwenda pamoja.

Awali kabla ya kusomewa hukumu hiyo, mtuhumiwa huyo ambaye ni mkazi wa wilayani Misungwi mkoani Mwanza, anadaiwa kuruka dhamana baada ya kuona mwelekeo wa kesi yake unaenda vibaya.

Hata hivyo, alikamatwa Aprili 9 mwaka huu jijini Mwanza, akiwa amejificha na tangu wakati huo alikuwa rumande hadi jana alipohukumiwa kifungo cha miaka 250 jela.

Source: Tanzania Daima

Nafikiri huu ni mfano wa kuigwa na Mahakama zote Tanzania. Ufisadi utapungua kama mahakama na waendesha mashitaka watafanya kazi zao kwa uadilifu.
 
This is it!! Hii kiboko hata kama atatoka kwa rufaa lakini cha mtema kuni kakiona na walio na tabia kama hiyo wapunguza wizi na ufisadi.

Huyo hakimu alitakiwa aongezewe cheo ili awakomeshe wengi zaidi.
 
Kwa hiyo effectively kwa vile 'adhabu zinakwenda pamoja' atatumikia miaka 5 jela ama sio?

Huyo hakimu wamlete Kisutu sasa ahangaike na wajamaa wa EPA
 
Yes good job.....but ....mmmmh! 25mil...stolen punished with 250 years in jail.......! Billions of money lost through EPA,Twin towers, meremeta, TANGOLD.......watu wanakula bata tu mitaani...hii imekaaje?
 
Huyo jaji apewe kesi za wezi wa EPA na ujenzi wa towers za BOT.

Mil 25 = 250 years, I.e 1mil =10 years
40 bil (Kagoda EPA) = How many years?
200 bil (BOT towers) = How many years?
 
mnh, hapa mzee wa red cars si itakua mvua ya elnino?
 
this is stupid

sasa huyo jaji anataka kuprove nini?

Soma habari yote ndugu yangu.

Kifungo cha kutumikia ni miaka 50 tu.

Jaji anafanya kazi yake. Angemfunga mwaka 1 ingekuwa makelele, miaka 50 makelele, sasa watu mnataka nini?

Sheria lazima ifuate mkondo wake. Kila meneja anayefanya huu mchezo pamoja na wapambe wao wakipata mvua za aina hii, nchi itaanza kubadilika.
 
actually mahakimu wanayo nafasi kubwa katika mambo mengi sana ila problem ni kwamba are they reasonable enough! 52 year then 250 years in jail will it work that way! Jaman me kilio changu ni wale jamaa wa samaki za Mh. Magufuli upelelezi bado! Hawa mahakimu vipiiiiiiiiii! i wish to hear from them!
 
Sina interest na huyu maana watuhumiwa wa aina hii ni wengi lakini nataka kujua wakina Jitu Patel, Mramba,Yona, and the like watapewa kifungo kiasi gani?! hii itathibitisha jinsi mahakama zilivyo siriasi na mafisadi.
Sio huyu aliyechota mil anatangazwa saaaaaaaaaana ili mahakama zionekane zinafanya kazi kumbe........
 
Huyo jaji apewe kesi za wezi wa EPA na ujenzi wa towers za BOT.

Mil 25 = 250 years, I.e 1mil =10 years
40 bil (Kagoda EPA) = How many years?
200 bil (BOT towers) = How many years?


Tufahamu kuwa hiyo miaka ni matokeo ya adhabu kwa kila count/kosa.
Makosa 50 counts x 5yrs= 250yrs. Na adhabu inatumikiwa kipindi kimoja
( concurrently) na sio baada ya kila kifungo ( consecutively)
Wanaosema huyo jaji/hakimu ni mjinga/ stupid hawaelewi the art of sentencing. Thats how it goes.
 
Kweli wewe umesema,kifungo hiki ni concurently hivyo kwa makosa yote atatumikia miaka mingapi sasa 5 au zaidi ya hapo?
 
Soma habari yote ndugu yangu.

Kifungo cha kutumikia ni miaka 50 tu.

Jaji anafanya kazi yake. Angemfunga mwaka 1 ingekuwa makelele, miaka 50 makelele, sasa watu mnataka nini?

Sheria lazima ifuate mkondo wake. Kila meneja anayefanya huu mchezo pamoja na wapambe wao wakipata mvua za aina hii, nchi itaanza kubadilika.

Ndugu...hata wewe umechanganya...kifungo atatumikia miaka 5 tu na siyo 50.
 
Back
Top Bottom