Membe sasa apania Kuvunja muungano

Tusitake kupotosha Ukweli tuwe honest Shinyanga ni Mkoa na zanzibar ni sehemu ya muungano ,Hoja ya ogwari ni ya msingi and it look kuna tatizo kubwa Foreign ,State house na Wezi wa protocol.Ni mwenye fikra finyu tu ndiye anayeweza kulinganisha Kigoma, Kagera na Zanzibar. Zanzibar ni Nchi ina Rais , Mawaziri ila hawana wizara ya mambo ya Nje ,kulingana na katibu ya Jamhuri ya Muungano kuna wizara ambazo zitakuwa chini ya serikali ya mapinduzi Zanzibar na kuna wizara zitakazokuwa chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Membe hawezi hakakwepa hizi lawama anahusika moja kwa moja na Hili suala .Solution ni Kihipa kura CDM muachane na Magamba yote CUF na CCM
mkuu chadema hawakwenda zanzibar hata kwenye kampeni, si ndo watazidi..wao hawaitambui zanzibar

Alivyokuja Amiri wa Qatar Zanzibar. Hatujalalamika hakufika bara.

Dhis iz veri konfyuzing.
Kama wazazibar wana wimbo wao wa Taifa, bajeti, KMKM, Rais na kadhalika zote, kwa nini wasimwalike kiongozi yeyote wanaemtaka? Wanaweza hata kumpa Gadaff hifadhi ya kisiasa kama wanapenda.

Unajua hapa tatizo ni muumdo huu wa muungano tulio nao, nchi mbili zimeungana na kuwa nchi moja na kanchi kadogo! Sasa hapo ndio kuna shida kama zingeungana nakuwa nchi moja kamili swali lako lingepata majibu lakini sasa hapo hakuna jibu maana zanzibar wana wimbo wao, bendera yao na mizinga, bara nako vivyo hivyo

Hii point nadhan haina maana sana,ni kweli kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, na lengo hawa watu ni kutembelea Tanzania ambayo ni kubwa, na tunajua kabisa tulipoungana tulikubaliana kuwa na makao makuu ya serikali ya Muungano ambayo ni Dar es Salaam, sasa wanapokuja lengo lao ni kuonana na viongozi wa serikali ya Muungano na kukagua miradi wanayoona inafaa, kwa kuonana na viongozi ni wazi watafikia Dar, na ukaguzi wa miradi inategemea mradi uko wapi kama uko Zanzibar watakuja kama upo Dar wataishia Dar kama uko Pwani wataenda kama alivyofanya mama Clinton, sasa unataka wafike zanzibar kwa sababu tu ni sehemu ya Muungano? Au waje kwa sababu gani?

Marekani pamoja na kuwa ni muungano wa majimbo mengi wageni wa kitaifa wanapofika hawatembelei majimbo yote, wataenda kule dhamira yao inapowatuma, kwa nini hamjahoji baadhi ya wizara za Muungano zisiwe na ofisi Zanzibar.

waziri wa mambo ya Nje na usirikiano wa kimataifa Bernard membe sasa ameonyesha dhairi ana mikakati ya siri ya kuvunja muungano kwa kuinyima zanzibar fursa ya kutembelewa na viongozi wa kimataifa pindi wanapofanya ziara Nchini .Sisi wazanzibar tunasikitishwa na kitendo cha waziri membe kuweka utaratibu mbaya wa kutoleta viongozi wa kimataifa zanzibr tunafahamu ana ajenda ya siri na akuanza leo ameanza siku nyingi mifano ipo hai akiwa ofisa mwandamizi wa ubalozi wa Tanzania Itali aliwahi kukataa kukutana na wanafunzi wa kizanzibar waliokuwa wakisoma Italy kwa madai kuwa yeye sio mzanzibar na mambo ya Zanzibar hayamhusu.

Viongozi waliotembelea Tanzania bila kufika Zanzibar na Nchi zao kwenye mabano ni Rais wa Marekani (George Bush) Rais Hu Jintao wa (China) Rais Abdulah Gur (Uturuki) Waziri Mkuu wa India Mohan Singh na waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton hawa viongozi wote wamefika Tanzania hakuna hata MMoja aliyefika zanzibar

Kuna mikoa mitano Zanzibar na mingine 20+ Tanzania Bara. Yot ekwa ujumla inaunda nchi inaitwa TANZANIA!! Hao viongozi unaowasema wamekuja kutembelea TANZANIA, wengi wao wanishia Dar es Salaam tu (ambako Rais wa Tanzania yupo)...wakifika kwingineko ni sehemu ya Tanzania!!
Umeshawahi kusikia MTANZANIA wa Kigoma, au Rukwa, au Manyara akilalamika kwamba serikali haipeleki viongozi hawa kwenyemikoa yao??
Hebu acha hoja zisizo na tija, tuko busy na Bunge

Kama foreign affairs is one of union matters,sasa kwa nini Zanzibar iwe na status tofauti na ile ya Tanganyika?kama amekuja ikulu ya Tanzania maana yake amekuja Tanzania ikiwemo na Zanzibar in respect of foreign affairs perspective.My take then Membe hapaswi kulaumiwa kwa hili!!!
Kweli, Membe hajakosea popote!

waziri wa mambo ya Nje na usirikiano wa kimataifa Bernard membe sasa ameonyesha dhairi ana mikakati ya siri ya kuvunja muungano kwa kuinyima zanzibar fursa ya kutembelewa na viongozi wa kimataifa pindi wanapofanya ziara Nchini .Sisi wazanzibar tunasikitishwa na kitendo cha waziri membe kuweka utaratibu mbaya wa kutoleta viongozi wa kimataifa zanzibr tunafahamu ana ajenda ya siri na akuanza leo ameanza siku nyingi mifano ipo hai akiwa ofisa mwandamizi wa ubalozi wa Tanzania Itali aliwahi kukataa kukutana na wanafunzi wa kizanzibar waliokuwa wakisoma Italy kwa madai kuwa yeye sio mzanzibar na mambo ya Zanzibar hayamhusu. Viongozi waliotembelea Tanzania bila kufika Zanzibar na Nchi zao kwenye mabano ni Rais wa Marekani (George Bush) Rais Hu Jintao wa (China) Rais Abdulah Gur (Uturuki) Waziri Mkuu wa India Mohan Singh na waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton hawa viongozi wote wamefika Tanzania hakuna hata MMoja aliyefika zanzibar
Kwani Zanzibar sio tanzania? Punguzeni unafiki!

Uvunje kabisa, hata sis tunataka Tanganyika yetu. Usanii mtupu. Muungano gani wa kumeza nchi moja.

wadanganyika ni waoga na wanafiki wakubwa na wapo kama watumwa. Kwani siku zote hawataki kujinasibu kutokana na nasaba zao za utanganyika. Ni watu wanaorubuniwa kidogo tu na kukubali kuuza utaifa wao. Ndio maana tunawaita wadanganyika.

Ndio maana wanashikwa kigugumizi kudai serikali yao ya tanganyika kama walivyodai wazanzibari. Ni kama makondoo tu
na wew ni kondoo pia au wewe ni mbuzi mkuu????

Msijitie Ubabaifu Zanzibar ni Nchi kamili ilipokubaliana Mambo ya Nje kuwa ni ya Muungano, yualikuwa yawe sawa kwa sawa kwa maslahi ya pande zote.Kwani zilizoungana ni Jamhuri ya Wati wa Zanzibar na Jamhuri ya Watu wa Tanganyika, sio Ukerewe au Tukuyu kama mnavyodhihaki. Kwa kipindi kirefu tumeshuhudia Viongozi wa Kitaifa wanapofika hapa Tanzania kwa ziara Rasmi basi japo kwa Mchana mmoja Wakipelekwa Zanzibar kwa ajili ya Kuonana na Viongozi wakuu na Wananchi wakipata Fursa ya Kupokea Mgeni wao.Ila sasa huyu Membe hili kaliuwa yeye ndie Mhusika Mkuu wa kuan daa utaratibu, ilikwa ishafika pahala pa kuwa Zanzibar ni Kero tusiende mbali kwani Muungano huu sio wa maisha na TUUVUNJE

1.KAMA UMETEMBELEA UNGUJA NA PEMBA UTAGUNDUA KUWA KUNA MAMBO MUHIMU WAZANZIBARI WANAPASWA KUYAZUNGUMZIA KUHUSU
MUUNGANO,LAKINI HAWAYASEMI.SIKU ZOTE HUZUNGUMZIWA MAMBO MADOGO.
2.KWA MAWAZO YANGU,HUENDA WAZANZIBARI WANAFIKIRI WATAKUWA NA MAENDELEO ZAIDI WAKIWA KIVYAO,HII NI KUTOKANA NA MISAADA WATAKAYOPATA TOKA KWA WAARABU.LAKINI WAARBU PIA WANA MATATIZO YAO LABDA UKUBALI UWE MTUMWA.
3.KWA MTAZAMO WANGU ZANZIBAR IMEKUWA IKIPENDELEWA MNO KWENYE HUU MUUNGANO KULIKO TANGANYIKA.KI UKWELI TANGANYIKA HAIPO ILA ZANZIBAR IPO,HAPO ALIYOPO NI LAZIMA AFAIDI ASIEKUWAPO ATAFAIDIJE????IVI WAPEMBA WANGAPI WAPO DAR NA WAKAZI WANGAPI WA DAR WANAFANYABIASHARA PEMBA???
4.SIKU ZOTE UMOJA NI NGUVU,SIELEWI NCHI ZILIZOUNGANA HALAFU ZIKAJITENGA SASA HIVI MAENDELEO YAO YAKOJE?
5.NADHANI KUNA WATU,NCHI,AU VIKUNDI WANAFIKIRIA KUITUMIA ZAIDI ZANZIBAR KWA MASLAHI YAO.LAKINI NI VIGUMU KUITUMIA ZNZ IKIWA NDANI YA MUUNGANO.SOLUTION .....IJITENGE.
6.TUTATUE MATATIZO YETU YA MUUNGANO KWA NJIA MUAFAKA HAINA HAJA YA KULUMBANA WALA KUKASIRIKIANA,SISI NI NDUGU NA WAMOJA.

Kwa kipindi kirefu sana zaidi ya miaka 45 tumeshuhudia Kuongezeka kwa kero za Muungano kiasi ambacho kila upande wa Muungano huu kumekuwa na malalamiko, sio aibu wala sio dhambi kwa sasa kusema basi tumechoka na lawama hizi na Tuuvunje Muungano huu kwa salama na amani. Haitokluwa sisi ni kama wa kwanza wenzetu tena Waafrika kama sisi waliojaribu kufanya Miungano ilikuwa na baadae ikavunjika {Senegal/ Gambia} hata jina liliitwa SENEGAMBIA, leo kila Mmoja yuko kwake na Shuguli zake zikenda mwezi kesho tutashuhudia Sudan ya Kusini ikiwa inaendesha mamlaka yake rasmi kama Dola Huru dhidi ya Sudan ya Kaskazini. Wakati umeshafika wa Kuuvunja Muungano huu wa Kidhulma, kindamizaji, dhidi ya Watu Wa Zanzibar, hakuna manufaa wala faida iliopatikana ndani ya Muungano huu ila ni hasara tu kwa upande wa Zanzibar, faida ilionjema ipo kwa upande wa Tanganyika iliofichwa nyuma ya pazia la Tanzania na hasidi mkubwa wa Zanzibar Julias Nyerere na Wenzake akina Kambona, Paul Rupia, Rashid Kawawa, Buke Munaka nk walikuwa na nia mbovu sana na ya hadaa ya Kummaliza kisiasa Mzee Karume Kwa kumpelekea mawazo hadaa ya kufanywa kwa Muungano nashukuru Karume m toto hayo ameyatambua na kabla haja maliza uongozi wake alihakikisha kuwa anafanya Marekebisho ya KATIBA na Kuweka katika Katiba ya Zanzibar Kuwa sasa inatamka kama ZANMZIBAR NI NCHI ILIONA MIPAKA YAKE KAMILI YA ARDHINI NA BAHARINI

waziri wa mambo ya Nje na usirikiano wa kimataifa Bernard membe sasa ameonyesha dhairi ana mikakati ya siri ya kuvunja muungano kwa kuinyima zanzibar fursa ya kutembelewa na viongozi wa kimataifa pindi wanapofanya ziara Nchini .Sisi wazanzibar tunasikitishwa na kitendo cha waziri membe kuweka utaratibu mbaya wa kutoleta viongozi wa kimataifa zanzibr tunafahamu ana ajenda ya siri na akuanza leo ameanza siku nyingi mifano ipo hai akiwa ofisa mwandamizi wa ubalozi wa Tanzania Itali aliwahi kukataa kukutana na wanafunzi wa kizanzibar waliokuwa wakisoma Italy kwa madai kuwa yeye sio mzanzibar na mambo ya Zanzibar hayamhusu.

Viongozi waliotembelea Tanzania bila kufika Zanzibar na Nchi zao kwenye mabano ni Rais wa Marekani (George Bush) Rais Hu Jintao wa (China) Rais Abdulah Gur (Uturuki) Waziri Mkuu wa India Mohan Singh na waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton hawa viongozi wote wamefika Tanzania hakuna hata MMoja aliyefika zanzibar

Hilo la Kutembelewa na Wageni Mbona Dogo ni Komaza Muungano!
Vipi Muungano ulivyokomaa kwa Zanzibar kuwa na Bendera,Wimbo wa Taifa na Katiba inayosema bila Woga kwamba Zanzibar ni nchi Huru!!
Hapa Vip?

Back
Top Bottom