Membe Ubalozi karibia utafungwa kule Brussels

Kimbembe

Senior Member
May 14, 2006
122
15
Ndugu Membe nimetokea ubalozini muda huu kutafuta huduma basi sijakuta mkubwa yeyote wako wadogo tu pale ndani ambao hata majibu ya maswali yangu hawakuwa nayo na nimeondoka bila ya kuhudumiwa .Wote wana tetemeka hawana heating system katika jengo wiki nzima hii .Inasemekana wanaweza kufunga Ubalozi next kwa siku zile za kazi kisa baridi ndani ya jengo .Je ni pesa hakuna ? Au kubomoka kwa system hakuwezi kutengenezwa kwa uharaka kwa maana ya kujali afya za watu na hii ni winter ?Mkulo alikuwa hapa kaondoka jana toka kwenye kikao cha Mawaziri hajakueleza ama aliishia hotelini bila ya kufika ubalozini ?
Hiyo ndiyo habari hapa ubalozini .
 
Kila siku wako Ulaya na America; inaelekea wakiwa huko hawafiki ubalozini wanaishia mahotelini tu na ndio maana wakina Karamagi wanasign mikataba nje ya ubalozi!! Inaelekea hawa wanamtandao na Seikali yao kila mtu kivyakevyake tu; hawana common vision.Lumbanga si ndio yuko huko Brussels, inakuwaje balozi yupo lakini ubalozi unakosa central heating system? Mrudisheni aje ajibu maswali ya EPA .
 
Bulesi
Brussels yuko Hon.Mlay , Nyani Ubalozi wetu wa Brussels ni strategic .Kuna EU mission hapa hapa Brussels na pia Balozi wa Ubelgiji anaenda hadi Holland na Luxembourg .Sasa naamini bado ni muhimu sana sana kwa kila kitu kuwepo .Noma ni heating system hadi inatishia kufunga Ubalozi .Nimempa Membe taarifa maana tukimpa sirini anakuwa haelewi .
 
Hiyo noma....halafu ubalozi wa Brusels unatusaidia nini sisi? Funga tu

We Nyani, unakujua Brussels ni wapi na umuhimu wake? Funga balozi zote Duniani lakini siyo kule.
Lakini inawezekana wafanyakazi wamekula hela yote kw imprest ya sikukuu. Haiwezekani hayo yatokee at the heart of Europe wakati kwingine huku kuko shwali.
 
ccm leaders; is a political party with no common sense and common vision. Who is denying the allegation????? No never
 
ccm leaders; is a political party with no common sense and common vision. Who is denying the allegation????? No never

Nakubaliana nawe maana CCM ukitaka kuijua basi mwangalia Makamba then utajua kwamba CCM ndiyo hivyo walivyo .Membe nadhani keshapata ujumbe kwamba wabakufa na baridi huko Brussels
 
ccm leaders; is a political party with no common sense and common vision. Who is denying the allegation????? No never

Mie sikubaliani nawe mpendwa Mshiiri;
CCM is a political party with a common sense as well as common vision.
Kuwepo kwa CCM madarakani kumekuwezesha kuwa kama ulivyo sasa hata kuweza kutumia kompyuta.
Kuwepo kwa CCM madarakani kumekuwezesha kuwa na amani uliyo nayo na uhuru ulionao sasa.
CCM ikianguka leo, wewe na wengineo mnaoiponda mtaikumbuka kama watani wetu wa jadi (Kenya) wanavyoikumbuka KANU, pia kama marafiki zetu Zambia wanapoikumbuka UNIP; Vile vile kama waZimbabwe wanavyo ikumbuka ZAPU-PF iliyokuwa ikiongozwa na Joshua Nkomo (RIP).
 
Nyani, wewe vipi tena? Ufunge ubalozi makau Makuu ya EU (Shirikisho la Ulaya)?????????? Mhhhhh, hebu uliza tena!!!

Ubalozi wa Tanzania pale Brussels hauna hadhi hiyo kama unavyofikiri. Kwanza huwezi kujua kama kuna ubalozi. Hakuna kiashiria chochote. Wenyeji wanaolizunguka jumba wala hawajui kama kuna ubalozi wa Tanzania eneo hilo. Hii ni kwa sababu ubalozi unamiliki floor moja tu kwenye nyumba ya ghorofa lenye wapangaji wengi. Sheria za Ubelgiji haziruhusu kuningíniza bendera iwapo unamiliki floor moja tu. Isitoshe, kiutendaji, ubalozi wa Ubelgiji unalalamikiwa sana na watanzania waishio huko katika nchi za Ubelgiji, Luxemburg na Uholanzi. Haujitumi kabisa kihuduma na hata kuitangaza nchi ya Tanzania. Watanzania waishio Uholanzi wameshamlalamikia sana Balozi Mlay kuwa analaza mambo mengi japo wanajitahidi sana kumsukuma afanye kitu. Wakati mwingine Watz waishio uholanzi wanafanya kumbukumbu muhimu kama Nyerere day, Muungano, nk., na kumualika balozi ili kumchokoza tu afanye kitu. Wapi bwana!!! jamaa kalala tu! Anatuma wasaidizi!! Kukosekana kwa huduma za heating system kwenye floor hiyo ni dalili wazi za nje za kutowajibika kwa balozi. Sasa, unategemea nini! Ubalozi upo strategic area (makao makuu ya EU, ni kweli) lakini haujitumi!!! Una maana gani?
 
Mkuu Share sasa kwa maoni yako ya mwisho ni kwamba tuufungge ama tufanyeje maana bado tuna ongelea tatizo hatutaji solution Membe akurupuke usingizini ajue kwamba tunampa msaada wa shida ya jumba lile.
 
Mkuu Lunyungu, kuufunga ubalozi wa Brussels utakuwa uendawazimu. It is a strategic area, na inauwakilisha Tanzania kwenye nchi tatu. We are just sending live signals to Membe kuwa watchful na balozi zake, utendaji wao wa kazi na jumba lenyewe.
 
Hivi hizi balozi si zinatengewa bajeti yake kila mwaka wa fedha?Sasa huyo balozi ameshindwaje kuchota pesa kidogo ili afanye ukarabati wa hiyo heating system?
Sisi watanzania ni lini tutakuwa wazalendo jamani?Mtu unapewa kazi nzuri,unalipwa vizuri bado una vi opportunity vya kufanya mambo yako,sasa unashindwaje kutekeleza kazi za watu kwa ukamilifu?
 
Wacha basi tusikie wenzetu wa huko watasemaje juu ya Ubalozi kuwa on ama off kisa heating system .Hivi ni ofisi za Ubalozi tu ama jengo zima ambapo upo Ubalozi wetu ?
 
Bado sitakaa niamini kwamba ubalozi umeshindwa kuja na quick fix katika tatizo la heating (hata kwa kutumia fedha za visa) kama ni kweli basi mungu epushia mbali, mana next time tutaambiwa ubalozi hauna fedha za kukata nyasi upenuni mwake.
 
Nadhani hili ni suala zaidi la kiutawala wa ndani ya ubalozi wenyewe. Kama wanashindwa ku keep up na bills za gas kazi kweli kweli....
 
Hahaha kwa mara ya kwanza naona Nyani ameamua kuingia mtini bila kujibu post ya mtu doh sijui mmemshika pabaya!!!!! nafikiri atakuja kujibu hii ya kwangu
 
kwa upande wangu ,naona maswala mingine sio lazima ambiwe waziri membe kama ya 'central heating system' kwasababu balozi yupo na naamini anaweza kulishughulikia tatizo hilo.hata kama utamtumia ujumbe membe ataupuuza tu kwasababu mambo madogo kama hayo balozi anaweza kabisa kutatua tatizo hilo bila hata ya membe!
 
I think it can be very serious kama ubalozi utafungwa for not having heating system halafu bado tukadhani Membe na JK hawapaswi kujua .Ufike mahali ufunge ubalozi kwamba baridi imezidi ndani watu wakose huduma bado wadhani ni utani huu ?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom