Membe, zoka, mwambene, mwanahalisi na kutekwa kwa dk. Ulimboka

Status
Not open for further replies.
membe si mbaya hata kidogo

ila uraisi wa nchi hapana, hawezi kuua hata mbu?

Hawezi fanya maamuzi hata ya ale kitumbua au andazi.

Yee abaki tu kupendezesha wizara wizara lakini uraisi tunataka mtu atakayefanya 'KAZI'

tumechoka wanamme wanaosifiwa kwa sura.

Acha kuunganisha vitu visivyo na mantiki hata kidogo fanya utafiti kwanza kama humpendi membe acha kazi wizara hiyo katafute kazi pengine
 
zoka hana ubavu wa kumpa mtu urais yeye mwenyewe kashachafuka vyakutosha na membe analijua hilo na hakuna mtu mwenye kuutaka urais akamtegemea zoka huyo atakuwa hajui analolifanya pili uteuzi wa mwambene ulifanyika hata kabla ya mwanahalisi kuanza kuandika habari hizo tatu zoka hawezi kumtumia membe kumpa mtu nafasi serikalini kumbuka tiss inauwezo wa kumpa mtu nafasi katika taasisi yoyote hapa nchini kama kachero wao mamlaka hayo wanayo na rais anayafaham na hana uwezo wakupingana nayo bado unayumba yumba kwa taarifa yako inayoonekana wazi niyakutunga na iliyokosa mashiko ''Naye Mwambene, licha ya kuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, ni mtu wa karibu sana na Membe. Infact, pale wizarani watu wakiwa wanamsema vibaya Membe halafu ghafla Mwambene akitokea, wote wananyamaza kimya!'' hii pekee inaonyesha unatumikia wizara ya mambo ya nje na humpendi waziri wako sipingani nawewe ila usilete habari za kuunga unga kwa lengo la kupunguza machungu yako. fanya kazi kujenga taifa lako.
 
membe si mbaya hata kidogo

ila uraisi wa nchi hapana, hawezi kuua hata mbu?

Hawezi fanya maamuzi hata ya ale kitumbua au andazi.

Yee abaki tu kupendezesha wizara wizara lakini uraisi tunataka mtu atakayefanya 'KAZI'

tumechoka wanamme wanaosifiwa kwa sura.

Sisemi membe anafaa kuwa rais wa nchi hii mwenyewe simuungi mkono lakini haifai kuishushia hadhi jf kwa kupokea habari yakuunga unga isiyo na mantiki kisa hatumpendi membe
 
Acha kuunganisha vitu visivyo na mantiki hata kidogo fanya utafiti kwanza kama humpendi membe acha kazi wizara hiyo katafute kazi pengine
Na wewe acha vitisho kwani kakwambia anafanya kazi wizara hiyo ????Wacha hizo habari tuzipate live, mwambie bosi wako bado tunaye!!!

 
Acha kuunganisha vitu visivyo na mantiki hata kidogo fanya utafiti kwanza kama humpendi membe acha kazi wizara hiyo katafute kazi pengine

Usizibe midomo ya watu, fungua wa kwako.
Yeye kasema hayo, nawe sema ya kwako! Kama hampendi Membe hiyo safi na hapo ndo sisi tunaona ni pazuri kupata taarifa ambazo wewe unayempenda utazificha.

Kafiribangi, hebu lete yote yanayomuhusu Membe.

Hata hivyo hatuoni kama Memmbe ni Presidential material. Tumechoka na watu wanaofikiri kwa taabu kama huyu tuliye naye. Milioni 45 tukose mwenye kichwa kilichojaa!
 
........nani? Membe? si afadhali na Kikwete apewe mingine kumi na wala sio huyu nyoka wa mdimu, tumechoka marais wanaocheka cheka sisi....
 
Kafiribangi yawezekana kabisa ukawa na mantiki lakini mistari uliyounga siwez kuikonekti

vijana wa ZOKA walifuta uzi wako
Membe alipanga na mkuu wa nchi wa mchukue MWAMBENE awe sijui nani
hapo hapo ZOKA, kausika kwa utekaji wa dr ULI na pia
MEMBE kamshawish baba ritz afungie mwnahalis

yawezekana kabisa ukawa una logic ila kwa jinsi ulivyo dondosha huu wino hapa ni ngumu kuleta mantiki.

kwa kidogo nilichoelewa mimi nasema hivi
Membe hafai kabisa kuwa raisi wa taifa hili, uhandsome is not an ishu bana tuletewe hata masudI sura mbaya kama atachapa kazi ss hatuna neno na hilo. hatuangalii utanashati wala tabasamu hayo anaangalia Lundenga ila watazania wanaangalia mwajibikaji, mwenye maadili, asiye na upendeleo, mwenye msisimamo na maamuzi magumu. 2015 CCM ikitaka iingie Ikulu Imrudishe Edward LOwassa nje na hapo hakuna kitu. miye hata NRA NITAIPIGIA.
 
Last edited by a moderator:
Acha kuunganisha vitu visivyo na mantiki hata kidogo fanya utafiti kwanza kama humpendi membe acha kazi wizara hiyo katafute kazi pengine

Wala siyo siri Mwambene naye ni TISS kama walivyowengi pale kwa Membe na JK anamwamini Membe sababu ya kumpatia habari za ndani toka kwa Zoka na atajitahidi kuendelea kumfurahisha ili 2015 aundiwe EPA nyingine. Si unaona alivyokuwa keshaanza kuunganisha na Libya ya Ghadaffi? Sasa watu wa Benghazi wakaingilia ikatibua mpango mzima kwa sasa nadhani wanaandaa labda haya ma Symbion ndo mpango wenyewe. Na Mwambene ndo TISS wenyewe wakipata wanamtonya Membe hata akiwa nje naye anabofya tu kwa mzee wa kaya na anaonekana shujaa. Tusubiri ya Syria ndani ya TZ kwa mtindo wao huu wa kupokonya wenzao madaraka.
 
Umaskini wa watanzania unasababishwa na watu kupenda kutumia mda wao mwingi vijiweni kupiga soga.jf nayo imegeuka kijiwe cha soga na kahawa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom