Membe, zoka, mwambene, mwanahalisi na kutekwa kwa dk. Ulimboka

Status
Not open for further replies.

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
​NILIANDIKA hapa jana juu ya mada hapa juu. Nilisema najua baadhi ya watu watakuwa wamepongeza uteuzi wa Mwambene kuwa mkurugenzi wa MAELEZO kwa kuzingatia kuwa ni kijana na labda ataleta mabadiliko fulani kwenye tasnia ya habari.

Lakini nataka nitoe angalizo dogo ili muweze kufahamu kinundani kilichosababisha Mwambene kuteuliwa na Rais Kikwete kushika nafasi hiyo.

Uteuzi wa Mwambene unatokana na ile habari ya Membe na ufungiwaji MwanaHalisi. Membe ndiyo kiini cha kufungiwa MwanaHalisi kwa sababu ya kulinda maslahi yake binafsi kwa ZOKA. Membe na Zoka ni pacha na kidole, na kwamba ndiyo tegemeo la Membe la kufikishwa Ikulu ndani ya Usalama wa taifa.

Mnakumbuka jinsi stori za kutekwa kwa Dk. Ulimboka zilivyokuwa zinamuingiza moja kwa moja ZOKA katika mpango mzima. Kwa kuona hivyo, Membe akaamua kutumia njia za panya ikiwa ni pamoja na kumshawishi mkuu wa nchi kuagiza MwanaHalisi kufungwa.

Naye Mwambene, licha ya kuwa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, ni mtu wa karibu sana na Membe. Infact, pale wizarani watu wakiwa wanamsema vibaya Membe halafu ghafla Mwambene akitokea, wote wananyamaza kimya! Uteuzi wake ni sehemu ya majadiliano aliyofanya Membe siku ile anajadiliana na JK kuhusu MwanaHalisi. Hii sehemu ya strategies zake kuelekea 2015. Kwa sisi tunaojua nini kinaendelea kwenye teuzi hizi, tunasema ngoja tusubiri tuone.....
 
Unapotafuta uongo atleast uwe na visugar coat kidogo ili umezeke. Membe na kufungiwa mwanahalisi hakuna connection yeyote kwakuwa Mwambene aliteuliwa zamani kabla hata mwanahalisi halijachapisha ile habari ya Ulimboka.
 
sawa tumesikia, tufanye nini sasa na Mh. Rais kashafanya uteuzi?
 
mwanahalisi lilisema zoka ni naibu mkurugenzi mkuu ana power kiasi gani kumfanya membe awe rais inahitaji maelezo mapana ili tukuelewe
 
wametajwa watu watano ambao hawaunganishwi mahali popote na taarifa iliyo mbele yetu au ndio mwanahalisi imetokea jf. huu si udaku tu bali ni udakuzi
 
mods watakuban milele unaona sasa unasema waliban hadi IP ili ushindwe kubadili jina lingine. adhabu hiyo ni kali utakuwa umeshindikana
 
Acha kuunganisha vitu visivyo na mantiki hata kidogo fanya utafiti kwanza kama humpendi membe acha kazi wizara hiyo katafute kazi pengine
 
Mmmmmmmmmmmmmmm,nchi hii.

Asante kwa taarifa,wengi watakupinga lakini...................................??
 
issssshhhh!, kwani kwenye menu yetu kuna CCM peke yake?

Come 2015, hata SAU itapigiwa kura.
 
Acha kuunganisha vitu visivyo na mantiki hata kidogo fanya utafiti kwanza kama humpendi membe acha kazi wizara hiyo katafute kazi pengine
Vipi kaka? Mbona umetumia kauli kali hivyo? au inakuhusu moja kwa moja. kama una maoni tofauti naomba uyashushe hapa jamvini.
 
Acha kuunganisha vitu visivyo na mantiki hata kidogo fanya utafiti kwanza kama humpendi membe acha kazi wizara hiyo katafute kazi pengine

Tatizo lake sio Membe ni kukua kwa Mwambene wakati yeye anaishia ukarani.
 
Bange mbaya sana,jamaa ameitwika ya gizani imemchanganya ameamua kuja kumalizia malue lue yake hapa jukwaani,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom